Tabia ya Waarabu kugawa nyama misikitini imekaaje?

Tabia ya Waarabu kugawa nyama misikitini imekaaje?

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
890
Reaction score
3,091
Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu kujitolea ni jambo zuri sana ila pia inatakiwa uangalie huko kujitolea kwako kuna faida gani na hiyo faida ni yakuendelea au ni ya muda mfupi, watu wanasema ni heri ukampa mtu mbegu ya tunda kuliko tunda.

Tuendelee...
Hii kitu kusema ukweli haiingii akilini mwangu kabisa, jamaa wanakuja kwa mwezi hata mara 3 au zaidi na wanachinja ng'ombe, mbuzi, kondoo, yaani jumla inaafika 70 na zaidi kila mtu anapata nyama kg 1 mchele kg1 yaani hata mkitoka familia yote kwenu kila kichwa cha mtu kitapata hivyo; pia huwa inategemeana na siku hiyo kama kuna watu kiasi gani.

Na ni misikiti yote huko kijijini nilikotoka, huwa wanahama tu leo huku kesho kule.

Swali, wanatoa wapi hizi hela hawa Waarabu, au wametuona sisi tuna shida na nyama na wali kuliko elimu au vitu vingine?

Na je, ni kweli hao watu wanaowapa nyama shida yao ni nyama tu?

Na mwisho wake lini? Maana ndugu ukishuhudia hiyo mifugo inayochinjwa, lazima utajiuliza maswali mengi!

Nawasilisha akina nani, msije na hasira.
 
Mimi sijaona tatizo wao wamenuia kutoa sadaka hofu yako ni nini? Kama unaogopa kula hizo nyama na michele achana nazo mkuu huku kwetu kuna maeneo kila jumapili lazima mbuzi walale watoto wa madrasa waule na ubwabwa, ikifika sikukuu pia hutoa ng'ombe kila kitongoji, ramadhani hutoa sadaka za ftar kwa watu,
 
Wao wamekuletea nyama na wali sasa kwann hizo shida zingine kama elimu na nyinyi simjitahidi kuzitatua nyinyi wenyewe?

Kwamba nyinyi waafrika mmekuja duniani kukaa tu na kusubilia kutatuliwa shida zenu zote na waarabu au wazungu?

Alafu kingine hawajakushikia bunduki kwenda kuchukua hizo nyama sasa sijui ww kinacho kuuma ni nn hasa.
 
Kama kilivyo kichwa cha habari hapo juu kujitolea ni jambo zuri sana ila pia inatakiwa uangalie huko kujitolea kwako kuna faida gani na hiyo faida ni yakuendelea au ni ya muda mfupi, watu wanasema ni heri ukampa mtu mbegu ya tunda kuliko tunda.

Tuendelee...
Hii kitu kusema ukweli haiingii akilini mwangu kabisa, jamaa wanakuja kwa mwezi hata mara 3 au zaidi na wanachinja ng'ombe, mbuzi, kondoo, yaani jumla inaafika 70 na zaidi kila mtu anapata nyama kg 1 mchele kg1 yaani hata mkitoka familia yote kwenu kila kichwa cha mtu kitapata hivyo; pia huwa inategemeana na siku hiyo kama kuna watu kiasi gani.

Na ni misikiti yote huko kijijini nilikotoka, huwa wanahama tu leo huku kesho kule.

Swali, wanatoa wapi hizi hela hawa Waarabu, au wametuona sisi tuna shida na nyama na wali kuliko elimu au vitu vingine?

Na je, ni kweli hao watu wanaowapa nyama shida yao ni nyama tu?

Na mwisho wake lini? Maana ndugu ukishuhudia hiyo mifugo inayochinjwa, lazima utajiuliza maswali mengi!

Nawasilisha akina nani, msije na hasira.
Hao ndo WAARABU, kugawa nyama, tende, kujenga misikiti NO ELIMU, matokeo yake jamaa zao wanaanza dai hati miliki za mali zetu (KCMC)
 
Ni sadaka tu haina shida yoyote

Kaka tunaomba ufafanuzi zaidi ETUGRUL BEY
Kwanza asante madam Firdaus9 Kwa kunialika hapa hakika ni heshima Sana kwangu,asante Sana

Ngoja nianze na Aya hizi za Allah

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ
Hakika tumekupa kheri nyingi.
فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ
Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.
إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ
Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu

Kuchinja ni moja ya ibada kubwa Sana ingawa watu wengi hawafahamu,kwahiyo wale ambao wanafahamu umuhimu wake huwa wanashikamana na ibada hizi na ndio sababu ya kuzidi kufanikiwa zaidi na ni sehemu ya kushukuru pia neema za Allah
 
Mkuu

Ni simple TU

Mungu wa waislam anagawa vitu KWA WATU Mbali Mbali!

Lakini Mungu anaehubiriwa kwenye makanisa Mengi anakusanya vitu KWA WATU!

Chunguza ulete mrejesho mkuu

Japo YESU aliegawa Sana KWA watu kama samaki wale na mikate lakini watumishi na makanisa Mengi ya kileo yanakusanya kuliko kugawa KWA watu!!!!

Chunguza kwa MAKINI nilichoandika Hapa!!
 
Mimi ni mkristo tena mkatoliki kiukweli waislamu ni wath wakarimu sana wenye utu na upendo japo mafundisho yao yanamkanganyiko sehemu flani waislamu wengi wenye vipato vikubwa wameweka mabomba ya maji nje ili watu wachote bure bila kugharamia chochote ata misikitini ila makanisa mengi siyo sehemu ya kurudisha kwa jamii wao wanapokea tu ila si kutoa na ikitokea tatizo kidogo wanalirudisha kwa waumini, makanisa mengi yana falsafa za kibepari kuliko ujamaa maanaa ujamaa umebeba utu,huruma na upendoo
 
it's a ritual among arabs, no free meal. nyuma ya pazia kuna mambo mengi yanafanyika kuhusiana na hizo nyama wanazogawa bure kwa waswahili.

waswahili na njaa zenu huwa hata hamjiulizi,mnapokea tu na kwenda kula na familia zenu.

kuna tajiri mmoja maarufu sana hapa tz(muarabu), kugawa nyama kwa wafanyakazi wake ni moja ya kafara zake. baadhi huwa hawapokei.
 
Back
Top Bottom