Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu kujitolea ni jambo zuri sana ila pia inatakiwa uangalie huko kujitolea kwako kuna faida gani na hiyo faida ni yakuendelea au ni ya muda mfupi, watu wanasema ni heri ukampa mtu mbegu ya tunda kuliko tunda.
Tuendelee...
Hii kitu kusema ukweli haiingii akilini mwangu kabisa, jamaa wanakuja kwa mwezi hata mara 3 au zaidi na wanachinja ng'ombe, mbuzi, kondoo, yaani jumla inaafika 70 na zaidi kila mtu anapata nyama kg 1 mchele kg1 yaani hata mkitoka familia yote kwenu kila kichwa cha mtu kitapata hivyo; pia huwa inategemeana na siku hiyo kama kuna watu kiasi gani.
Na ni misikiti yote huko kijijini nilikotoka, huwa wanahama tu leo huku kesho kule.
Swali, wanatoa wapi hizi hela hawa Waarabu, au wametuona sisi tuna shida na nyama na wali kuliko elimu au vitu vingine?
Na je, ni kweli hao watu wanaowapa nyama shida yao ni nyama tu?
Na mwisho wake lini? Maana ndugu ukishuhudia hiyo mifugo inayochinjwa, lazima utajiuliza maswali mengi!
Nawasilisha akina nani, msije na hasira.