Taasisi za Kiislamu zaisafisha CHADEMA

TAASISI ya Kiislamu ya Islamic Peace Foundation (IPF) kwa kushirikiana na Baraza la Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI), zimesema Chadema si chama cha kidini.

Tamko hilo walilitoa jana kwa vyombo vya habari na kudai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na dhana waliodai imeenezwa katika jamii ya Watanzania na Waislamu nchini kuwa Chadema ni chama cha kidini.

“Tunatoa mwito kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuipuuza dhana hii na kuwapuuza wale wanaoieneza ili tuwaunge mkono watu wote wanaotetea maslahi ya wanyonge na rasilimali za taifa letu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa IPF, Shehe Sadik Godigodi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi wa taasisi hizo baada ya kutafakari dhana hiyo na hatima ya Taifa, wamebaini kuwa hakuna ukweli wowote wa jambo hilo bali ni propaganda.

Taarifa hiyo pia imewataka Watanzania kupuuza propaganda hiyo kwa kile ilichodai kuwa haikuanzia Chadema, bali katika Chama cha Wananchi (CUF).

Shehe Godigodi alidai kuwa CUF ilidaiwa ni ya kikabila na kidini (Uislamu) na kuleta athari kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.

“Hali kama hiyo sasa tunaiona inajitokeza ndani ya Chadema ambacho mwanzo kiliitwa cha kikabila kwa maana ya chama cha Wachaga.

“Lakini baada ya chama hicho kuimarika katika uchaguzi wa mwaka 2010 kama ilivyokuwa kwa CUF, kikabadilishiwa wimbo na kuwa chama cha udini yaani Ukristo,” ilieleza taarifa hiyo.

Viongozi wa taasisi hizo katika taarifa yao hiyo wamedai kuwa udini ndani ya Chadema haupo kwa kuwa chama hicho kama vilivyo vyama vingine kina Waislamu, Wakristo na wasio na dini.

Waliwataka Waislamu kutowabagua wenzao walio katika chama hicho kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha matakwa ya dini ya Kiislamu.

HabariLeo:

Mkuu source ni habari leo kweli? wameingiwa na pepo gani hawa mpka waandike habari hii? otherwise,nimekuwa nikisema hapa JF mara nyingi kuwa waislamu wenye akili timamu watafahamu maneno majisafi na majitaka,naona hawa wameonyesha njia kuwa uislamu sio dini ya kipuuzi kama ambavyo BAKWATA na waislamu wengine wanaovyoionyesha kwa watu...
 
Mi nadhani utakuwa mwelewa mzuri in case hauamini kila jambo na unakuwa mtu unaye badilika usiye rigid

halafu uangalie jamii inayokuzunguka kwa uwingi wao wanaaminije au wanasemaje hii itakusaidia sana kukukomboa kifikra maana hapa naona bado fikra zako bado ni za mgando na ni wa mtu kuamini sana uzushi na umbea wowote ule

hujui utendalo wewe,unafata tu mkumbo.hiyo tarifa tunayo na jana mmeufuta ukweli ulotolewa apa kuhusu hao waislam feki na taasisi zao feki maalum kwa ajili ya kuisafisha chaga development manifesto ionekane si ya wakatoliki....leo mmekurupuka toka usingizini mmeleta ndoto zenu apa...wizi mtupu..hao jamaa mtawaongeza sh ngp toka hiyo laki 8 mlowapa?
 
Kwa wale mnaoshabikia udini, basi tukubari kuwa CDM ni chama cha Wakiristo na CCM ni chama
chama cha Waislamu halafu viongozi wetu wakuu wa kidini kama TEC, CCT waanzae kukampain for CDM
na viongozi wakuu wa BAKWATA, BAMITA wakampain for CCM, labda ndiyo mtafunguka akili.
Maana mijutu mingine haiwezi kuona hatari iliyo mbele yetu kuendekeza udini ktk siasa hadi ione kama
Thomaso.

Haya viongozi wetu wa kidini go gooo Wakiristu for CDM, na Waislamu for CCM and CUF, hiyo ndiyo
Tanzania wanayoitamani watanzania.
 
Hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam
Sema haudanganyiki, sio hatudanganyiki!
 
kuwa mkweli ni sifa inayo hitajika sana hapa JF;
  • Mbowe alimpiga huyu jamaa kwa sababu alikuwa mfuasi wa CCM
  • Sumbawanga waliwatenga si kwa sababu hiyo mkuu, Usiwe mdini kihivyo tafuta sababu nyingine ya kuwachukia CDM ila si ya UDINI
  • Unakashifa za rejareja Waislamu feki wakoje au kwa sababu si watu wakujitoa mhanga kuua watu wengine " ufeki wa imani iliyoko ndani ya mtu ukoje usiwe bias kihivyo, tupendane tusigombane

sisi hatugombani ila ukweli ndo unaotenganisha nyeupe na nyeusi...hapa Jf na cdm kwa ujumla ukifatilia vizuri utagundua kuwa komenti na thred nyingi zinawaponda waislam,ccm,cuf na gazeti la habari leo,tbc 1 na associates.nashangaa leo taasisi feki zinatumika kuwadanganya muslems na chanzo ni habarileo!be critical mkuu..
 
