Taasisi za Kiislamu zaisafisha CHADEMA

...leo mnawanunua waislam feki kuwasafisha.

kwanza taasisi zenyewe zimeanzishwa lini izo mbona sijawai kuziskia,au ndo kazi maalum ya kuisafisha cdm?


Mkuu upo kijiji gani!? Unasema hujawahi kuzisikia hizo taasisi? Huu ni unafiki wa hali ya juu. Walipokuwa wanatoa matamko ya kwanza mbona hamkuwakana!? Leo unawakataa sababu tu bado unafikra mgando zisizotaka kubadilika.

Tena uwatake radhi kwa kuwadhalilisha viongozi wako wakiroho eti ni waislam feki na wamenunuliwa.

Unatakiwa ubadilike mkuu. Sisi tunasonga mbele, wewe unarudi nyuma. Wake up!
 
Mi niwashukuru tu kwa tamko lao japo wamelitoa wakiwa wamechelewa sana. Tusubiri bakwata tuone wao watasemaje!
 
Jamani mbona hizi taarifa (magazetini) zinatuchanganya?

Hebu soma hapa chini:
[h=2]* Yapewa siku tatu kuomba radhi[/h]*Vigogo wake wamtupia zigo Lissu
KAULI za CHADEMA kuwatuhumu masheikh kuwa wanatumika kuipa ushindi CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, sasa imewatokea puani. Hili linatokana na Baraza la Taasisi za Mikutano ya Kiislamu (BATAMIKI) kuipa CHADEMA siku tatu kuomba radhi kwa kuwahusisha viongozi hao kwenye masuala ya siasa na harakati za kuwania ubunge jimboni humo. BATAMIKI imesema iwapo CHADEMA haitafanya hivyo katika kipindi kilichotolewa, litafanya dua maalumu ya siku saba kumwomba Mwenyezi Mungu awadhalilishe viongozi wa chama hicho na kuwaondoa katika nyadhifa walizonazo.
Awali, uongozi wa CHADEMA ulipewa wiki moja kuomba radhi kwa Watanzania na Waislamu kutokana na kitendo cha wabunge na wafuasi wake jimboni humo kumdhalilisha Mkuu wa wilaya hiyo, Fatma Kimario na kumvua hijabu. Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Profesa Abdallah Safari, alidai Fatma hakuwa amevaa hijabu bali mtandio na kwamba, chama chake kinaamini masheikh wanatumiwa na CCM katika uchaguzi huo ili kuipa ushindi.
Profesa Safari, ambaye awali alikuwa CUF na alijiunga CHADEMA baada ya kuangushwa katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chama hicho na Profesa Ibrahim Lipumba, alidai masheikh walipaswa kuwa na subira.
Katibu Mkuu wa BATAMIKI, Sheikh Sadiq Godigodi, alisema jana kuwa, dua itafanyika kutokana na uongozi wa CHADEMA kushindwa kuwaomba radhi Watanzania na Waislamu.
“CHADEMA kutoa tamko kupitia Profesa Safari kuwa masheikh wanatumika kuipa ushindi CCM, si la kweli.
“Sheikh ni kiongozi wa Kiislamu ana mamlaka ya kutoa tamko kuhusu tendo lolote baya analoliona linafanyika kinyume cha utaratibu, ikiwemo kudhalilishwa kwa Uislamu,’’ alisema.
Alisema suala la masheikh kukemea si la kisiasa, bali lipo katika misingi ya heshima na kuutukuza utu wa Mwislamu.
“DC amedhalilishwa, viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuomba radhi na si kutoa majibu yasiyokuwa na mantiki, huku wakipotosha maana kuhusu hijabu,’’ alisema.
Kwa mujibu wa Sheikh Godigodi, Kuruani inaeleza hijabu kama vazi la staha na linalotambulisha heshima ya mtu mbele ya jamii.
Alisema Sura ya 33 aya ya 59 katika Kuruani inasema: “Ewe mtume waambie wake zako na mabinti zako wote wa Kiislamu wajiteremshie vizuri shungi zao mpaka kifuani mwao kufanya hivyo kutawafanya wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe.’’
Kutokana na hilo, alisema BATAMIKI inamtaka Profesa Safari asitumike kwenye jambo lolote linalohusu dini ya Kiislamu, kwa kuwa viongozi wake wamekwishakosea na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaomba radhi Waislamu.
Akizungumzia dua maalumu, Sheikh Godigodi alisema itasomwa kuanzia Jumanne na masheikh kutoka Uganda, Kenya na Tanzania.
“Endapo hadi Ijumaa CHADEMA hawatakuwa wameomba radhi Jumanne ijayo dua itasomwa kwa mikoa ya Tanga na Dar es Salaam na Zanzibar,’’ alisema.
Aliwataja masheikh watakaosoma dua hiyo kuwa Idrisa Adamu Waridi (Mombasa, Kenya), Mohamed Ismai (Lamu, Kenya), Mahmoud Lugaia (Uganda) na Rajabu Amran (Tanzania).
Katika hatua nyingine, CHADEMA imeanza kumshutumu mbunge wa Singida Kaskazini Tundu Lissu, kwa kushindwa kuomba msamaha kwa Waislamu kuhusu Fatma kuvuliwa hijabu.
Habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema katika kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika hivi karibuni mjini Tabora, iliamuliwa Lissu alimalize hilo kwa kuwaomba msamaha Waislamu.
“Unajua suala hili limefika hapa kutokana na baadhi ya viongozi kuwa wabishi na kuendeshwa chama katika misingi ya ubabaishaji. Wajumbe tulishakubaliana kwa kuwa tulishakosea tulipaswa kuomba radhi na kutoa sababu ambazo nahisi zingeeleweka kwa jamii na si kama ilivyo sasa,’’ kilisema chanzo hicho.
Alisema hatua iliyofikiwa ni matokeo ya ubishi wa Lissu na kuona CHADEMA inaonewa wakati mambo mengine sisi wenyewe ndio tunaojitakia.

JAMANI CHANZO NI HIKI: CHADEMA maji ya shingo
 
GODIGODI nadhani ungesimama kidete kuwataka CHADEMA waombe radhi kwa waliyomfanyia mwanamke wa Kiislamu kule Igunga kuliko kuwasafisha hawa watu baada ya kuhongwa shilingi laki 8. Muogope Mungu na uwe na msimamo.... CHADEMA wataifikisha nchi pabaya dalili ni magwanda wanayovaa... huoni au???????
 
mimi sijui cha ccm apa,rais wa kwanza wa tz alikuwa mkiristo na watanzania wote tulimkubali,mkapa ni mkristo tumemwamini wote hawa wanatoka ccm.kwa ivo huwezi kuinasibu ccm na uislam ni kujidanganya na kupotosha umma.CHAGA Development manifesto ndio imejikita kanisani na hilo wao wanalikubali..nashukuru pia na wewe umekubaliana na hilo,sasa cdm isajiliwe kama taasisi ya kidini badala ya chama cha siasa...
Ndani ya CCM kuna wakristo na waislam makini. Ndani ya CDM kuna wakristo na waislamu makini. Vivyo hivyo katika Taasisi mbalimbali za Umma na kijamii. Huko kote watu hao wanafanyakazi bila kubaguana na wakati mwingine bila hata kuulizana dini zao.
Humu JF pia makundi hayo yapo, lakini utagungua ya kuwa wale wachangiaji makini wanakwepa sana kuyazungumza maneno ya kijinga kama haya yako kwa vile ni fikra potofu na mara nyingi zinatoka kwa watu wasiojiamini au wanaotumiwa kuvuruga kutokana na kuendekeza njaa zao.
Dini ni Imani binafsi, ya mwenzio haikusaidii kuongoka katika ile ya kwako kwa nini usiachane nayo? watu wamejikita kwenye malumbano ya Uislamu na Ukristo kama vile hakuna dini zingine kwa nini kama huo sii ujinga? mbona kuna wahindu,Budha nk hatusikii kelele?
Tuache ujinga na ufinyu wa mawazo, hawa watawala wa ovyo ovyo wataendelea kutumia UDINI kama silaha ya kuvuruga harakati za mageuzi kwa kutugawa. TUUKATAE.
CCM,CHADEMA,CUF na vinginevyo ni vyama vya Watanzania wote bila kujali dini, ila TEC,BAKWATA, BAMITA, CCT nk ndizo Taasisi za dini.
 
