Nawezaje kuacha tabia sugu niliyoanza ya kupenda kula kula

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
unaweza kuona ni rahisi kuacha kwasababu wewe hauna hili tatizo lakini kwa mtu ambae ni mraibu huu ni mtihani mzito, ni sawa na kumwambia mtu aache uraibu wa simu, aache ulevi wa pombe, aache sigara, aache kamali, n.k.. sio rahisi kihivyo, Nimekuja kwa unyenyekevu humu ndani muwezi kunipa ushauri na mbinu zinazoweza kunisaidia kuacha hiuu uraibu maana kiukweli unanigharimu.

Zamani nilikuwa mara mbili ama mara tatu asubuhi kunywa chai, chakula cha mchana na cha usiku

Lakini kwa sasa ni lazima nile mara tatu na kuna ratiba za ziada,,,

ASUBUHI

Asubuhi saa moja nakunywa chai na maandazi au chapati

mida ya saa nne asubuhi lazima nakunywa tena chai ya pili na chapati moja.

MCHANA

Chakula cha mchana saa saba nakula ugali au wali,,,, pembeni parachichi na maziwa ya mgando

mida ya saa tisa hivi nanunua karanga za 200 na chungwa la 200

Jioni mida ya saa 11 nagonga chips nyama na pepsi

USIKU

mida ya saa moja hivi wakati narudi kwangu huwa naunua crips ya ndizi au mwindi wa kuchoma

chakula rasmi cha usiku mida ya saa tatu nakula ugali au wali,,,, pembeni maziwa ya kuchemsha huwa nalipa bili kwa jirani mwenye ngombe,

WEEKEND

ratiba ya msosi mkuu wa mchana pilau nyama ama biriani ....

ratiba ya msosi mkuu wa usiku mbuzi wa kuchoma ama kuku wa kuchoma

MAJI.

Kila siku lazima ninywe maji lita na nusu

kiukweli ni kama utumbo wangu umetanuka unahitaji supply zaidi.

Ni vipi nawezaje kuacha huu uraibu
 
View attachment 2356837

Zamani nilikuwa mara mbili ama mara tatu asubuhi kunywa chai, chakula cha mchana na cha usiku

Lakini kwa sasa ni lazima nile mara tatu na kuna ratiba za ziada,,,

mida ya saa nne asbuhi lazima ninywe chai ya pili pamoja na vitafunwa

Jioni nagonga chips, mshkaki na pepsi, ikifika usiku nashindilia dinner kama kawaida

hizi karanga za mtaani, mahindi ya kuchoma na machungwa nanunua sana....

kiukweli ni kama utumbo wangu umetanuka unahitaji supply zaidi.

Ni vipi nawezaje kuacha huu uraibu
Kula tu mkuu hamna namna. Fidia maana ukianza kuumwa kisukari, pressure, obesity watakukataza kabisa kula hivyo vitu. Kwa hiyo wewe kwa sasa shindilia tu hamna namna

Ila kumbuka wanasema...." kama hauwezi kupanga jinsi ya kula ukiwa mzima, Utapangiwa jinsi ya kula ukiugua."
 
Nimeomba ushauri wa jinsi ya kuacha, hivyo vingine navijua
 
Mimi sijutii kupenda kula huwa nikipata hela napenda kula misosi mizuri na naona ni bora kuliko hela kuliwa kwenye betting.
 
Mimi sijutii kupenda kula huwa nikipata hela napenda kula misosi mizuri na naona ni bora kuliko hela kuliwa kwenye betting.
Kula ni raha aisee,,,hapa nimetoka kupiga kyepe na nyama choma sina stress

tatizo linaanza ukifanya kula kuwe too much.
 
Back
Top Bottom