Taarifa za kukamatwa kwa waandishi wa habari jijini Arusha

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Taarifa za kukamatwa kwa waandishi wa habari jijini Arusha

Waandishi wawili Victor Korumba wa Global TV na Alphonce Kusaga wa Triple A FM wanashikiliwa na Polisi Kituo Kikuu, walikuwa wakifuatilia tukio la askari kituo cha polisi sakina kupiga raia jana Februari 23, 2022.

Nimeongea na Mwenyekiti wa Arusha Press Club amethibitisha na sasa yupo Kituo cha Polisi kufuatilia tukio hilo.

Tunaendelea kufuatilia tukio hilo.

Edwin Soko
24.02.2022

Pia, soma:

FMW-b6GXwAYI8RZ.jpg
 
Huyo jamaa Mwenye koti LA suit wakuitwa korumba anapenda masifa balaa aligombea na ubunge Arusha kupitia ccm
 
View attachment 2129774
Inasikitisha sana
 
Huyo jamaa Mwenye koti LA suit wakuitwa korumba anapenda masifa balaa aligombea na ubunge Arusha kupitia ccm
Naona kama hamuweki mambo sawa na stori sawa tukaelewa hali halisi ilivyokuwa badala yake mnatuletea mambo ya masifa,mara ubunge,mara ccm,mara chadema,mara afande.Acheni kututoa kwenye mada.Mmeshatuingiza huko twambieni kilichojiri.

Baada ya kujaribu kujua ni nini, nilipata habari hizi.Bodaboda wanaoendesha shughuli zao halali hasa wa sakina,wamekuwa wakisumbuliwa sana na maaskari waendesha pikipiki na wanaojiita wanamgambo na mara nyingi hujikusanya hapo kituoni kana kwamba ni watuhumiwa bila shughuli yoyote kuanzia asubuhi wanajazana hapo nje kwenye benchi wakisubiri yeyote apite na begi ili wamkamate.

Wanasema hata kama ni mwanafunzi hakatizi hapo,ni lazima begi lifunguliwe na ikizingatiwa kuwa kituo hiki kipo pembeni kidogo sana na barabara ambayo hutumika kwa watembea kwa miguu na magari kila dakika.Wanasema kuna mama mmoja aliyekuwa na asili ya kiarabu (mweupe) waliona akipekuliwa begi lake na mwanamgambo wanaume wawili alipokuwa akibishana nao wakamvutia kituoni,na baadaye alitoka na begi lake akiwa analia.

Wanasema baada ya malalamiko ya wananchi ndipo walipokuja waandishi wa habari kutaka kujua kulikoni hayo malalamiko ya wananchi.

Rc,Dc,Rpc,Mbunge,Diwani,Mkiti wa Kijiji cha Elerai,Balozi na viongozi wa vyama mbalimbali haya malalamiko ya wananchi kuonewa na kupigwa na mgambo wakishirikiana na baadhi ya maaskari yalikwisha siku nyingi.Sasa yamerudi kwa kasi kubwa,kaeni na wananchi wa Sakina hasa hapo Elerai wawape picha halisi kinachoendelea kila siku hapo kituoni.Wanasema jana wakati vurugu zikiendelea,alikuja mama mmoja machinga mwenye pub hapo raskazoni akilalamika kuwa waliingia kwenye biashara yake wakawapiga wateja wake na kumwaga vinywaji vyao.

Wanasema,hao waandishi wa habari walikuja kutaka kujua hali halisi ndipo waliponyanganywa vifaa vyao vya kazi camera na kuanza kupigwa pamoja na wananchi waliokuwa wapita njia.

Sasa najiuliza uccm,uchadema vinahusikaje na matukio ya kipuuzi kama haya.
 
Hawo waandishi wa habari hawana kinga zinazowaruhusu kuendelea na kazi hata kama walionekana wana vunja taratibu? Waandishi wasiokua na mipaka wanafanyaje kazi zao huko Duniani?
 
Back
Top Bottom