Tabia ya kupenda kula matunda asubuhi

Tabia ya kupenda kula matunda asubuhi

Wewe ni msabato?

Nimekutana nao kadhaa hawanywi chai!
Habari zenu wanajamvi,

Ama baada ya salamu napenda niende moja kwa moja kwenye dhumuni la andiko hili.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 ninaishi Dar es Salaam.

Kuna jambo ambalo linanitatiza sana linalotokana na tabia yangu ya kupendelea zaidi kula matuda asubuhi kuliko chai, supu wala chakula kingine chochote. Ni mwaka wa 7 sasa sijui hata ladha ya chai ikoje kwani kila nikiamka asubuhi najikuta natamani kula matunda kama ndizi mbivu, machungwa, mananasi, matikiti n. K

Tabia hii ya kutokupenda kunywa chai nilianza tangu nikiwa mdogo kwani ilikuwa ikiachwa pesa ya matumizi nyumbani basi kwenye kipengele cha chai nilikuwa naiomba pesa ya vitafunwa naenda kununua matunda au vitafunwa vingine ambavyo nilikuwa nikipendelea kuvila bila ya chai.

Naomba ushauri wenu (ikiwezekana wa kitabibu) juu ya madhara au faida inayoweza kujengwa kutokana na tabia yangu hii.

NAWASILISHA
 
Hongera! Utumiaji wa matunda ni bora na muhimu, natumai utakuwa mwenye ngozi angavu, kinga imara na lishe.

Pia ni vizuri endapo utatumia chai/kufungua kinywa chenye uvuguvugu/joto kuwezesha kulichangamsha tumbo na misuli iliyopoa. Pia tafiti inaonesha utumiaji wa vitu vyenye joto unaondosha hali ya kuzeeka haraka.
 
Kitu cha moto si chochote tu hata kama sio chai?
 
Habari zenu wanajamvi,

Ama baada ya salamu napenda niende moja kwa moja kwenye dhumuni la andiko hili.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 ninaishi Dar es Salaam.

Kuna jambo ambalo linanitatiza sana linalotokana na tabia yangu ya kupendelea zaidi kula matuda asubuhi kuliko chai, supu wala chakula kingine chochote. Ni mwaka wa 7 sasa sijui hata ladha ya chai ikoje kwani kila nikiamka asubuhi najikuta natamani kula matunda kama ndizi mbivu, machungwa, mananasi, matikiti n. K

Tabia hii ya kutokupenda kunywa chai nilianza tangu nikiwa mdogo kwani ilikuwa ikiachwa pesa ya matumizi nyumbani basi kwenye kipengele cha chai nilikuwa naiomba pesa ya vitafunwa naenda kununua matunda au vitafunwa vingine ambavyo nilikuwa nikipendelea kuvila bila ya chai.

Naomba ushauri wenu (ikiwezekana wa kitabibu) juu ya madhara au faida inayoweza kujengwa kutokana na tabia yangu hii.

NAWASILISHA
Unafanya jambo zuri sana kiafya. Tulipaswa kufanya hivyo wote kwa afya zetu. Ukila matunda asubuhi wakati tumbo ni tupu unapata manufaa zaidi kiafya kama vile kuondoa sumu mwilini na kusafisha utumbo.

Tena kula matunda peke yake asubuhi Husaidia kupunguza unene.
 
Je kama sio mnene si ndio nazidi kukonda?
 
Unahisi utofauti wowote katika mwili wako?
Mfano:-
Nguvu za Kiume
Ufanyaji kazi
Choo
Minyoo
Kulegea mwili
Kama upo Ok, basi endelea ila warm foods husaidia pia kwa mwili wako kuufanya utoe jasho na kurekebisha jotoridi la mwili
 
Habari zenu wanajamvi,

Ama baada ya salamu napenda niende moja kwa moja kwenye dhumuni la andiko hili.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 ninaishi Dar es Salaam.

Kuna jambo ambalo linanitatiza sana linalotokana na tabia yangu ya kupendelea zaidi kula matuda asubuhi kuliko chai, supu wala chakula kingine chochote. Ni mwaka wa 7 sasa sijui hata ladha ya chai ikoje kwani kila nikiamka asubuhi najikuta natamani kula matunda kama ndizi mbivu, machungwa, mananasi, matikiti n. K

Tabia hii ya kutokupenda kunywa chai nilianza tangu nikiwa mdogo kwani ilikuwa ikiachwa pesa ya matumizi nyumbani basi kwenye kipengele cha chai nilikuwa naiomba pesa ya vitafunwa naenda kununua matunda au vitafunwa vingine ambavyo nilikuwa nikipendelea kuvila bila ya chai.

Naomba ushauri wenu (ikiwezekana wa kitabibu) juu ya madhara au faida inayoweza kujengwa kutokana na tabia yangu hii.

NAWASILISHA
Mwanangu nakuita hivo kwa umri wako wa 27
Wengi wamekujibu hapa wengi ni kejeli na masihara hakuna aliyezama kitaalamu ila wako wamegusia kidogo nimewapa likes zao.
Unachofanya uko 100% na ndio maana wazungu breakfast yao asubuhi hukosi matunda.
Matunda hasa ya rangi rangi yana kemikali yenye anti-oxidant hii antioxidant ni kemikali inayozuiya cell za mwili hasa ngozi zisisinyae.Tuchukulie mfano msumari mpya ili upate kutu unahitaji vitu viwili maji na hewa ya oxygen.
Kwa maana hiyo ukiunyima oxygen haupati kutu asilani.
Kwa cell za binadamu za ngozi nazo matunda yanazuiya oxidation isifanyike haraka kwenye ngozi kwa vyovyote ngozi inakuwa nyororo baby face japo umri mkubwa.
By the way kwa tabia yako hii toka utotoni lazima utakuwa una ngozi nyororo kuna mtu amekutania hapa ngozi yako ikoje ukamuambia iko kama ina mafuta ukweli ni kwamba haijakakamaa.
Chunguza wakazi wengi wa Muheza,Wasambaa na Tanga kwa ujumla wana baby face sababu kule kunakubali matunda misimu yote.
Matunda yote yana antioxidant ila ya rangi rangi ni zaidi maana yana flavonoids mfano wa matunda hayo ni zabibu na BlackBerry,zambarau na mengineyo.Nakuwekea picha.
Ila kushtua utumbo kama hupendi chai kama niichukiavyo kunywa kitu chochote cha moto mfano maziwa au hata maji baada ya kula matunda yako.
20200528_235306.jpg
20200528_235203.jpg
 
Unahisi utofauti wowote katika mwili wako?
Mfano:-
Nguvu za Kiume
Ufanyaji kazi
Choo
Minyoo
Kulegea mwili
Kama upo Ok, basi endelea ila warm foods husaidia pia kwa mwili wako kuufanya utoe jasho na kurekebisha jotoridi la mwili
Hivyo vyote vipo sawa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom