Taasisi za Marekani, zamtambua Muhongo

Aende akalime huko. Sie tutanunua matrekta toka India

Sina shaka nawe ndugu yangu, maana umejipambanua kwa ID yako kuwa u MPITA NJIA. Hata huko ulikotekwa kiakili na mafisadi unapita tu. Si muda mrefu utarejea kwenye njia sahihi na utampa kura ya NDIYO Prof. Muhongo.
 
Nakubaliana new K-Boko. Nafasi ya uwaziri kwa jembe kama Muhongo haifai. UKUU WA NCHI ndo unamfaa huyu jamaa ili awanyooshe mafisadi walioshindikana, wanaokwiba mali za wananchi kasha kujifanya wanatoa vijimisaada ili kuwapumbaza.

Kama SETH vile anavyotoa vijimisaada policcm.
 
Kilichomponza ni lugha chafu na kudharau waafrika wenzake kumbe kwa vile anajiona ni sehemu ya wazungu, basi apake krimu awe mzungu kabisa

Lugha chafu ulimlisha? Tutaanza kukupaka wewe hiyo cream. Baadae pitia kopo la Carolite dukani kwa Mangi nakuja kulipa!
 
Sina shaka nawe ndugu yangu, maana umejipambanua kwa ID yako kuwa u MPITA NJIA. Hata huko ulikotekwa kiakili na mafisadi unapita tu. Si muda mrefu utarejea kwenye njia sahihi na utampa kura ya NDIYO Prof. Muhongo.
Endeleeni kuota mchana. Hivi kwa nini hamuamini kuwa Kikwete ameshateua waziri wa Nishati mwingine?
 
Tafakari kauli hii ya basha lako kwa umakini... " Watanzania wanamitaji ya kukamua juicy tu" ..."Hawana Uwezo wa kumiliki utajiri wa Gas"... Then Uliza OPHIR GAS walitengeneza kiasi gani na Waliwekeza kiasi GANI? ... Kwanini Maliasili zetu hazitumiwi kama Collateral? ... Najua kuwa wewe ni akili ndogo kama huyo jamaa yako alierudia darasa la saba mara 7 ... Tambua kuwa Intelligensia ya mtu hujengwa na kuonekana Udogoni...
hehehehehehhehe kweli nyani haoni kundule! mbona nyie safari za ujerumani kila siku, mwatafuta nini kule, au nanyi mwatumiwa!''' yeye anatambuliwa kwa akili zake matata sio nyie mnaojipendekeza
 
Wakati dunia na mataifa ya Magharibi ya Ulaya na Marekani, yakifanya jitihada kubwa kukusanya wasomi wenye vipaji toka sehemu mbalimbali duniani, kwa ajili ya tafiti na vumbuzi ili kijipeleka mbele zaidi kisayansi na kiteknolojia;

na wakati wasomi wanaosaka maslahi zaidi kimaisha wakiendelea kukimbilia Ulaya na Marekani (Brain drain), Wabunge masilahi Tanzania wanafanya jitihada za kubwa kufukuza na kuwakatisha tamaa wachache wenye nyoyo za Uzalendo.

Profesa Muhongo, ni mmoja wa wanasayansi mahiri katika sayansi ya madini (Geologist), anayetambuliwa na kuheshimika na mashirika mbalimbali ya kisayansi na tafiti ulimwenguni.

Miongoni mwa taasisi zinazoaminika kimataifa zinazomtambua na kumtumia Profesa Muhongo katika uwezo wake wa utendaji wa Kazi ni pamoja na FGSA la Marekani, FGS la London, Uingereza: Hon FCAGS la London, Uingereza; Hon FCGS la China, na Chuo cha kuendelea Sayansi ya dunia (FTWAS).

(Source AL-HUDA)

Wanamtambua kwa kuwa ana maslahi kwao na sisi hatumtambui kwa kuwa hana maslahi kwetu full stop.
 
