Tabia mbili mbaya ambazo tumegoma kabisa kuziacha

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,715
Nsikuchoshe na usinchoshe, tusichoshane!


Kuna tabia ambazo miongoni mwetu kama watanzania tumegoma kabisa kuziacha,sijui ni lini zitafikia tamati.Mimi ni mtu ambaye nakerwa sana na hizi tabia za kipumbavu.

Leo nitaanza na hii tabia ya kwanza ambayo huwa inakera sana.

TABIA - 1

Familia au Ukoo wenu mnapatwa msiba wa moja wa ndugu yenu, sasa wewe baada ya kupata taarifa ya msiba unapanga kwenda msibani.

Unakuta msiba umetokea eidha Bukoba/Mwanza/Kigoma au Sumbawanga, tunaelewa kabisa kutoka Dar es Salaam hadi kwenye hiyo mikoa niliyoitaja nauli yake si chini ya elfu 60, sasa wewe unakwenda msibani na ukifika badala ya kushiriki kwenye msiba kwa kutoa michango itakayowezesha ununuzi wa mahitaji muhimu, wewe kwa nyodo na dharau unaanza kusema huna hela umebaki na nauli tu ya kukurudisha,mbaya zaidi hata ukitoa unatoa kama umelazimishwa na pesa yenyewe haizidi elfu 20, sasa aliyekwambia utumie gharama kubwa kwenda msibani ni kitu gani kama huwezi kutoa michango?.

Hiyo pesa uliyotumia kama nauli kwanini usingeituma ili manunuzi yafanyike msibani kuliko kubeba li tumbo na makalio yako makubwa kupeleka msibani? Kwani ukituma hela ikatumika kwa mahitaji muhimu hapo msibani halafu wewe ukaenda baadae hata kuona tu kaburi la ndugu yako utapungukiwa na nini? Kama huna hela ni vema ukatuma hiyo ambayo umepanga kuitumia kama nauli kuliko kwenda msibani halafu usitoe mchango.Msiba wowote ule jambo la kwanza ni fedha ya mahitaji muhimu na muache porojo za vijiweni kwamba uwepo wako ni muhimu kuliko fedha,uwepo wako utakua muhimu kama ukitoa fedha na kama hutotoa fedha(Mchango) wala usijidanganye kuhusu uwepo wako.Usipotoa mchango utaacha watu wakujadili wewe na ndugu zako kwenye vikao visivyo rasmi.

Mfano.

Watu "Ina maana wafiwa hawana hela hata ya kununua ng'ombe wa kuchinja?"

Watu "Ina maana wameshindwa kununua hata jeneza la laki 5?mbona marehemu hawamfanyii fea jamani?

Watu "Jamani wameshindwa hata kutoa picha kubwa ya marehemu ikae hapa mbele ya Jeneza?"

Watu "Kati ya misiba ambayo haiko Organized ni huu,yaani hata maji ya kunywa tu hakuna"


Haya mambo bila michango hayawezekani na ndiyo maana naandika mbadirike Hebu badilikeni na muache hizi tabia za kijinga.

Msiba unakuta unatumia bajeti kubwa kwasababu ya kulisha watu ambao wakiambiwa watoe michango wanakuwa wakali,yaani mtu afiwe na ndugu yake halafu awaze na kukulisha? Kwanini hamtaki kubadilika?.

Unakuta mtu alikuwa hataki kutoa hela ya matibabu wakati wa ugonjwa wa marehemu lakini baada ya kufa ndipo atachukua ka gari kake uchwara ka Harrier tako la nyani na kuweka mafuta zaidi ya laki 5 kwenda msibani kujionyesha kwamba amenunua gari,aliyekwambia msibani ni sehemu ya maonyesho nani?,Hako ka gari kako kama unataka maonyesho kwanini usikapeleke kwenye mashindano ya Urembo na ulimbwende au pale Sabasaba ili kila mtu aone?,Hivi huu ujinga baadhi yenu mtaacha lini?,Hela ya matibabu ulikuwa ukiambiwa utoe unakula kona huku ukitoa sababu lukuki,ila mgonjwa ameshafariki sasa ndiyo utajibeba wewe na familia yako kwenye hako ka Prado/Raum kako hadi msibani ili muonekane waungwana kumbe ni uozo mtupu!.

Msibani tunataka michango hatutaki kuja na vigari vyenu uchwara hivyo,kama hutaki kutoa michango ni heri usije msibani ukaacha wananzengo wakapambana,siyo unakuja umetunisha tumbo lako mbele ili kujionyesha kwamba umeyapatia maisha kumbe ni uozo mtupu!.

Acheni sifa kwenye misiba ya watu.

