Taarifa za uongo kutoka BBC

Masai wa Town

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
6,542
Reaction score
23,856
Jioni hii nilikuwa nasikiliza habari za dira ya dunia nimemsikia muandishi wa habari David Nkya, akisema yupo kambi la wakimbizi la Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma

Kwanza hilo kambi halipo, tulilifunga miaka mitatu iliyopita. Akaongeza uongo wake kuwa Tanzania ina makambi matatu ya wakimbizi wakati ni mawili tu.

Wiki iliyopita mtangazaji huyu huyu alisema Kambi la Nyarugusu limepoke wakimbizi zaidi ya 12,000 kutoka DR- Congo! Wakati uhalisia ni kwamba, Hadi Leo tarehe 1, wakimbizi tuliowapokea hawafiki hata 9,000.

Najiuliza tu, Hizi contents za uongo za BBC zinamnufaisha nani?
 
waandikie email
 

Ashughulikiwe kwa kupotosha
 
Ni kweli hakuna kambi ya mtendeli. Nadhani atakuwa amekosea au kuchanganya na kambi ya nduta.
 
Ni kweli hakuna kambi ya mtendeli. Nadhani atakuwa amekosea au kuchanganya na kambi ya nduta.
Baadae alimesisitiza kuwa Tanzania Kuna kambi tatu. Kwahiyo Siyo bahati mbaya
 

Mkuu Kwa nini usiombe u ripota huko BBC ili upeleke taarifa za kweli?
 
Hatuna uhakika kama ni wewe au David Nkya anasema ukweli.Kwanini unalazimisha tukuamini wewe tuu sio yeye?
 
BBC Swahili ni ugoro mtupu
 
Hivi hawezi kukamatwa huyu na kufungwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…