Waislamu siyo wajinga kiasi hicho. IPF na BATAMIKI siyo wasemaji wa waislamu, these are just institutions. Kawambie waislamu wa Mtambani maneno hayo kama hujatoka na ngeu. Wale ndo wanaijua vizuri CHADEMA na tafiti wamefanya wanajua ukweli kuhusu Chadema siyo tu kwamba ni cha kidini na cha familia bora hata kingekuwa cha kikabila. Mtambani noma bwana wanajua mpaka fedha za CDM zinatoka wapi. Waislamu tusidanganyike , Huyo GODIGODI kishalishwa. Hivi hana uhusiano kweli na Prof. Safari?

wewe ni mjinga kweli
 
...hapa Jf na cdm kwa ujumla ukifatilia vizuri utagundua kuwa komenti na thred nyingi zinawaponda waislam,ccm,cuf ..
Mkuu usichanganye JF na CDM. Nakubali ukisema "hapa JF" kwa kuwa ni kweli hapa ni JF, lakini sikubali ukisema "hapa CDM" kwa kuwa hapa si CDM !! Ukilitambua hilo ndio utagundua kuwa hata kama kuna michango ya kuwashambulia waisilamu, CCM na CUF, basi hiyo ni michango ya wana-JF, kwa kuwa hii ni JF, lakini sio michango ya CDM, kwa kuwa hii forum si ya CDM, ni ya wana JF !!
 
Kwa wale mnaoshabikia udini, basi tukubari kuwa CDM ni chama cha Wakiristo na CCM ni chama
chama cha Waislamu halafu viongozi wetu wakuu wa kidini kama TEC, CCT waanzae kukampain for CDM
na viongozi wakuu wa BAKWATA, BAMITA wakampain for CCM, labda ndiyo mtafunguka akili.
Maana mijutu mingine haiwezi kuona hatari iliyo mbele yetu kuendekeza udini ktk siasa hadi ione kama
Thomaso.

Haya viongozi wetu wa kidini go gooo Wakiristu for CDM, na Waislamu for CCM and CUF, hiyo ndiyo
Tanzania wanayoitamani watanzania.

mimi sijui cha ccm apa,rais wa kwanza wa tz alikuwa mkiristo na watanzania wote tulimkubali,mkapa ni mkristo tumemwamini wote hawa wanatoka ccm.kwa ivo huwezi kuinasibu ccm na uislam ni kujidanganya na kupotosha umma.CHAGA Development manifesto ndio imejikita kanisani na hilo wao wanalikubali..nashukuru pia na wewe umekubaliana na hilo,sasa cdm isajiliwe kama taasisi ya kidini badala ya chama cha siasa...
 
Mkuu usichanganye JF na CDM. Nakubali ukisema "hapa JF" kwa kuwa ni kweli hapa ni JF, lakini sikubali ukisema "hapa CDM" kwa kuwa hapa si CDM !! Ukilitambua hilo ndio utagundua kuwa hata kama kuna michango ya kuwashambulia waisilamu, CCM na CUF, basi hiyo ni michango ya wana-JF, kwa kuwa hii ni JF, lakini sio michango ya CDM, kwa kuwa hii forum si ya CDM, ni ya wana JF !!

sawa mkuu lakini kawadanganye watoto na wale wasiofuatilia na kuchambua mambo...
 
Sema haudanganyiki, sio hatudanganyiki!

kwa hiyo mtawadanganya hao kwa izo laki 8 tu au mtawaongeza mana makubaliano ilikuwa dau litaongezeka kazi ikiwa na ufanisi...je hizo taasisi mpya sijui ppf,mara ips,sory ipf...usajili wake umekamilika au inafanya kazi ktk mazingira ya dharura kwanza.
 
sisi hatugombani ila ukweli ndo unaotenganisha nyeupe na nyeusi...hapa Jf na cdm kwa ujumla ukifatilia vizuri utagundua kuwa komenti na thred nyingi zinawaponda waislam,ccm,cuf na gazeti la habari leo,tbc 1 na associates.nashangaa leo taasisi feki zinatumika kuwadanganya muslems na chanzo ni habarileo!be critical mkuu..

kwako wewe JF ni CDM, na CDM ni adui wa uislam, na wewe ni member wa JF, kwahiyo wewe ni CDM, kwa maana nyingine wewe ni adui wa uislam, malaria sugu ikipanda sana kichwani huwa haina dawa.
 
Hii JF kwa CDM!! Lol..naona kila kukicha ni habari za CDM tu..hivi TZ kuna chama kimoja tu cha upinzani?
 
Waislamu siyo wajinga kiasi hicho. IPF na BATAMIKI siyo wasemaji wa waislamu, these are just institutions. Kawambie waislamu wa Mtambani maneno hayo kama hujatoka na ngeu. Wale ndo wanaijua vizuri CHADEMA na tafiti wamefanya wanajua ukweli kuhusu Chadema siyo tu kwamba ni cha kidini na cha familia bora hata kingekuwa cha kikabila. Mtambani noma bwana wanajua mpaka fedha za CDM zinatoka wapi. Waislamu tusidanganyike , Huyo GODIGODI kishalishwa. Hivi hana uhusiano kweli na Prof. Safari?

Huu ni upuuzi mwingine tena!
 
Wewe mpuuzi waambie hao masheikh wa mtambani nao waje na tamko lao. Waseme yote wanayoyajua kuhusu cdm au mnatangaziwa huko mtambani tu.. Nyie ndo mnaufanya uislam uonekane kama dini ya wahuni. Kila mwislam akijua kusoma quaran anajitenga na msikiti wake na kundi lake bila msingi wa kupinga wenzake. Tupinge mambo kwa ushahidi sio misimamo yakukaririshwa kama mtoto mdogo.
 
Back
Top Bottom