Unapanda ndege kwenda Bukoba msibani ukifika ukiambiwa utoe mchango ili kuwezesha shughuli za msiba wewe unatoa elfu kumi!,Hivi kweli uko serious?,Aliyekwambia hiyo elfu kumi mwananzengo wa pale Katerero,Kibeta au Kahororo ameshindwa kutoa ni nani?, Aliyekwambia mwananzengo wa mitaa ya Igoma,Nyashishi,Buhongwa au Kisesa hiyo elfu kumi ameshindwa kutoa ni nani?Aliyekwambia mwananzengo wa mitaa ya Mkendo,Nyasho,Kamnyonge,Makoko,Buhare au Bweri ameshindwa kutoa elfu kumi ni nani?,Aliyekwambia mwananzengo wa mitaa ya Ngarenaro,Usa river,Kikatiti,Kijenge au Kisongo ameshindwa kutoa elfu kumi ni nani?Aliyekwambia mwananzengo wa mitaa ya Butunga,Gungu,Kibirizi au Mwanga ameshindwa kutoa elfu kumi ni nani? yaani upande ndege ya laki 5 halafu msibani uje uchangie elfu kumi?,Hivi unaakili timamu kweli?,tulitegemea uchangie walau milioni 1,halafu bila aibu wakati wa kupiga soga na ndugu unaanza kujisifia kwamba umekuja na ndege ili watu wakuone uko matawi ya juu!,Huu upumbavu hebu uacheni na mbadirike wapuuzi nyie.

Hivi kweli unatoka Dar es salaam unakwenda msibani kunywa pombe?,yaani umeshindwa kutoa hela ya mchango lakini baadae unatafuta ndugu baadhi mnaoshibana mnaelekea kwenye mabaa kunywa pombe!,yaani umetoka kabisa Dar es salaam na fungu la pesa uliloandaa kwa ajili ya kura raha na kupiga starehe,na huishii hapo tu bali utaenda mbali zaidi na kutafuta malaya na kulala nao?,Hivi hizi nguvu wakati wa msiba wa ndugu yako unazitoa wapi? Yaani watu wanalia kuhusu michango na inapelekea wanashikana mashati kwa kukamuana lakini wewe huna habari unakunywa pombe,tena pombe unakuta unatumia si chini ya milioni 1 kununulia marafiki na ndugu wapumbavu lakini kwenye mchango umetoa elfu 20 tu bila aibu!.Hizo pesa za pombe kwanini usingemuachia mfiwa akabaki anakukumbuka?,Aliyekwambia kununulia wajinga wenzio pombe wakati wa msiba utapewa shukurani nani?.

Nauliza tena,kwanini hamtaki kubadirika?

Hivi hizi tabia za kijinga mtaacha lini?

Haya,unakuta umefika msibani lakini hata kujishughulisha na shughuli walau za kuchota maji,Kupanga viti,kupasua kuni,kuosha vyombo au kupika wewe hutaki,kila unachoambiwa wewe unasema umechoka,hivi hapo msibani ulienda kufanya kitu gani kama hata kazi ndogo kama hizo huwezi?,Nani alikwambia msibani hapo wanashida na hilo dera lako lililopauka?,Nani alikwambia hapo msibani wana shida na hiyo miwani koko yako?,Nani alikwambia hapo msibani wana shida na hilo wigi lako chafu?,Nani alikwambia hapo msibani wana shida na hizo kucha zako ndefu kama misumari?,Nani alikwambia hapo msibani wanashida na hako ka Iphone kako uchwara?,Nani alikwambia hapo msibani wanashida na huo weupe wako wa mkorogo?,Nani alikwambia hapo msibani wanashida na hizo Sangita/yeboyebo ulizosuka kichwani?

Watu wanataka msaada wa kikazi ili mambo yakamilike mapema ila wewe unaleta ujuaji wa kijinga.Hebu acheni huu upumbavu,badirikeni!.

Unakuta wengine msibani ndipo sehemu za kuonyesha fasheni ya mavazi,hivi huu muda unautoa wapi?,kweli umefiwa na ndugu yako kipenzi huo muda wa kubadili nguo kila dakika unautoa wapi?.


Wengine msibani ndipo panakuwa sehemu ya majungu na Uongo wa kujadili wake za watu.Uongo wako mpelekee mumeo au Mkeo,msibani si sehemu ya huo ujinga.


Ni hayo tu.
 
Unajua maana halisi ya kuzika mkuu???

tunaenda msibani hasa tukisukumwa na upendo kwa wapendwa wetu. Tunaenda kuwazika.

