Tabia ya kupenda kula matunda asubuhi

Tabia ya kupenda kula matunda asubuhi

encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
517
Reaction score
405
Habari zenu wanajamvi,

Ama baada ya salamu napenda niende moja kwa moja kwenye dhumuni la andiko hili.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 ninaishi Dar es Salaam.

Kuna jambo ambalo linanitatiza sana linalotokana na tabia yangu ya kupendelea zaidi kula matuda asubuhi kuliko chai, supu wala chakula kingine chochote. Ni mwaka wa 7 sasa sijui hata ladha ya chai ikoje kwani kila nikiamka asubuhi najikuta natamani kula matunda kama ndizi mbivu, machungwa, mananasi, matikiti n. K

Tabia hii ya kutokupenda kunywa chai nilianza tangu nikiwa mdogo kwani ilikuwa ikiachwa pesa ya matumizi nyumbani basi kwenye kipengele cha chai nilikuwa naiomba pesa ya vitafunwa naenda kununua matunda au vitafunwa vingine ambavyo nilikuwa nikipendelea kuvila bila ya chai.

Naomba ushauri wenu (ikiwezekana wa kitabibu) juu ya madhara au faida inayoweza kujengwa kutokana na tabia yangu hii.

NAWASILISHA
 
Ni addiction tu...Na case yako kwa afya ni nzuri si mbaya ukiendelea.

Mimi nilikuwa nadisi chai nikaanza kupenda maji.Nikawa addicted sasa.Kila nikiamka asubuhi ni maji.Nikajitahidi kuvumilia hamu yangu ya maji asubuhi,nikashinda kwa kiasi chake.So nikawa napiga breakfast kabla ya kunywa maji ila nikimaliza maji ni lazima nipige.Na ndo ipo hivyo hadi leo.

Chai ya rangi sipendi.
 
Mtu usipo tumia kitu cha moto asubuhi kwa muda mrefu haiwezi kuleta shida badaye?
Kipasha tumbo asubuhi kuna faida zake uamkapo asubuhi na si lazima iwe chai inaeza kuwa ata maji ya vuguvugu kidogo unaliweka sawa kwa glass moja ya maji ya vuguvugu then unaendelea na ratiba zako.
 
Ni addiction tu...Na case yako kwa afya ni nzuri si mbaya ukiendelea.
Mimi nilikuwa nadisi chai nikaanza kupenda maji.Nikawa addicted sasa.Kila nikiamka asubuhi ni maji.Nikajitahidi kuvumilia hamu yangu ya maji asubuhi,nikashinda kwa kiasi chake.So nikawa napiga breakfast kabla ya kunywa maji ila nikimaliza maji ni lazima nipige.Na ndo ipo hivyo hadi leo.
Chai ya rangi sipendi.
Daah.. upo kama mimi yaani chakula chochote hata kama nakipenda vipi ukinilazimisha kula na chai nakula kidogo kama mtoto
 
Ni vizuri,ingawa asubuhi mara nyingi tunashauriwa kuweka menyu yenye akili kidogo ili uweze kuhimili mikiki ya kutafuta mkate wa kila siku,ila kama unakula hayo matunda na hayakupi shida yoyote endelea tu na utaratibu wako...
 
Hii risk ya utumbo kujikunja inakuwaje maana kuna mtu alinitishia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom