Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi

hiki kituo cha television kina matatizo sana. ila kuna baadhi ya vipindi kwa mfano kipindi cha wanyama, dokumentary, habari za michezo ndo kidogo huwa naviamini, lakini vingine......,duh!!!!!
 
Mimi binafsi sijaisoma report yenyewe lakini niliichosikia TBccm wakisema kimenipa hasira na nikasema kama jaji mzima kasema hivyo basi nchi hii ina shida kubwa sana
Hicho cha TBC ni upotoshaji mkubwa, kuna haja ya kudai TBC ifungiwe kwa kupotosha kwa makusudi report muhimu kama hii.

ITV wameonyesha vizuri hiyo habari, ukiweza angalia marudio saa 5 usiku huu au kesho asubuhi.
 
huwa nashangaa sana bajeti ya wizara ya habari inavyopita bila kuongelea upuuzi wa TBC.sio ccm au upinzani!
Kila siku tunaimba TBC TBC TBC kwa nini hatusikilizwi?
 
Nisaidieni mimi mwenzenu, maana nina king'amuzi cha star times ambacho ndani yake kuna channel mbili tu mhimu, chennel ten na TBC, ninafanyeje ili niweze kuaccess chennel nyingine kwa kutumia king'amuzi hiki. vinginevyo itabidi tu nikitupe nitafute kingine, maana huwa daima nikiangalia taarifa za habari za TBC naishia kukereka tu.

sio lazima kununua decoder nyingine. tafuta cable link ya antenna halafu tumia antenna ya kawaida. waya kutoka kwenye antena upitie kwenye decoder yako ya startime na utumie link cable kuiunga kwenye Tv Monitor yako. utapata matangazo thru TV yako na thru decoder kwa ku switch kitufe cha TV/AV. hii ni kama uko maeneo ambayo unaweza kupata matangazo thru antenna, yaani dar & pwani.
 
Hii sentence hapa chini nimeipenda:

"Kuwepo kwa vyama vya siasa ionekane kuwa ni kukuwa kwa demokrasia na sio kuwaniupinzani kwa chama tawala"

Unajua Mkuu wengi wanadhani upinzani ni kwa CCM.. Hata kwenye suala la katiba mpya.. tunaposhauri raisi kupunguziwa madaraka wao wanadhani tunamlenga raisi wao...
ila hii report ya Jaji Manento imetulia..
 
Big up Mzee Mwanakijiji kwa makala yako kuponda tume ya jaji Ihema.............Natumai hii ndo tume ambayo tulitarajia watanzania japo haina nguvu kisheria lakini ukweli umejidhihirisha bayana.
 
ripoti inaonekana kukwepa baadhi ya wahusika kama vile IGP,NCHIMBI,PAUL CHAGONJA, PAMOJA NA ASKARI WALOHUSIKA NA TUKIO HILO LA KINYAMA,ni suala la kipuuzi kumtaja aliyeuawa kuwa ni daud mwangosi bila kumtaja aliyemuua,yeye anaogopwa au mnamficha wa nini?na katika mapendekezo mbona hamuoneshi uwajibishwaji wa waliohusika?kama hiyo tume imefanya kazi kwa uhuru watanzania tunataka msimamo wenu juu ya mauaji ya mwanahabari huyo.
 
ripoti ya kisomi isiyoegemea upande wowote. Je jaji anatetea haki au posho?
 
Hivi sisi Watanzania tulisoma shule za wapi jamani??

Yaani ripoti inaonesha kila kitu kwa uwazi na nani kafanya kosa gani lakini inashindwa kuhitimisha kwa kupigilia msumali wa wa kile kilichopatikana kwenye uchunguzi wenyewe.

Ina maana hatuwezi kuandika hitimisho na mapendekezo (conclusion and recommendations)??

Kwa sababu ukiniletea ripoti kama hii siwezi hata kuelewa inanitaka kufanya kitu gani? Tunahitaji consultant wa kutusaidia kitu kidogo kama hiki??

Why not say kwamba, kutokana na uchnguzi huu...wale wote walivunja haki za binadamu na kuhitimisha maisha ya Mwangosi kikatili (Kamuhanda na timu yake + mtuhumiwa ambaye watu wengi wamekuwa hawamtaji Tendwa) wachukuliwe hatua za kisheria?

Why not say, wale waliojaribu kupotosha umma wawajibishwe?

And why not hit them kwamba, hakuna anayetakiwa kubaki pale wizara ya mambo ya ndani?

Inakera sana kwa kweli....ripoti inakuwa kama inabembeleza bembeleza mtoto alale!!
 
Kwangu ripoti hii ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
Kama haiwezi tutoa mapendekezo ya waliovunja sheria wafanywe nini sidhani kama ina umuhimu wowote mbali na kuwa ngonjera kama ngonjera nyingine.
Nakumbuka ni tume hii hii iliyodharauliwa si na rais tu bali hata na mkuu wa wilaya wa serrengeti miaka ile na ni tume isiyo na meno yoyote.
Tupa kuleeeeeeeeeee kabisaaaaaaa
 
hii ripoti mbofu kabisa

."Tume imejiridhisha kuwa tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi
limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora......

kutumia neno "limegubikwa na ukiukwaji wa haki" sio sawa na kusema "kifo cha daudi ni ukiukwaji wa haki za binadamu". halafu eti wanadai wao ni idara huru ya serikali...uhuru gani kwa ripoti kama hii? mbona hawapendekezi waliokiuka hiyo haki wachukuliwe hatua?

Laiti kama yule DC ALbert Mnali ndio angekuwa bosi wenu.........
 
Back
Top Bottom