Maisha yetu haya unayajua ni utoke leo ndio upate hela ya kula. Wakati mwingine unapigiwa simu ya msiba ukiwa na akiba kidogo sana. Inabidi nyingine ukakope upate nauli huku nyuma uiachie familia kidogo wasije lala njaa.
 
Wachaga lazma wakuparue ,,

Ukweli usemwe TU kwenda msibani then unapikiwa pilau nyama soda na maji wakat umechanga 10k Ni Dhambi kubwa sana ,,,yaan umechanga hela kidogo halafu unakula msosi wa gharama kubwa na ubaya ukute unalala msibani siku 3 ,,Wallah Dhambi na dhulma sana
 
Wachaga lazma wakuparue ,,

Ukweli usemwe TU kwenda msibani then unapikiwa pilau nyama soda na maji wakat umechanga 10k Ni Dhambi kubwa sana ,,,yaan umechanga hela kidogo halafu unakula msosi wa gharama kubwa na ubaya ukute unalala msibani siku 3 ,,Wallah Dhambi na dhulma sana
Wao ngoja waniparue mkuu lakini ukweli lazima usemwe!.
 
Unajua maana halisi ya kuzika mkuu???

tunaenda msibani hasa tukisukumwa na upendo kwa wapendwa wetu. Tunaenda kuwazika.

Maisha yetu haya unayajua ni utoke leo ndio upate hela ya kula. Wakati mwingine unapigiwa simu ya msiba ukiwa na akiba kidogo sana. Inabidi nyingine ukakope upate nauli huku nyuma uiachie familia kidogo wasije lala njaa.
Ni jambo jema ukaituma hiyo kidogo ikasaidia masuala ya hapo msibani,wewe utajipanga utakwenda siku nyingine kumsalimia mfiwa na kama umeamua kwenda inapaswa ujiandae kikamilifu kwa suala la michango.

Huo ndiyo ukweli
 
Ni jambo jema ukaituma hiyo kidogo ikasaidia masuala ya hapo msibani,wewe utajipanga utakwenda siku nyingine kumsalimia mfiwa na kama umeamua kwenda inapaswa ujiandae kikamilifu kwa suala la michango.

Huo ndiyo ukweli
Ni dharau sana mkuu eti usiende uwaambie sina pesa natuma hii laki moja itawasaidia... Aiseeh utakuwa umeonyesha dharau kubwa sana kwa marehemu na wafuwa yaani kana kwamba umeweka pesa mbele badala ya utu.

Hivi kila mtu atume pesa asiende huwo msiba utakuwaje? Uwepo wako ww pale pia unawapa faraja wafiwa.
 
Ni dharau sana mkuu eti usiende uwaambie sina pesa natuma hii laki moja itawasaidia... Aiseeh utakuwa umeonyesha dharau kubwa sana kwa marehemu na wafuwa yaani kana kwamba umeweka pesa mbele badala ya utu.

Hivi kila mtu atume pesa asiende huwo msiba utakuwaje? Uwepo wako ww pale pia unawapa faraja wafiwa.
Uwepo wako ni muhimu lakini mchango wako wa fedha ni muhimu zaidi mkuu
 
Nsikuchoshe na usinchoshe,tusichoshane!


Kuna tabia ambazo miongoni mwetu kama watanzania tumegoma kabisa kuziacha,sijui ni lini zitafikia tamati.Mimi ni mtu ambaye nakerwa sana na hizi tabia za kipumbavu.

Leo nitaanza na hii tabia ya kwanza ambayo huwa inakera sana.

TABIA - 1


Familia au Ukoo wenu mnapatwa msiba wa moja wa ndugu yenu,sasa wewe baada ya kupata taarifa ya msiba unapanga kwenda msibani.

Unakuta msiba umetokea eidha Bukoba/Mwanza/Kigoma au Sumbawanga,tunaelewa kabisa kutoka Dar es salaam hadi kwenye hiyo mikoa niliyoitaja nauli yake si chini ya elfu 60,sasa wewe unakwenda msibani na ukifika badala ya kushiriki kwenye msiba kwa kutoa michango itakayowezesha ununuzi wa mahitaji muhimu,wewe kwa nyodo na dharau unaanza kusema huna hela umebaki na nauli,sasa aliyekwambia utumie gharama kubwa kwenda msibani ni kitu gani kama huwezi kutoa michango?.

Hiyo pesa uliyotumia kama nauli kwanini usingeituma ili manunuzi yafanyike msibani kuliko kubeba li tumbo lako kupeleka msibani?,kwani ukituma hela ikatumika kwa mahitaji muhimu hapo msibani halafu wewe ukaenda baadae hata kuona tu kaburi la ndugu yako utapungukiwa na nini?,Kama huna hela ni vema ukatuma hiyo ambayo umepanga kuitumia kama nauli kuliko kwenda msibani halafu usitoe mchango.

