Taasisi za Kiislamu zaisafisha CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
TAASISI ya Kiislamu ya Islamic Peace Foundation (IPF) kwa kushirikiana na Baraza la Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI), zimesema Chadema si chama cha kidini.

Tamko hilo walilitoa jana kwa vyombo vya habari na kudai kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na dhana waliodai imeenezwa katika jamii ya Watanzania na Waislamu nchini kuwa Chadema ni chama cha kidini.

“Tunatoa mwito kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuipuuza dhana hii na kuwapuuza wale wanaoieneza ili tuwaunge mkono watu wote wanaotetea maslahi ya wanyonge na rasilimali za taifa letu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa IPF, Shehe Sadik Godigodi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi wa taasisi hizo baada ya kutafakari dhana hiyo na hatima ya Taifa, wamebaini kuwa hakuna ukweli wowote wa jambo hilo bali ni propaganda.

Taarifa hiyo pia imewataka Watanzania kupuuza propaganda hiyo kwa kile ilichodai kuwa haikuanzia Chadema, bali katika Chama cha Wananchi (CUF).

Shehe Godigodi alidai kuwa CUF ilidaiwa ni ya kikabila na kidini (Uislamu) na kuleta athari kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.

“Hali kama hiyo sasa tunaiona inajitokeza ndani ya Chadema ambacho mwanzo kiliitwa cha kikabila kwa maana ya chama cha Wachaga.

“Lakini baada ya chama hicho kuimarika katika uchaguzi wa mwaka 2010 kama ilivyokuwa kwa CUF, kikabadilishiwa wimbo na kuwa chama cha udini yaani Ukristo,” ilieleza taarifa hiyo.

Viongozi wa taasisi hizo katika taarifa yao hiyo wamedai kuwa udini ndani ya Chadema haupo kwa kuwa chama hicho kama vilivyo vyama vingine kina Waislamu, Wakristo na wasio na dini.

Waliwataka Waislamu kutowabagua wenzao walio katika chama hicho kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha matakwa ya dini ya Kiislamu.

HabariLeo:

Inaonekana kuna U turn kwa hawa wenzetu hebu someni tamko lao la mwezi uliopita
BATAMIKI kufanya dua ikiwa CHADEMA haitaomba radhi

Kauli CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, zimechukua hatua mpya baada ya Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo.

BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.

Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.

Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.

Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.

“CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.

“Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,’’ alisema.

Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.

“DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.

Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: “Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.’’

Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.

Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.

“Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,’’ alisema.

Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).

Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.

Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.

“Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,’’ kilisema chanzo hicho.

Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.

Source:
Wavuti - Habari

My take, Mtajulikana na kila mtu kuwa hamna mwelekeo, mmepotoka na mtaliangamiza taifa hili, mnataka wakristo pia watoe tamko ili mpate pa kusemea kuwa CHADEMA ni chama cha kikrsto! Mlachemshije!
 
Ahsante Sheikh GodiGodi, umefunguka baba sasa tusonge mbele daima hadi pale utu wwetu waafrika utakaporudi mikononi mwetu. Propaganda za kidini, kikabila hazina nafasi kwenye nchi zilizoendelea, zinatumiwa kwenye nchi zisizoendelea ili hizi nchi ziendelee kuwa makoloni ya nchi zilizoendelea.

Ni maneno machache lakini ya maana kubwa katika jamii yetu!!
 
Hongerani sana IPF na BATAMIKI sisi tulio pembeni tulikuwa tunawaona mnatumiwa na wasioitakia mema nchi yetu, lakini sasa kwa tamki hili mmeonyesha uwezo wenu wa kutafakari jambo japo mmechelewa sana...

Sitaki nirudie matamko yenu ya nyuma maana nitakuwa natonesha kidonda, leo naomba niakikishiwe tu kama BATAMIKI walikuwa hawatumiwi kisiasa.

Vipi mbona hawakuyasema haya wakati wa uchaguzi mwaka jana na hata wakati wa uchaguzi wa Igunga!!?? Najua mmekaa chini na kuona kwamba siasa za kidini hazitaijenga nchi zaidi ya kuibomoa... Wakristo na Waislamu tuishi kama tulivyokuwa mwanzo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.
 
Hongerani sana IPF na BATAMIKI sisi tulio pembeni tulikuwa tunawaona mnatumiwa na wasioitakia mema nchi yetu, lakini sasa kwa tamki hili mmeonyesha uwezo wenu wa kutafakari jambo japo mmechelewa sana... Sitaki nirudie matamko yenu ya nyuma maana nitakuwa natonesha kidonda, leo naomba niakikishiwe tu kama BATAMIKI walikuwa hawatumiwi kisiasa. vipi mbona hawakuyasema haya wakati wa uchaguzi mwaka jana na hata wakati wa uchaguzi wa Igunga!!?? Najua mmekaa chini nakuona kwamba siasa za kidini hazitaijenga nchi zaidi ya kuibomoa... Wakristo na Waislamu tuishi kama tulivyokuwa mwanzo. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.
Nafikiri tuwapongeze kwa kufunguka akili si muda mwafaka wa kuanza kuulizana kwanini hawakusema mwaka jana au juzi, ni sawa na mtu aliyeokoka kumuuliza kwanini hakuokoka mwaka jana.
 
