Taasisi za fedha za kimataifa zaombwa kuzifutia Madeni nchi za Afrika kupambana na athari zilizotokana na janga la COVID19

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1593065257027.png

Serikali ya Tanzania imeendelea kuziomba taasisi za fedha za kimataifa pamoja na nchi za Jumuiya ya Madola kufikiria kufuta kabisa madeni yaliyokopeshwa kwa nchi zinazoendelea ili fedha hizo ziweze kutumika kupambana na athari zilizotokana na Covid - 19.

Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamamba Kabudi alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa Marais, Mawaziri Wakuu pamoja na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) jana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Mkutano umejadili, masuala mbalimbali ikiwemo, covid19, biashara, uchumi, viwanda, uwekezaji pamoja na mabadiliko ya tabia nchi. April, 2020 Mhe. Rais Dkt. Magufuli aliiomba Benki ya Dunia pamoja na mashirika ya fedha ya kimataifa kuzisamehe madeni nchi zinazoendelea ili ziweze kutumia fedha hizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid 19
 
Hata virtual conference nako bado anawakilishwa?? Basi huenda ile sababu inayotajwa mara nyingi ni ya kweli!!

Kama waziri anaweza kufanya mkutano huo, Rais anaweza zaidi!
 
Back
Top Bottom