​kwanini wasimtambua kwa kugawa vitalu vya gas kwa wageni

Fisadi Mengi pia anamtambua, kamwulize. Alidhani atajichotea tu vitalu vya gesi kama alivyofanya kwenye madini kwa kumiliki 'Dar es Salaam tatu' bila kuziendeleza wala kulinufaisha Taifa kwa kisingizio cha UZAWA!! Kwa Prof. Muhongo alikwama na hatokaa apate, maana naamini hata uongozi mpya wa wizara ya nishati na madini hautampa fursa hiyo. Mfikishie salamu.
 
Msitupotezee muda, wapo wengi kama yeye ndani na nje ya nchi, hawatumii muda wao kupata watu kama wewe kupewa maelekezo yakutuletea humu. wacha watu wamuelewe prof Muhongo wanavyo mfahamu.

Sasa ni kama prof Muhongo anajidhalilisha au ana dhalilishwa na hao wanao fikiri wanamjenga. aendelee kutambuliwa duniani kwa utaalam wake, atabaki kutambuliwa ni Mtanzania tu, lakini kwa hapa nyumbani ameambiwa na prof mwenzake atupishe hatoshi.

Mtabwabwaja sana mwaka huu. Mwanasayansi ndio kaisha tambulika hivyo. Kama vipi panda kazifute hizo Awards alizopewa kama wewe Kipanga zaidi yake!
 
Fisadi Mengi pia anamtambua, kamwulize. Alidhani atajichotea tu vitalu vya gesi kama alivyofanya kwenye madini kwa kumiliki 'Dar es Salaam tatu' bila kuziendeleza wala kulinufaisha Taifa kwa kisingizio cha UZAWA!! Kwa Prof. Muhongo alikwama na hatokaa apate, maana naamini hata uongozi mpya wa wizara ya nishati na madini hautampa fursa hiyo. Mfikishie salamu.

Bhupe nakuunga mkono kwa ka Bwana mdogo Simbachawene ndio hatapata kitu kabisaaa. Dogo kakomaa kama Muhongo!
 
Endeleeni kuota mchana. Hivi kwa nini hamuamini kuwa Kikwete ameshateua waziri wa Nishati mwingine?

Yes, Rais kateua waziri wa nishati mwingine, baada ya JEMBE MUHONGO KUAMUA MWENYEWE KWA RIDHAA YAKE KUONDOKA. Ila sisi wapenda maendeleo tungali tunamhitaji sana. Baada ya kupita njia, mwishoni mwa safari yako ya upita njia (ambayo si muda mrefu) utapiga kura za ndiyo kwa JEMBE au sio?
 
Mtabwabwaja sana mwaka huu. Mwanasayansi ndio kaisha tambulika hivyo. Kama vipi panda kazifute hizo Awards alizopewa kama wewe Kipanga zaidi yake!

Kwa hiyo wewe hata kama angevunja sheria na kumbaka mzazi wako kwako wewe ungesema aachwe tuu kwa vile Marekani wanamtambua? Acha akili za kushikiwa wewe! Kwenye utumishi wa umma kuna maadili yake na hata angekuwa nani lazima awajibishwe tuu. Hata huko alikoenda ziko nyadhifa ambazo hata kumshika ta.ko tuu mtu hadharani unaachia ngazi.
 
Muhongo kwisha habari yake,aende akafie mbele.Hatuna mpango naye mwizi wahedi! ma.sa.buri yake yamekomaa!
 
Yes, Rais kateua waziri wa nishati mwingine, baada ya JEMBE MUHONGO KUAMUA MWENYEWE KWA RIDHAA YAKE KUONDOKA. Ila sisi wapenda maendeleo tungali tunamhitaji sana. Baada ya kupita njia, mwishoni mwa safari yako ya upita njia (ambayo si muda mrefu) utapiga kura za ndiyo kwa JEMBE au sio?
Hata wakati wa kupiga kura nitapita njia tu
 
Yes, Rais kateua waziri wa nishati mwingine, baada ya JEMBE MUHONGO KUAMUA MWENYEWE KWA RIDHAA YAKE KUONDOKA. Ila sisi wapenda maendeleo tungali tunamhitaji sana. Baada ya kupita njia, mwishoni mwa safari yako ya upita njia (ambayo si muda mrefu) utapiga kura za ndiyo kwa JEMBE au sio?

Muhongo Hoyeeeee! Kama vipi wakajitundike tutawakuta huko huko!
 
Back
Top Bottom