Tabia za Makondakta zinazonikera

Tabia za Makondakta zinazonikera

Kama najua napaswa kuwalipia wangapi sina haja kukusubiri uniulize.
Nisipokuambia na wewe ukaona jamaa hajipapasi mdai ili ajipapase.

Huwa tunakutana na ile mtu anakupa hela unahangaika kutafuta chenji, ukishampa anakuambia kata wawili, sasa kwa nini hukusema mwanzoni?

Kukwepa hii adha inabidi nikuulize mapema.
 
hahaha siwapendi makonda mmetunyanyasa enzi tunasoma acheni tuwadharau ni haki yenu mpaka mnyoooke tu ina diamond'voice

Hivi nyie mnajua kama baba zenu wanataka hesabu ile ile bila kujali umebeba madent wangapi!

Katika kuhakikisha hesabu inatimia inabidi tupunguze idadi yenu nyie madent na nauli zenu za robo bei.
 
Hivi nyie mnajua kama baba zenu wanataka hesabu ile ile bila kujali umebeba madent wangapi!

Katika kuhakikisha hesabu inatimia inabidi tupunguze idadi yenu nyie madent na nauli zenu za robo bei.

sheria ni wanafunzi watano sometime nyie mnasukuma watoto afu hambebi hata mmoja
 
sheria ni wanafunzi watano sometime nyie mnasukuma watoto afu hambebi hata mmoja

Unajua nyie pia mnazingua mkitupush huwa mnajazana kwenye gari.

Imagine ungekuwa wewe bado ungefanya hivi hivi tu.
 
"Una mia nikupe mia mbili?"

Kuna abiria anakuwa na chenji kamili ila nauli anatoa buku 10. Mi huwa nawakomeshaga kwa kuwapa sarafu nyiingi, hapo utakuta anasema nirudishie hiyo nikupe chenji.
 
Abiria;Konda naomba chenchi yangu..
Konda;(kwa sauti kubwaa)aah subiri nakupa mia yako..si mia tu..!!
 
Mkuu kuna haja gani ya kuuliza ukate wangape pindi unapopewa hela kubwa? Ni lazima kumlipia mtu?

Ni kweli kuna baadhi ya abiria ambao huwa wanawakera makonda pamoja na abiria wenzao lakini kwa ujumla makondakta wamezidi kuwa kero.
Kwa uzoefu wangu na kazi ya ukonda ni mara chache sana kukuta abiria ambao wapo pamoja kimaongezi kila mmoja kulipa nauli yake...tena utasikia anamwambia mwenzake ngoja tu nilipe.......lakini hata hivyo kuna haja gani ya kumtukana mwenzio kwa swali kama hilo wakati jibu lake ni jepesi tu...otherwise uwe umeshavurugwa tangu huko kwako.....na ukaamua kuzihamishia hasira zako kwa konda..........
 
KikulachoChako umenikumbusha enzi hizo, nilikuwa konda wa ruti ya Kimara Posta, siku ya siku mama mmoja akapandia Akiba, nauli ilikuwa 200 tu kufika posta (route yote ilikuwa sh 300).

Wakati wa kushuka mi namdai nauli yeye ananidai chenji eti anadai kanipa sh 5,000/-, mi nikamwambia sijapokea chochote kutoka kwako, abiria wengine wakaanza kunishambulia eti sisi makonda ndo tabia zetu, sasa yule mama nikamuuliza ilikuwaje kwanza utoe hela kubwa vile kwa sh 200 tu, akasema hana hela nyingine yoyote na kwa hasira akataka kuvua nguo eti nimsachi.

Baada ya abiria kupiga sana yowe nikamwambia suka peleka gari central police, tulivyofika tukatoa maelezo ya kina, kuja kumsachi yule mama alikuwa ana sh 500 kama ishirini hivi kazichimbia kwenye mfuko wa nguo ya ndani. Tulimwacha police na sijui nini kiliendelea.
Nafikiri alisema hana hela ndogo kwasababu alikuwa amezificha mbali ili pengine asiibiwe na akawa amebakisha hiyo elfu tano kwa ajili ya nauli na mambo mengine madogomadogo.
 
Nafikiri alisema hana hela ndogo kwasababu alikuwa amezificha mbali ili pengine asiibiwe na akawa amebakisha hiyo elfu tano kwa ajili ya nauli na mambo mengine madogomadogo.

Kwa nini alisema hana hela kabisa? Na akatishia kusaula, ila kwa vile alikuwa mmama mtu mzima watu walipiga kelele sana.

BTW, ile kazi ni ngumu bana, kila nikikumbuka masahibu ya ukonda nawaonea huruma jamaa.
 
Ukimwambie asiongeze abiria wengine ndani kuna joto "anakwambia ungepanda friji"
Anakudnganya kuna siti ukipanda unakuta hamna ukimuuliza anakujibu "ungekuja na stuli toka nyumbani"

SINA IMANI NA UKAWA

Na wewe ungemwambia mbona gari lina friji (AC) ila ikatengezwe.
 
Huwa tunakutana na ile mtu anakupa hela unahangaika kutafuta chenji, ukishampa anakuambia kata wawili, sasa kwa nini hukusema mwanzoni?

Kukwepa hii adha inabidi nikuulize mapema.
Abiria wa namna hii ni wasumbufu kwakweli, na hii haina maana kwamba abiria wote ni wastaarabu.
 
sipendi konda anapitisha mkono kuchukua nauli kwa abiria aliyekaa nyuma yangu huku kwapa lake likiwa kichwani kwangu,wengi wao makwapa yao yananuka
 
Unampa hela ya nauli anakuuliza,"una 100???"
Kama hauna unasubirishwa chenchi na usipodai hupati hiyo100
Wengine bila aibu et 100 tu unadai?
Gongo la mboto - mnazi mmoja wanakuuliza una hamsini??
 
sheria ni wanafunzi watano sometime nyie mnasukuma watoto afu hambebi hata mmoja
Wanafunzi wanaopata shida zaidi ni wale wa shule za msingi,wa sekondari angalau wanajitahidi kupambana na makonda.
 
Back
Top Bottom