Sijui nimewaambukiza wangapi ila wengi ni waume za watu

mkunga wa jadi

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2025
Posts
208
Reaction score
457
Mimi ni mwanafunzi wa chuo, binti mwenye sura ya kawaida lakini anayejua kuitumia. Natabasamu na kuongea kwa upole, lakini ndani yangu nimebeba maumivu makali sana. Na leo, nimeamua kusema ukweli wangu, kwa sababu nimechoka kubeba mzigo huu peke yangu.

Nilipoingia darasa la sita, familia iliniamini sana, nilikuwa nakaa kwa dada yangu mkubwa, alinihudumia kama mama. Shemeji yangu,mume wa dada yangu alikuwa kama baba kwangu. Lakini usiku mmoja uliharibu kila kitu,alinibaka, nilijichukia sana.

Dada yangu hakutaka kusikia haya mambo,alisema namkosea heshima mume wake. Nilikua nalia kila usiku. Hakuna aliyeniona,hakuna aliyeniuliza "uko sawa?"

Miaka ikaenda niliendelea kusoma, lakini nikawa siyo yule yule tena. Nilianza kuwa na hasira na wanaume,nikawa siamini mtu yeyote. Nilijifundisha kuficha chuki yangu ndani ya tabasamu na nikaanza mpango wangu wa kulipa kisasi. Bila kujua, nilikuwa nimeambukizwa virusi vya UKIMWI na shemeji yangu.

Nilipofika chuoni, nikageuka kuwa mtu mwingine nikawa natafuta wanaume hasa waliooa nilikuwa nawafanya wanione kama mwanamke wa ndoto zao nikawaambia maneno wanayotaka kusikia, nikawapa mapenzi ya kuwakoleza,na baada ya hapo, nilihakikisha wanakuwa sehemu ya kisasi changu.

Sijui ni wangapi nimewaambukiza mpaka sasa wengi wao ni waume za watu, viongozi wa makanisa, walimu, wafanyabiashara na sijawahi kuwaambia ukweli. Niliamini kama mimi niliumizwa bila huruma, basi nitafanya dunia yote ilie pamoja nami.

Lakini leo… leo nimechoka kuvaa tabasamu la kishetani huku nikiungua kwa ndani.Najua ninachokifanya si sahihi,lakini je, ni nani aliyenisaidia kipindi nilipokuwa nalia na unyanyasaji niliofanyiwa?

Siombi huruma yenu maana ni mfu mtarajiwa,naomba ushauri tu. Je, naweza kubadilika? nawezaje kuiponya nafsi yangu yenye uchungu? Nawezaje kurudisha utu wangu uliopotelea kwenye visasi?
 
doh........wazee wa nusu mlingoti(CHAPUTA) Tunakoswa na mengi
btw pole sana new member
sheria ni moja duniani kote(no one is interested in ur feelings)
unachoona sawa endelea kufanya tu
kama unaamini mungu, OMBA MWISHO UWE MWEMA.
 
Mimi ni mwanafunzi wa chuo, binti mwenye sura ya kawaida lakini anayejua kuitumia. Natabasamu na kuongea kwa upole, lakini ndani yangu nimebeba maumivu makali sana. Na leo, nimeamua kusema ukweli wangu, kwa sababu nimechoka kubeba mzigo huu peke yangu.

Nilipoingia darasa la sita, familia iliniamini sana, nilikuwa nakaa kwa dada yangu mkubwa, alinihudumia kama mama. Shemeji yangu,mume wa dada yangu alikuwa kama baba kwangu. Lakini usiku mmoja uliharibu kila kitu,alinibaka, nilijichukia sana.

Dada yangu hakutaka kusikia haya mambo,alisema namkosea heshima mume wake. Nilikua nalia kila usiku. Hakuna aliyeniona,hakuna aliyeniuliza "uko sawa?"

Miaka ikaenda niliendelea kusoma, lakini nikawa siyo yule yule tena. Nilianza kuwa na hasira na wanaume,nikawa siamini mtu yeyote. Nilijifundisha kuficha chuki yangu ndani ya tabasamu na nikaanza mpango wangu wa kulipa kisasi. Bila kujua, nilikuwa nimeambukizwa virusi vya UKIMWI na shemeji yangu.

Nilipofika chuoni, nikageuka kuwa mtu mwingine nikawa natafuta wanaume hasa waliooa nilikuwa nawafanya wanione kama mwanamke wa ndoto zao nikawaambia maneno wanayotaka kusikia, nikawapa mapenzi ya kuwakoleza,na baada ya hapo, nilihakikisha wanakuwa sehemu ya kisasi changu.

Sijui ni wangapi nimewaambukiza mpaka sasa wengi wao ni waume za watu, viongozi wa makanisa, walimu, wafanyabiashara na sijawahi kuwaambia ukweli. Niliamini kama mimi niliumizwa bila huruma, basi nitafanya dunia yote ilie pamoja nami.

Lakini leo… leo nimechoka kuvaa tabasamu la kishetani huku nikiungua kwa ndani.Najua ninachokifanya si sahihi,lakini je, ni nani aliyenisaidia kipindi nilipokuwa nalia na unyanyasaji niliofanyiwa?

Siombi huruma yenu maana ni mfu mtarajiwa,naomba ushauri tu. Je, naweza kubadilika? nawezaje kuiponya nafsi yangu yenye uchungu? Nawezaje kurudisha utu wangu uliopotelea kwenye visasi?
Mi naona ni sawa tu hayo yote ulofanya.
When it comes to love, everything is fair
 
IMG-20230419-WA0023.jpg
 
Pole...... Achavisasi jifunze kuishi kwa matumaini, ila kumbuka hakuna atakaye ishi milele hapa Duniani
 
Ukimwi hauambukizi kirahisi hivyo especially kwa mwanaume aliyetahiriwa. Unajipa stress buree na kujiongezea maambukizi tu. Nishakula jimama lenye ngoma miezi 6 bila kujua,nilipojua nilipanick hatari. Kwenda kupima majibu yakatoka negative. Relax tu.
 
Offside
0909973F-4E6E-49E9-B6E9-BCF4CA46AC44.jpeg

Back
Top Bottom