Tabia hii inatugharimu mamilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabia hii inatugharimu mamilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WomanOfSubstance, Oct 15, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Muda ni mali..ukipita umepita huwezi ku rewind!
  Inakuwaje watu wanashindwa kuzingatia rasilimali hii muhimu inayoitwa MUDA? Utamwalika mtu nyumbani kwako aje kwa chakula cha mchana au usiku.Unampa na muda kuwa chakula kitakuwa saa saba mchana au saa moja usiku.Unashangaa... mhusika anakuja masaa matatu baadae! Haoni anakushindisha njaa?
  Unamwalika mtu kuhudhuria mkutano saa 3 asubuhi... anafika baada ya saa 4..ina maana hajui kuwa kila agenda ina muda?
  yako mengi sana...na ukiyafikiria sana unaweza kuona mateso na hasara ambayo inatokana na kupoteza hii rasilimali.....
  hebu endelezeni huu mjadala..maana natoka kidogo nitarudi kuendelea
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wabongo hawajui kuwa mshahara wa mtu ni masaa aliyofanya kazi. Ulaya unalipwa kwa man hour. Bongo kwa kwa siku na hata uispoenda unalipwa tu. Watajuaje heshima ya hii rasilimali MUDA??????????
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nchi zilizoendelea ukijifanya hujali muda basi utajikuta unapitwa na kila kitu kuanzia appointment ya daktari, kusukwa nywele, kusafisha meno yang'ae,......
  utaachwa na train, tram, bus, ndege.... na hivi vikishakuacha automatically utachelewa kila kitu kingine hadi kazini.... ukichelewa kazini ujue muda wako nao utakuwa pungufu na ujira wako utakuwa pungufu hivyohivyo kwa vile unalipwa kwa kazi ulizofanya kwa masaa kadhaa!
  TZ unakuta eti mtu hajafika kwenye miadi..unampigia simu " uko wapi"..anakujibu "niko njiani kuna foleni"...kumbe ndio kwanza anaamka hajaoga wala kupiga mswaki!
   
 4. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  "Huyu jamaa anayeitwa muda sio rafiki wa mwanadamu,atakukosesha mavumba kama hauko on time"-Fid Q!!Mimi inaniuma sana kukuta vijana wamekaa maskani discussing maisha ya wengine na issue zisizowezekana,sisemi kwamba sipendi kukaa maskani,lakini baada ya mihangaiko na maskani pawe kama darasa yani tuwe tunaongelea mada zinazojenga sio kubomoa!!
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,045
  Likes Received: 24,043
  Trophy Points: 280
  VC
  Kipindi pekee ambacho watu wanajali muda ni kwenye appointment za kungonoka. Ningekushauri ungeliweka hili kwenye thread yako uone ambavyo watu wangeichangia. Kwenye vi date hakuna kupoteza muda, ndo ujue Yesu kashalipa nauli ya kurudi duniani.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Interesting!
  Hii dimension sikuwa nimeifikiria kabisa. Hebu tuwasikie...
  Fidel upo?
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Gademu Chris.... Yaani hii ni kweli aisee in most cases!!! Hasa kabla ya kumega, na utakuta mtu anawahi hata masaa... Hahahaaaaaa

  Hii naipa platinum ya wiki mazee
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  KUMBE INAWEZEKANA KUWAHI EH?
  Kwanini hawachelewi kwenye hili?
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ahh wapi,
  Mie nilishachelewa mara kadhaa. Kila mtu ananifahamu kwa hilo. Ila muda wote hujitahidi kumjulisha mwenyeji wangu kuwa NAJA na ntachelewa......
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kuna Audio kwenye YOUTUBE, Sean Paul alichelewa kwenye kipindi cha Radio kama dakika 45. Walipomuuliza kulikoni akawajibu "This is Jamaican Time...."

  Sasa tuje kwa hawa Rastaman, hawafahamu kutunza kabisa muda. Kiboko ni Wacongo. Kuna Mkongo mmoja ukikubaliana naye leo, anaweza kuja baada ya siku tatu...... Na akifika kitu cha kwanza anacheka. Hafahamu kabisa kuchukia. Huyu jamaa nasikia alionekana mitaa ya London na gitaa lake maana ni Mlevi si kawaida. (Mtanzania, umeshamuona huko kijana JINO?).
  Kuna mwaka nilipata habari jamaa walitoa hela nyingi tu kukodisha jukwa na jukwa likajengwa eneo zuri tu. Walikuwa wafanye mashindano ya Queen of Dancehall". Kila kitu kilikuwepo na hadi Wasichana na familia zao wamekuja kuwashangilia ila kasoro Waendeshaji pambano. Ilikuwa waanze saa 5 asubuhi na wamalize saa 9 mchana. Huwezi amini jamaa wamekuja saa tisa kasoro mchana. Wenye eneo wakawaambia inabidi muanze kuliondoa jukwaa lenu na si kuanza mashindano. Ukaanza ubishi hadi ikafika saa tisa mchana...... muda umekwisha. Jamaa wakati wanaangalia huku na kule, wakaona unapita msafara wa watu wamebeba mabango "Legalise Marijuana....." Jamaa wakaacha jukwaa na kwenda kuungana na hayo maandamano. Wala hawakujali kuwa mashindano hayakufanyika......

  Yep, kuna wengine si tu kuwa wanapoteza mamilioni, cha ajabu ni kuwa hata HAWAJALI........

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=8HcXcYlF3_0&feature=related[/ame]
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Waafrica/Watanzania sijui kwanini hatujaelewa umuhimu wa muda.Cha ajabu kwetu kunapambazuka mapema kuliko sehemu nyingi yet tuko nyuma kila kitu!
  Kitu kingine, utasikia majamaa yakisema bila aibu " leo saa haziendi kabisa, napoteza muda tu maana siku ndefu sana" Hapo ujue hana kitu cha kufanya..ameshinda maskani/kijiwe akipiga soga na kuhesabu magari na kutizama nani kapita.Hawahawa utasikia wakilala " maisha magumu, sina kitu! Lol!
   
Loading...