A
Anonymous
Guest
Kuna kero kubwa inayowakumba vijana wengi waliokuwa wakijitolea kama waongoza watalii (Tour Guides) katika Taasisi ya TAWA kwa muda mrefu sana. Wapo vijana wamejitolea kwa miaka mingi wakifanya kazi ya kuongoza watalii, wakilitangaza taifa na vivutio vyake, wakiamini siku moja watapata ajira rasmi au kutambuliwa kwa mchango wao.
Lakini cha kusikitisha, wengi wao wanaishia kubaki kwenye kujitolea kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote. Wengine hata hufukuzwa ghafla baada ya miaka ya kujitolea wakidaiwa wamechokwa au nafasi zimejaa.
Hii inaumiza sana kwa sababu vijana hawa wamewekeza muda wao, elimu yao ya utalii, na nguvu zao kuitangaza Tanzania kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi.
Je, ni haki vijana kujitolea kwa miaka mingi bila mfumo wa kuwaingiza kwenye ajira au kuwapa fursa rasmi?
Tunaomba mamlaka husika ziangalie upya suala hili ili vijana wa Kitanzania wanaojitolea katika sekta ya utalii wapate haki, kuthaminiwa, na kuona matunda ya juhudi zao.
Sauti ya vijana isikike.