Tabia za Makondakta zinazonikera

Tabia za Makondakta zinazonikera

I wish angetokea konda hapa naye akaeleza kero zake kuhusu abiria. Kuna abiria wanakera jamani mweh!
ABIRIA:
-Unakuta umepigania daladala hapo kitu darajani ubungo kwenda Gomz, ile kuingia tu unakuta eti abiria anadai kawahi siti huku kaweka kipochi au liboksi lake ktk siti kupitia dirishani, ukikaa anazusha!!
-jitu limekaa siti moja na wewe alafu linaongea ktk simu lwa sauti utadhani linaongea na mtu yupo Rorya.
-Safari ndefu ktk foleni, jimbaba linasinzia alafu linanilalia begani, SIPENDI KWELI.
 
ABIRIA: Unakuta umepigania daladala hapo kitu darajani ubungo kwenda Gomz, ile kuingia tu unakuta eti abiria anadai kawahi siti huku kaweka kipochi au liboksi lake ktk siti kupitia dirishani, ukikaa anazusha!!
Aaah mimi usintanie kabisa natoa kipochi nakaa unless otherwise niheshimu umri.
 
Kuna abiria anakuwa na chenji kamili ila nauli anatoa buku 10. Mi huwa nawakomeshaga kwa kuwapa sarafu nyiingi, hapo utakuta anasema nirudishie hiyo nikupe chenji.
Hapo uko sahihi kabisa.
 
  1. Abiria anapanda huku anajua ana hela pungufu, baadae ukianza kudai nauli yako anakupa hela pungufu, ukimmaind abiria wanaanza ooh hiyo mia tu si uachane naye, ukiwaambia wamlipie wanakaa kimya.
  2. Abiria unamwomba nauli anakwambia ntakupa nimekaa vibaya, umekaa vibaya kivipi? Leta nauli niende kudai wengine, ukijifanya kumsahau unamwona anataka kuondoka bila kulipa.
  3. Tabia ya abiria kuwapa makonda noti mbovu, ukiikataa anakwambia eti sina nyingine, na hapo mmeshafika mbali, jamani noti mbovu pelekeni benki
  4. Tabia ya mtu kupandia Kimara anakwambia eti nashukia Manzese ambapo nauli ni 400 (hapo kama route ya Posta ni sh 500), mkifika Manzese hashuki, ukianza kumdai nauli mpya anajifanya ooh sina, au nimebadili maamuzi nashukia Posta, sasa mbona hukunijulisha mpaka nimekukumbuka mimi?
  5. Tatizo la abiria kuingia kwenye gari ukimwambia sogea nyuma wenzio wapande anamaind, kama vipi tafuteni usafiri wenu.
  6. Harafu kuna hawa jamaa ambao wengi watakuwa ni member wa JF, kila akiingia kwenye gari anajifanya kupiga simu eti anaongea na fundi wake kuhusu gari lake lililoko garage ili aonekane matawi kwenye dala dala.
  7. Abiria analala gari inampitisha kituo, anaanza kulalamika eti konda hakuita vituo, ni jukumu lako kujua unashukia wapi, kama ni mgeni niambie mapema kwamba wewe ni mgeni.


mara nyingi sana kwenye daldala naona jinsi abiria wanavyosumbua makonda. mwingine unaona kabisa anatafuta ugomvi kitu kidogo tu matusi. kazi ya ukonda ngumu sana!
 
Abiria;Konda naomba chenchi yangu..
Konda;(kwa sauti kubwaa)aah subiri nakupa mia yako..si mia tu..!!
ha ha ha ha ha lengo la konda hapo inakuwa ni kumuaibisha anayedai mia yake au?
 
sipendi konda anapitisha mkono kuchukua nauli kwa abiria aliyekaa nyuma yangu huku kwapa lake likiwa kichwani kwangu,wengi wao makwapa yao yananuka
Yaaaan hadi nimesisimka baada ya kuvuta picha ya mazingira.
 
mara nyingi sana kwenye daldala naona jinsi abiria wanavyosumbua makonda. mwingine unaona kabisa anatafuta ugomvi kitu kidogo tu matusi. kazi ya ukonda ngumu sana!
Hayo ni matokeo ya kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya konda abiria.
 
Unakuta abiria wanaibiwa sana kwny daladala lakin kondakta anaela nyingi mfukoni lakin wezi hawamwibii kondakta hata kidogo
Au unakuta kondakta anasema abiria chunga mzigo wako hujue kuna wezi kwny gari wamepanda kondakta anawajua so anafurahi tu
 
unalipa nauli halafu baada ya muda konda anakugongea na mkono wenye silver,kekele hzo,balaa
 
Kwani mia pia si ni hela, mimi nadai kwa sauti "KONDA HIYO MIA MOJA YANGU VIPI UNATAKA NISAHAU"
Mkuu kuna wengine wakiona mtu anadai mia wanamshangaa eti ni hela ndogo wakati hiyo hiyo hela ndogo ukiikosa konda anakudhalilisha.
 
Ukisema makonda ni wachafu nitakuunga mkono. Lakini hili la chenchi linawahusu abiria na kondakta ambao lazima tuwasemee maana muda wa kuingia humu hawana. Ni asubuhi abia wanne wanatoa noti za sh. Kumi 10 sawa na sh 40, 000 wkt nauli ni sh 500?

Konda anatakiwa awe na float ebo!! ajiandae kabisa , si anajua biashara yake ni machenji chenji au? Ni kiasi tu cha kujiongeza . hapo wa kulaumiwa ni konda tu , kama unamtazamo wa mbali.
 
Konda anatakiwa awe na float ebo!! ajiandae kabisa , si anajua biashara yake ni machenji chenji au? Ni kiasi tu cha kujiongeza . hapo wa kulaumiwa ni konda tu , kama unamtazamo wa mbali.
Umenena vyema mkuu,baadhi wanasema eti unatoaje shilingi elfu kumi asubuhi.Sasa mimi nisipande gari asubuhi kwakuwa tu sina pesa ndogo? au nianze kuamsha majirani kuomba chenji? hapana ,hii mimi siikubali hata kidogo.
Kama konda hawezi kupambana na changamoyo zake ni bora tu awe mpiga ndebe.
 
Back
Top Bottom