Kama hupendi unene na uzito usiofaa pata haya maarifa ufanikiwe ndani ya mwezi mmoja

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,424
11,096
Habari wadau,

Naomba ushiriki katika ujenzi wa afya, Dunia hii malaika ni watu na si vinginevyo, kila mmoja wetu kaumbwa kama malaika wa pekee, niwape hili moja la kupunguza mwili na Uzito na kuondokana na tabia ya kula kula kila wakati.

Anza zoezi la kutumia kahawa iliosagwa vizuri ya dukani au ya kutengenezwa vizuri, weka ratiba kila asubuhi kabla ya mlo wowote. Kijiko Cha chai kimoja na maji yako ya moto hutajuta. Ondoa kitambi kwa afya na Punguza Uzito.

Ukitumia hii weka ratiba ya kula saa 7 mchana au saa10 Kwa sababu hutahisi njaa.

Tafadhari: kama una pressure usitumie fuata ushauri wa daktari.

Awamu ijayo ntawaletea njia ya juice na aina ya mchanganyiko wa matunda.

Unaefanya mazoezi endelea na ongeza na matumizi ya Kahawa.

Pambana usilete lawama mara oooh nafsi inataka mwili unakataa, msisahau kula protein, zinc na vitamin kwa wingi.

Mnaotumia Asali na Maziwa Mgando au Maziwa Mtindi msiache. Ali kasusu, pweza tumieni.

K-Vant , Konyagi, smart etc kunywa kiasi Kwa afya yako.

Nawasilisha Afya ni msingi na ndio Utajiri Linda afya ufaidi Dunia.

Wadiz na Malaika wake.

Am out comrades.
 
Acha hizo! Kitambi noma lakini kinaleta heshima fulani. Ukiongea na mtu kwa kujiamini, na huku unakishikashika kitambi, mara utasikia unayeongea naye anataka kukukopa!

Akuu! Mie naendelea nacho!
 
Ambao hatutumii kahawa tutumie nin tupungue mim sijui raha zimenizidia nanenepa tu 😂😂
Ntakuja na next phase ya mixer ya matunda usage juice itakusaidia tu usihofu
 
Back
Top Bottom