Tena wewe kaa pembeni kabisa na wala mimi si mwana-CCM mie CUF dam dam. Inaonekana huna data. Tena usihusianishe POLISI na siasa that is Governmental institute. Hivi unajua maeneo ambayo polisi walitumia nguvu? sasa leo nakueleza ili ukawashauri viongozi wako vizuri. Maeneo mengi ambayo polisi walitumia nguvu ni yale ambayo Katibu wako mkuu na Mwenyekiti wako walipanda majukwaani kuwaambia wananchi wasitii amri ya Polisi. Maeneo hayo ni kama vile Arusha, Igunga, Dodoma, Mara na kwingineko, Sasa kama wananchi walishaambiwa majukwaani wasitii amri na chombo halali cha Serikali what did u expect. Yaani hata ile semina waliyopewa Bungeni na SAID MWEMA ya Utii wa bila kushurutishwa haikuingia akilini mwao. What these type of leaders do we expect in the future?



Hili ni jukwaa la GT! Unapoandika lazima utumie akili na kuziweka kumbukumbu zako sawa.
Polisi walipomkamata mbunge wa cuf huko Tabora, tena mwanamke, wakampiga, kumdhalilisha na kumweka ndani kwa siku nne, nyie cuf ndio mlikuwa wakwanza kulaani na kusema wanatumiwa kisiasa. Leo unasema wewe ni cuf na unawatetea polisi bila aibu. Acha ujinga!?
 
Ndani ya CCM kuna wakristo na waislam makini. Ndani ya CDM kuna wakristo na waislamu makini. Vivyo hivyo katika Taasisi mbalimbali za Umma na kijamii. Huko kote watu hao wanafanyakazi bila kubaguana na wakati mwingine bila hata kuulizana dini zao.
Humu JF pia makundi hayo yapo, lakini utagungua ya kuwa wale wachangiaji makini wanakwepa sana kuyazungumza maneno ya kijinga kama haya yako kwa vile ni fikra potofu na mara nyingi zinatoka kwa watu wasiojiamini au wanaotumiwa kuvuruga kutokana na kuendekeza njaa zao.
Dini ni Imani binafsi, ya mwenzio haikusaidii kuongoka katika ile ya kwako kwa nini usiachane nayo? watu wamejikita kwenye malumbano ya Uislamu na Ukristo kama vile hakuna dini zingine kwa nini kama huo sii ujinga? mbona kuna wahindu,Budha nk hatusikii kelele?
Tuache ujinga na ufinyu wa mawazo, hawa watawala wa ovyo ovyo wataendelea kutumia UDINI kama silaha ya kuvuruga harakati za mageuzi kwa kutugawa. TUUKATAE.
CCM,CHADEMA,CUF na vinginevyo ni vyama vya Watanzania wote bila kujali dini, ila TEC,BAKWATA, BAMITA, CCT nk ndizo Taasisi za dini.
hao waislamu unaosema hapo kwenye nyekundu ni wangapi? Mi naona kama kuna wawili tu, mmoja ni yule mpemba na mwingine anaefanyiwa kila njia atolewe(Zitto)
 
Hadi hapo wantazania watamtambua adui wao ambao anawagawa kwa madhumuni ya kuendelea kutawala, ukombozi wa kweli wa mtanzania utaendelea kuwa ndoto.
 