Kwa kifupi inapendeza kuyasikia haya maneno kutoka kwa ndugu zetu waislamu, na walaaniwe wale wote wanaoeneza habari za udini wawe wakristo au waislamu kwa maana kamwe udini hautakaa usimame katika taifa hili zaidi ya kutufarakanisha na kutupotezea muda katika kuleta maendeleo na ustawi wa taifa letu sote, njaa haichagui mkristo au muislam, na Mungu aendelee kutuongoza na kutusimamia.
 
  • Thanks
Reactions: PhD
kifo cha nyani miti yote huteleza! Tunakaribisha singo mpya kutoka ccm! Tutaipa promo ya kutosha kufunua upumbavu wao!!
 
Ngoja nione Bakwata watasemaje na wao..kwa maana kila mtu akiamka kule atokako na yeye anatoa tamko..
 
Hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam
 
Bakwata ni jumuiya ndani ya CCM sii ya waislam!

Cha muhimu waislam tuungane kupambana kuitoa CCM ktk vyama vya siasa nchini kutokana na maovu wayafanyayo.

Jamani ndugu yangu juzi kafariki kwa ajali ya ndege arusha kisha hakuna umeme uwanja wa ndege! Wakasubiri angani mpaka mafuta yakaisha. Mpaka leo sijasikia aliyesababisha uzembe huo kuhojiwa wala kuchukuliwa hatua. Yaani raia kupoteza uhai nchi hii kwa uzembe sio tatizo.
 
hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam

itakusaidia au kukuongezea nini ukisema hivyo!chuki unayoipandikiza itaanza kuku cost ktk familia yako!
 
Wanaisafisha au wao ndo wanajisafisha coz wao ndo waliochafuka na udini na kuipendelea CCM, CDM ni wasafi wala hawana udini wala ukabila. Lakin ni vema kama wameona na kujisafisha tunawapa hongera wamejivua gamba na BAKWATA nao watafuata mkondo.
 
Poleni sana ndungu zangu. U are always late like fire brigade!? Moto ukishaanza kuunguza nyumba ndio wanapewa taarifa na hadi wafike, nyumba imeteketea! Ndivyo mlivyotumika Igunga, waliowatumia wameshafanikiwa, nyie ndio mnashtuka.
Ninachoweza kuwaambia kwa sasa ni kuwakaribisha tena kwenye mapambano ya kuikomboa nchi huku mkiangalia mbele kwa makini ili msitumike tena kijingajinga na kuturudisha nyuma.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake (waislamu, wakristo, wapagani, makabila yote na wa kanda zote)!
 
itakusaidia au kukuongezea nini ukisema hivyo!chuki unayoipandikiza itaanza kuku cost ktk familia yako!
hiyo ile thread ya hongo ya laki nane nayo ni propaganda. Tusubiri tutaona ukweli , lisemwalo lipo na kama halipo laja. Acha Mbowe mwenyewe akanushe au wewe ndo msemaji wa CDM?
 
Hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam
Kwani nyie huwa mnatoa ngapi kwa Bakwata.
 
"Tunatoa mwito kwa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuipuuza dhana hii na kuwapuuza wale wanaoieneza ili tuwaunge mkono watu wote wanaotetea maslahi ya wanyonge na rasilimali za taifa letu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa IPF, Shehe Sadik Godigodi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi wa taasisi hizo baada ya kutafakari dhana hiyo na hatima ya Taifa, wamebaini kuwa hakuna ukweli wowote wa jambo hilo bali ni propaganda.

Taarifa hiyo pia imewataka Watanzania kupuuza propaganda hiyo kwa kile ilichodai kuwa haikuanzia Chadema, bali katika Chama cha Wananchi (CUF).

Shehe Godigodi alidai kuwa CUF ilidaiwa ni ya kikabila na kidini (Uislamu) na kuleta athari kubwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.
Who is GODIGODI? ama kweli njaa noma. Fafanua sasa kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Igunga alidhalilishwa au la! Waislamu watakusaka uwaeleze mlikubaliana na nani kutoa tamko kama hilo?
 
Hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam
Hata kwenye kundi la wajinga, kuna mjinga kuliko wenzake! Wenye akili hatuwezi kukushangaa!
 
Back
Top Bottom