JACKLINE CELESTINE KITALE
Member
- Jul 29, 2021
- 81
- 158
Kisheria mtu anahesabiwa kuwa ni mtu mwenye haki mpaka pale ambapo mahakama ita thibitisha kuwa huyu mtuhumiwa amefanya kweli hayo makosa anayoshutumiwa kufanya.
Na kama mtu ambaye ametuhumiwa tu, ana haki zake sawa na raia wa kawaida tu, hivyo, hizo haki zinatakiwa ziheshimiwe mpaka pale itakavyo thibitishwa kinyume kwasababu wakati mwingine mtu huyo anaweza kuwa amesingiziwa au Ni chuki tu au Kuna mazingira ambayo yamefanya mpaka akamatwe lakini yeye hana kosa lolote lile.
Hivyo polisi wanatakiwa wamchukue kwa kuzingatia haki zakusubiri akisubiri hukumu.
Kitu cha kusikitisha ni kwamba hawa polisi wa Kitanzania huwa wakimkamata mtuhumiwa yeyote cha Kwanza humpiga sana kabla hata hawajaambiawa au kujua kama kweli amefanya hilo kosa au la. Huwa Watuhumiwa wanachukuliwa kwa nguvu na ma askari hao huku wakiwa wakipigwa makofi, mateke na kutupwa kwenye magari hayo na kupelekwa katika kituo cha polisi na wakati wako njiani bado polisi hao huendelea kuwapiga watuhumia hao sehemu mbalimbali bila kujali.
Sio kwamba ninayasema haya bila kuwa na ushahidi wowote , hili tukio limeshatokea kwa mtu wa karibu yangu.
Siku hiyo walikuja kumkamata kaka yangu,nyumbani kwetu akiwa chumbani kwake. Walimtoa kwa nguvu kutoka ndani wakiwa wamefunga mikono na miguu yake na bado wakiendelea kumpiga tu bila Sababu yoyote na bado walipomweka kwenye gari waliendelea kumpiga.
Hata hivi ninavyoyaandika haya maneno ninajawa na uwoga sana na kujiuliza hivi kwa kile kipigo ningempoteza kaka yangu ingekuwaje? Kiukweli watu wengi wamepoteza ndugu zao kwa huu ukatili wa mapolisi.
Unakuta mtuhumiwa amepelekwa polisi alafu baadae ndugu zake wanaambiwa kuwa mtuhumiwa amekufa akiwa kituo Cha polisi, wakiuliza Sababu wanaambiwa aliumwa au alijinyonga. Sasa utajiuliza mtu anajinyongaje akiwa kituo cha polisi.
Huwa mara nyingi Watuhumiwa hufa kwasababu ya maumivu waliyoyapata kutokana na vipigo wanavyopewa kuanzia wanavyokamatwa.
Sisi kama vijana tunawajibu wa kuliongelea na kulidhihirisha hili tatizo , ili watu waache kulichukulia kama Ni Jambo la kawaida. Serikali naiomba iingilie kati na iache kuyafukia fukia haya mambo, Jeshi la Polisi liache kuficha haya matendo na ichukue hatua ya kuwaelimisha polisi ili wafuate njia na utaratibu unaofaa wakati wa kumkamata mtuhumiwa na sio kufanya sifa eti kumpiga mtuhumiwa ili aweze kuonekana anafanya kazi.
Na Jambo kama hili linapotokea walidhihirishe kwenye vyombo vya habari ili watu wajue na wajifunze.
Tusisubiri mpaka Jambo la kusikitisha litokee mtandaoni ndio tujifunze, tuchukue hatua sasa.