Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

ZITTO ni mwanasiasa kanjanja na wote mnaomtete naona mmepigwa upofu na hizo hongo zake,ZITTO alishagundulika kuwa anatumika na mtandao wa TISS sasa leo mnamtetea nini!
 
mimi ndo sisomi kabisa MAWIO yan afadhali usome TANZANIA DAIMA la MBOWE.kwa mujibu wa MAWIO viongozi wa CDM ni MALAIKA hawakosei na Serikali haijafanya chochote kizuri.yan kama GAZETI la UHURU wapinzani wote wabaya nalo silisomi.

kweli kabisa,nashangaa wanaosoma kile kipeperushi ambacho
 
Kutokana na taarifa zilizoandikwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' linalomilikiwa na James Rugemalira, tuhuma dhidi ya Dr. Reginald Mengi alizozielekeza kwa Zitto Kabwe.

Mwami ZITTO KABWE atajibu kupitia mkutano wa Shinyanga utakaofanyika leo.

Sambaza uzalendo wachana na vichukichuki
 
Utajuaje kuwa ni habari ya kijinga?
Silence means Yes.Habari imeandikwa sie pamoja na Mengi tunaamini ni ya Kweli,itakuwa ya uongo pale tu wahusika watakapokanusha,au kulitaka gazeti lithibitishe pasiposhaka

Huhitaji kuwa na degree kugundua habari hile ilitungwa na mtu mmoja aliyekuwa chini ya mti..na kiini cha habari hile ni kumchafua Zitto na kumgombanisha na watu! Nilifurahishwa na jinsi mwanzo walivyo ipuuza habri ile! Rais hawezi kufanya utoto wa vile..hili gazeti kama mnataka lipigwe ban halafu muanze kulalamika kuwa uhuru wa habari una binywa sawa lakini kimsingi ni kupoteza muda kuhangaika na habari ya kijinga kama hile..
 
habari yenyewe ni yakidaku daku tu! nimeisoma haina kichwa wala miguu,Mengi acha kilialia,Raisi ni jalala haiwezekani kila kitu kukanusha,magazeti na majarida yapo zaidi ya 160.

Habari hii ni ya kidaku kwa lengo la kumchafua Mh Rais na Zitto na target kuu ni Zitto. Nilitegemea waipuuze kama kawaida.
 
Kutokana na taarifa zilizoandikwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' linalomilikiwa na James Rugemalira, tuhuma dhidi ya Dr. Reginald Mengi alizozielekeza kwa Zitto Kabwe.

Mwami ZITTO KABWE atajibu kupitia mkutano wa Shinyanga utakaofanyika leo.

Kaijage ni moja ya walimu makanjanja na wasiojitambua na nina mashaka na hii title yako ya ualimu yawezekana ualimu uliosomea sio huu wa kufundisha.
 
Mimi nafikiri lile gazeti linapaswa kupigwa ban na wala Mengi haja mtuhumu Zitto bali amelalamika taarifa kuto kanushwa..ila mtu yeyote akiisoma hiyo taarifa anajua ni ya kutunga..hata hivyo uzushi hule wa kumchafua Rais ulianzia kwenye mitandao humu

Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..

CCM amuoneini huruma, Mzee mengi mnataka kumungoa meno...
 
> Wanasiasa wetu wote wana siasa ya kijinga sana ili uwe mwanasiasa kanjanja unatakiwa kuwa mtu wa fitina, unafiki, uwatumikie mabwenyenye na wala rushwa, mfumo wetu wa siasa bado ni uongo na ubaladhuli mkubwa hapa hakuna msafi wote wala rushwa na waongo wakubwa.
Ni kweli brother!Lakini Wananchi ndio wanaoruhusu hali hiyo.Ingekuwa Mwanasiasa yeyote anaeendekeza UWONGO,CHUKI,FITNA na VISASI Anapuuzwa.HESHIMA INGERUDI....
 
Huu ushirikiano Mpya kati ya Rugemarila (Mtuhumiwa wa Escrow)na Mmiliki wa Mwana Halisi Forum na Mwandishi wa gazeti la Mawio si Salama kwa Rasilimali za nchi.

Katika kuhangaika Mzee Mengi,amemtuhumu Zitto Kabwe kuwa ndiye kampelekea Rais Kikwete taarifa juu ya Mengi Kumshighulikia pindi atakapo staafu.Lengo la habari hii ni mwendelezo wa visasi na vita ya kuhakikisha Zitto anapotea hatimae kufifiza harakati za ACT-wazalendo.

Kwamujibu wa Mengi, Chanzo cha habari hizo ni Gazeti Jipya la 'Taifa Imara' lililoanzishwa Kimkakati.

Gazeti la Taifa Imara lenyewe mnajua linamilikiwa na nani?