Hebu badirikeni na muache hizi tabia za kijinga.

Msiba unakuta unatumia bajeti kubwa kwasababu ya kulisha watu ambao wakiambiwa watoe michango wanakuwa wakali,yaani mtu afiwe na ndugu yake halafu awaze na kukulisha?,Kwanini hamtaki kubadirika?.

Unakuta mtu alikuwa hataki kutoa hela ya matibabu wakati wa ugonjwa wa marehemu lakini baada ya kufa ndipo atachukua ka gari kake uchwara ka Harrier tako la nyani na kuweka mafuta zaidi ya laki 5 kwenda msibani kujionyesha kwamba amenunua gari,aliyekwambia msibani ni sehemu ya maonyesho nani?,Hako ka gari kako kama unataka maonyesho kwanini usikapeleke kwenye mashindano ya Urembo na ulimbwende ili kila mtu aone?,Hivi huu ujinga baadhi yenu mtaacha lini?,Hela ya matibabu ulikuwa ukiambiwa utoe unakula kona huku ukitoa sababu lukuki,ila mgonjwa ameshafariki sasa ndiyo utajibeba wewe na familia yako kwenye hako ka Prado kako hadi msibani ili muonekane waungwana kumbe ni uozo mtupu!.

Msibani tunataka michango hatutaki kuja na vigari vyenu uchwara hivyo,kama hutaki kutoa michango ni heri usije msibani ukaacha wananzengo wakapambana,siyo unakuja umetunisha tumbo lako mbele ili kujionyesha kwamba umeyapatia maisha kumbe ni uozo mtupu!.

Acheni sifa kwenye misiba ya watu.

Unapanda ndege kwenda Bukoba msibani ukifika ukiambiwa utoe mchango ili kuwezesha shughuli za msiba wewe unatoa elfu kumi!,Hivi kweli uko serious?,Aliyekwambia hiyo elfu kumi mwananzengo wa pale Katerero ameshindwa kutoa ni nani?,yaani upande ndege ya laki 5 halafu msibani uje uchangie elfu kumi?,Hivi unaakili timamu kweli?,tulitegemea uchangie walau milioni 1,halafu bila aibu wakati wa kupiga soga na ndugu unaanza kujisifia kwamba umekuja na ndege ili watu wakuone uko matawi ya juu!,Huu upumbavu hebu uacheni na mbadirike wapuuzi nyie.

Hivi kweli unatoka Dar es salaam unakwenda msibani kunywa pombe?,yaani umeshindwa kutoa hela ya mchango lakini baadae unatafuta ndugu baadhi mnaoshibana mnaelekea kwenye mabaa kunywa pombe!,yaani umetoka kabisa Dar es salaam na fungu la pesa uliloandaa kwa ajili ya kura raha na kupiga starehe,na huishi hapo tu bali utaenda mbali zaidi na kutafuta malaya na kulala nao?,Hivi hizi nguvu wakati wa msiba wa ndugu yako unazitoa wapi?,yaani watu wanalia kuhusu michango na inapelekea wanashikana mashati kwa kukamuana lakini wewe huna habari unakunywa ponbe,tena pombe unakuta unatumia si chini ya milioni kununulia marafiki na ndugu wapumbavu lakini kwenye mchango umetoa elfu 20 tu bila aibu!.Hizo pesa za pombe kwanini usingemuachia mfiwa akabaki anakukumbuka?,Aliyekwambia kununulia wajinga wenzio pombe wakati wa msiba utapewa shukurani nani?.

Nauliza tena,kwanini hamtaki kubadirika?

Hivi hizi tabia za kijinga mtaacha lini?

Haya,unakuta umefika msibani lakini hata kujishughulisha na shughuli walau za kuchota maji hutaki,kila unachoambiwa wewe unasema umechoka,hivi hapo msibani ulienda kufanya kitu gani kama hata kazi ndogo tu ya kupanga viti huwezi?

Hebu acheni huu upumbavu,badirikeni!.

Unakuta wengine msibani ndipo sehemu za kuonyesha fasheni ya mavazi,hivi huu muda unautoa wapi?,kweli umefiwa na ndugu yako kipenzi huo muda kubadili nguo kila dakika unautoa wapi?.


Wengine msibani ndipo panakuwa sehemu ya majungu na Uongo.Uongo wako mpelekee mumeo au Mkeo,msibani si sehemu ya huo ujinga.


Ni hayo tu.
Naona umeelezea vzr tabia 1, nyingine je.!?

H
 
Back
Top Bottom