Tabasamu lako ni ishara ya nini?☺️☺️

Tabasamu lako ni ishara ya nini?☺️☺️

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
4,927
Reaction score
11,633
Tabasamu ni nini? 😊
Tabasamu mara nyingi huonekana kama ishara ya furaha
Kuna wakati mtu hutabasamu kutokana na jambo zuri alilofanyiwa labda mguso wenye upendo, busu tamu la hisia kuona mazingira mazuri au kitu kinachovutia na kuleta amani moyoni

Lakini si kila tabasamu lina maana ya furaha😊
Wakati mwingine watu hutabasamu huku ndani wakiwa na maumivu makubwa Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa fake smile tabasamu la kujifanya kila kitu kiko sawa ilhali sivyo😢

Baadhi ya watu hutabasamu ili kuficha huzuni zao
Pengine wanaogopa wakionyesha majonzi wataonekana dhaifu, watasimangwa, au watu watatumia matatizo yao kama fursa ya kuwanyonya

Mf: kuna wanawake wakionyesha udhaifu mbele ya mwanaume mwenye nia mbaya, anaweza kutumia maumivu yao kama advantage kwa maslahi yake binafsi

Kwa upande wa wanaume ndiyo zaidi
Wengi wamelelewa kuamini kuwa mwanaume hapaswi kulia wala kuonyesha maumivu

MF; Kuna member mmoja niliona akisema et amechoshwa na nyuzi za wanaume kulalamika
Nilishangaa kwamba wanaume wao hawana hisia🤔
Wao hawapaswi kusema au kuomba ushauri au kueleza namna wanavyojisia?
Utasikia👇
Wewe ni mwanaume, jikaze
Ndiyo maana wengine wanabaki na tabasamu la uongo huku ndani wakiteketea kimya kimya

Hapo tunaona wazi kuwa si kila tabasamu hutafsiri furaha
Kuna tabasamu ni la kupretend, lakini ndani limebeba huzuni, stress, upweke na majeraha ya moyo

Cha kushangaza, baadhi ya wanasayansi na wataalamu wa psychology wanasema hata fake smile inaweza kumsaidia mtu kwa muda, kwa sababu ubongo huweza kudanganyika na kuhisi hali ni nzuri kuliko ilivyo

Sasa swali linabaki
Je, kuna ulazima wa kutabasamu hata wakati moyo umechoka?
Au mtu akae tu na sura yake ya (mbuzi sura ya ngwasuma)bila kujilazimisha kucheka ili kufurahisha dunia? 😎

ShesRise_1 👋 MR Blue TABASAMU NIPATE FURAHA😊😊
 
Wengine hapa, tabasamu mdomoni, maumivu moyoni.

Cha msingi hakuna haja ya kuonyesha maumivu kwa mtu ambaye unaona hawezi kukusaidia.

Una njaa, badala mtu akupe chakula anaanza kukupa mahubiri 🗑️
 
Kilichokufanya utabasamu asubuhi ya leo kishikilie kwa wivu mkubwa ili upate uhakika wa tabasamu lako😊
Boss mkubwa kakosea namba kanipigia mimi alafu anasema shikamoo baba nikaitikia ndiyo akagundua ni mimi akakata simu
Nikajikuta nacheka na kutabasamu na siku yangu iko vizuri mno lile lijamaa kunipa mimi shikamoo najiona mwamba sana aisee
 
Back
Top Bottom