Mwanangu nakuita hivo kwa umri wako wa 27
Wengi wamekujibu hapa wengi ni kejeli na masihara hakuna aliyezama kitaalamu ila wako wamegusia kidogo nimewapa likes zao.
Unachofanya uko 100% na ndio maana wazungu breakfast yao asubuhi hukosi matunda.
Matunda hasa ya rangi rangi yana kemikali yenye anti-oxidant hii antioxidant ni kemikali inayozuiya cell za mwili hasa ngozi zisisinyae.Tuchukulie mfano msumari mpya ili upate kutu unahitaji vitu viwili maji na hewa ya oxygen.
Kwa maana hiyo ukiunyima oxygen haupati kutu asilani.
Kwa cell za binadamu za ngozi nazo matunda yanazuiya oxidation isifanyike haraka kwenye ngozi kwa vyovyote ngozi inakuwa nyororo baby face japo umri mkubwa.
By the way kwa tabia yako hii toka utotoni lazima utakuwa una ngozi nyororo kuna mtu amekutania hapa ngozi yako ikoje ukamuambia iko kama ina mafuta ukweli ni kwamba haijakakamaa.
Chunguza wakazi wengi wa Muheza,Wasambaa na Tanga kwa ujumla wana baby face sababu kule kunakubali matunda misimu yote.
Matunda yote yana antioxidant ila ya rangi rangi ni zaidi maana yana flavonoids mfano wa matunda hayo ni zabibu na BlackBerry,zambarau na mengineyo.Nakuwekea picha.
Ila kushtua utumbo kama hupendi chai kama niichukiavyo kunywa kitu chochote cha moto mfano maziwa au hata maji baada ya kula matunda yako.
View attachment 1461945View attachment 1461946