Gazeti la Taifa Imara ni Mali ya Rugemalila ambae ni Miongoni mwa watuhumiwa wa Ufisadi wa Escrow waliowaponza Tibaijuka na Werema .

Sasa mtu huyu huyu alianikwa tena hivi karibuni kwenye ziara ya ACT-Wazalendo kuwa kapewa tenda ya Tril 54 kujenga Bandari ya Mwambani corridor kinyemela bila Zabuni hiyo kufuata taratibu za manunuzi.

Rugemalila na genge lake la mafisadi wanaofukarisha taifa hili kila kukicha wanaendelea kutafuta target ya kumsambaratisha Zitto ili waendelee kuliibia taifa bila kukemewa.

Halafu habari yenyewe,Chanzo chake eti ni Mwana Halisi forums.

Yaani Mwana Halisi inayomilikiwa na viongozi wa Chadema (Kubenea) wanaweza kuwa chanzo cha habari ya kuaminika na ikawa njema kwa Zitto?

Hizi ni tuhuma za kutunga,na ndio maana mara kadhaa tumetahadharisha kuwa huu ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi wa Chadema na watu wachafu kama Rugemalila unapaswa kutiliwa mashaka hasa na wazalendo wa mchi hii.

Haya si mahusiano yenye Afya na kamwe hatuwezi kuendelea kuwachekea na kuwaunga mkono.

Vita dhidi ya Ufisadi imemfanya Zitto kupata maadui wengi, Sasa Rugemarila na Kubenea wanashirikiana kupambana na Zitto.

Gazeti la Mawio kila wakiamka hawana habari yoyote zaidi ya Zitto na ACT-Wazalendo.

Kubenea na Anthon Komu wameona nguvu ya kumdhibiti Zitto haitoshi,wameamua kufanya Collaboration na Rugemarila kupambana na Zitto.

Wametunga habari ili kutaka msaada wa Reginald Mengi kwenye hii vita.

Na Mengi bila kufuatilia mmiliki wa Gazeti na Chanzo cha habari (Source) ameamini kichoandikwa.

Tunachoweza kufanya wanyonge wa nchi hii ni kugomea kununua Magazeti yanayoshirikiana na Mafisadi kudhoofisha vita dhidi ya Ufisadi.

Tusinunue gazeti la Mawio,na Taifa imara kutokana na kusaliti Vita dhidi ya Wizi.

Wanyonge bado tunasafari ndefu na tusipoungana aki na Rugemarila watatumaliza na wataendelea kutukejeli kuwa Mil 25 ni pesa za Chai.

Mwobho,unamatatizo ya akili kamanda.!
 
Chadema wameamua kushirikiana na mafisadi ili kumpunguza spidi Zitto hapa ndio wameamua kujionyesha rangi yao harisi.
 
Mimi nafikiri lile gazeti linapaswa kupigwa ban na wala Mengi haja mtuhumu Zitto bali amelalamika taarifa kuto kanushwa..ila mtu yeyote akiisoma hiyo taarifa anajua ni ya kutunga..hata hivyo uzushi hule wa kumchafua Rais ulianzia kwenye mitandao humu

Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..

Umeongea vizuri mwanzoni, mwishoni 'ugonjwa' wako ukakushika ghafla inafaa uanze dose.
 
Kutokana na taarifa zilizoandikwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' linalomilikiwa na James Rugemalira, tuhuma dhidi ya Dr. Reginald Mengi alizozielekeza kwa Zitto Kabwe.

Mwami ZITTO KABWE atajibu kupitia mkutano wa Shinyanga utakaofanyika leo.

Siku zote alikuwa wapi maani hii taarifa ilichapishwa tangu tarehe 23/03/2015?
 
Siku zote alikuwa wapi maani hii taarifa ilichapishwa tangu tarehe 23/03/2015?

Tume washitukia..kweli kama huwezi kuwapiga bora uungane nao..na hichi ndicho kinacho fanywa na wapinzani wa Zitto wameona ni bora kuungana na watu fulani ili kumuangamiza Zitto kisiasa! Mwaka huu lazima mchanganyikiwe mtatunga kila aina ya uongo...
 
Mahaba yako kwa ZZK yamekufanya usifikiri chochote.Mbowe kaingiaje hapo

Yaan huwezi kumtoa mbowe KWENYE hio team Ya kumchafua ZITTO yaan jamaa umeonyesha chuki za waziwazi dhidi ya ZITTO
 
Kumbe gazeti ni la yule jamaa alieshirikiana na mafisadi kugawana mabilioni? Siwezi kusoma gazeti Kama hili mimi.
 
Kwa kweli hii nchi ina filam za kushangaza
kumbe Rugemalira now ana gazeti?
 
Back
Top Bottom