Tabasamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabasamu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 5, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,475
  Likes Received: 5,715
  Trophy Points: 280
  [h=3]Tabasamu[/h]

  [​IMG] Tabasamu ni njia rahisi isiyo na gharama ya kubadilisha mwonekano wako.
  Tabasamu ni kitu gani?
  Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka.
  Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.

  Kila unapotabasamu kwa mtu yeyote ni ishara ya upendo, ni zawadi kwa yule mtu ni kitu kizuri.
  Tabasamu ni kusema karibu, tabasamu ni uwezo ambao unaweza kuifanya siku ya giza kuwa siku ya nuru, huweza kufanya pasipo na upendo kuwa na upendo.
  Inagharimu misuli 17 tu kutabasamu na inakugharimu misuli 43 kuwa na ndita kwa nini ujizeeshe mapema?
  Amani huanza kwa tabasamu!

  Huwezi kuvaa ukapendeza bila kuvaa tabasamu, huwezi kuwa mrembo bila kuvaa tabasamu huwezi kuitwa beautiful one kama hujavaa tabasamu huwezi kuitwa handsome kama hujavaa tabasamu period!
  Tafiti zinaonesha mtu anayetabasamu huwezi kuongeza miaka mingi katika maisha yake.
  Hata hivyo watoto hujifunza kutabasamu kutoka kwa wazazi wao.

  Umemaliza kusoma hapa, sasa zamu yako kutabasamu then kicheko
   
Loading...