Hadi hapo wantazania watamtambua adui wao ambao anawagawa kwa madhumuni ya kuendelea kutawala, ukombozi wa kweli wa mtanzania utaendelea kuwa ndoto.
Kumbe tanzania bado utumwa upo? Au ni maneno ya kisiasa kuwahadaa wananchi kuwa wanahitaji ukombozi?
 
Mbowe alimpiga kofi mwangalizi maalum wa kiislam huko hai na kesi ipo mahakamani,sumbawanga wakristo walitengwa kanisani kisa wameunga mkono mgombea mwislam wa ccm,leo mnawanunua waislam feki kuwasafisha.

Kwanza taasisi zenyewe zimeanzishwa lini izo mbona sijawai kuziskia,au ndo kazi maalum ya kuisafisha cdm?

Id unayotumia inaendana na utaahira wako. Sasa mtu unajiita "inauma" kwanini ujinga usiendelee kukuumiza,maradhi ya ubongo yanakuumiza,udini unakuumiza,ukabila unakuumiza,uelewa finyu unakuumiza....kweli "inauma" na itaendelea kuuma
 

Kwanza napenda kuwasalimu wana JF wote.Leo ndio siku mara yangu ya kwanza hapa Jamvini.
Nampa hongera sana huyu Shehe,lakini ukweli ni kuwa wameamua kuwa wazi baada ya kugundua
kuwa kila kikicha wanazidi kukosa mvuto katika jamii.Na hili limeonekana wazi kwa jinsi CUF kule
iginga walivyopigwa mweleka.
Ukabila ulishindwa,Udini umeshindwa.Magamba watakuja na wimbo upi sasa.
Peopleeeeeeeeeeeeeeeessssssssssssssss
 
hujui utendalo wewe,unafata tu mkumbo.hiyo tarifa tunayo na jana mmeufuta ukweli ulotolewa apa kuhusu hao waislam feki na taasisi zao feki maalum kwa ajili ya kuisafisha chaga development manifesto ionekane si ya wakatoliki....leo mmekurupuka toka usingizini mmeleta ndoto zenu apa...wizi mtupu..hao jamaa mtawaongeza sh ngp toka hiyo laki 8 mlowapa?



Hivi hauoni aibu!? Huoni kwamba unawavua nguo viongozi wako wa dini!? Haujisikii vibaya unapotuambia viongozi wanaokuongoza kiroho wamehongwa na unajiita bado mwislamu! Huoni kuwatangazia wasio waislamu kuwa viongozi wenu are that cheap ni aibu kubwa sio tu kwa uislamu bali na kwako pia!

Fikiria kabla hujachangia maoni yako, tena ya kukurupuka maana unabomoa zaidi ya kujenga!
 
Suala la Udini hasa Ukiristo ndani ya Chadema kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki kulikanusha lazima Uwe kichaaa! Chadema inanuka harufu mbaya ya Ukiristo hasa Kanisa Katoliki!
 
hawa wamenunuliwa kwa pesa ndogo sana ili wafanye propaganda ya kuwadanganya waislam.jana kulikuwa na thred inayosema wamehongwa laki 8 si mmeona?hatudanganyiki ht siku moja.cdm na ukristo na uchaga dam dam
ccm ni uislam damdam
 
Kama BAKWATA wamenunuliwa na CCM,basi nayo Chadema imenunua kwa bei poa BATAMIKI na IPF kwa bei poa kwa kuwapa viongozi wa taasisi hizo viroba vya mchele na mafuta ya kula! Chadema lazima iamue yenyewe bila unafiki kuachana na Kanisa Katoliki isitafute vibaraka wa kuikanushia kuwa haina udini! Viongozi wa Chadema wafike waseme sasa Kanisa basi tuacheni tuiendeshe Chadema yetu! Ukiristo Chadema na Uchaga upo bila kificho!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom