Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi

Baada ya hizi tume kitu gani kitafuatia au ndio itaishia watu kulalamika tu.
Mkuu wangu unategemea nini ikiwa siku zote report ya TUME ndio hukumu ya mwisho..Lini tumevuka swala hata moja baada ya report ya tume kutolewa?. Tusubiri tu tume ya Waziri mkuu, Chadema na pengine ya JK..
 
Kilichotusaidia kwenye report hii ni huyu mtuhumiwa muhimu ambaye mara zote amekuwa akisahaulika wala hatajwi na si mwingine bali ni Bwana John Tendwa.

Mkutano waliofanya CCM Bububu na hawakuingiliwa nao ni msumari mwingine kwa hawa Wauwaji, mimi nadhani report hizi hata ningekabidhiwa mimi kazi ya kuziandaa nisingepata shida yoyote. kila kitu kiko open n clear, labda tu kama Watanzania tumezoea kekundu keusi ndio muendelee kusubili jipya.
Huyu John Tendwa ni dhahiri sasa ni janga la Taifa. Kwa kuwa bila shaka yoyote siku zote amekuwa akifanya upendeleo wa wazi kwa CCM, kama atakuwa muungwana na kulinda hadhi ya ujaji alionao ni vyema sasa hivi, bila kuchelewa, akafanya uamuzi wa busara kujiuzuru nafasi yake ya usajili wa vyama na kumkabidhi barua ya kujiuzuru aliyemteua ambaye ni JK. Kwa kuwa ni dhahiri amedhindwa jukumu lake kubwa ambalo ni kuvilea vyama vyote vyenye usajili wa kudumu, bila upendeleo wowote!!
 
hi ripoti imekaa sawa kama ya kimataifa vile.manento ni jembe la ukweli .big up jaji wa ukweli .kwa mfano huu tanzania tutaweza kuendelea
 
tindu lissu was right,angalieni tofauti ya quality kati ya report ya jaji mstaafu mh manento na yule wa tume ya nchimbi!!!!
Was very right indeed, Jaji ihema hajawahi kuandika hukumu, kwa hiyo inawezekana hii report ni ya kwanza kwake kuandika. Ukiwa kilaza ni kilaza tu, Nchimbi naye kilaza anachagua kilaza mwenzake kufanya kazi ya kisomi, wapi na wapi bana.
 
Huo ni Muhtasari wa taarifa.
Tafuta taarifa kamili ndio uhitimishe.
Muhtasari sawa!!hivyo unataka kunishawishi kuwa kwenye ripoti kamili maneno hayo hapo juu hayatakuwepo??nazungumza kwa kadiri ya hichi nikionacho,nikiipata hiyo ripoti kamili nata bold hichi nilichokiona hapa.
 
Huyu John Tendwa ni dhahiri sasa ni janga la Taifa. Kwa kuwa bila shaka yoyote siku zote amekuwa akifanya upendeleo wa wazi kwa CCM, kama atakuwa muungwana na kulinda hadhi ya ujaji alionao ni vyema sasa hivi, bila kuchelewa, akafanya uamuzi wa busara kujiuzuru nafasi yake ya usajili wa vyama na kumkabidhi barua ya kujiuzuru aliyemteua ambaye ni JK. Kwa kuwa ni dhahiri amedhindwa jukumu lake kubwa ambalo ni kuvilea vyama vyote vyenye usajili wa kudumu, bila upendeleo wowote!!
Jaji Liundi wakati akiwa msajili wa vyama, siku chache tu baada ya kuachia ofisi ya msajili wa vyama vya siasa alichukuwa fomu CCM kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki na Magamba kama kawa kama dawa wakampiga chini.

Hakuna mtu wa kunishawishi kwamba Tendwa si kada wa CCM hell no, Wilson Mukama wakati akiwa yeye akiwa ndio mwenyekiti wa bodi ya Daily News, Gazeti lao lilitowa tahariri kwamba Dr Slaa kamwe hawezi kuwa Rais 2010, je unadhani ilikuwa ni bahati mbaya? Mukama leo yuko wapi?
 
Hiki kipengele vipi, hebu someni hapo....

Elimu ya vyama vya siasa na sheria ya Polisi kuhusu vyama vya siasa itolewe kwa askari polisi ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa

Sio kwamba CCM wanaitumia hii umbumbumbu kujipatia unfair advantage? Maana Ignorantia juris neminem excusat..
 
Muhtasari sawa!!hivyo unataka kunishawishi kuwa kwenye ripoti kamili maneno hayo hapo juu hayatakuwepo??nazungumza kwa kadiri ya hichi nikionacho,nikiipata hiyo ripoti kamili nata bold hichi nilichokiona hapa.

hi ripoti imekaa sawa kama kimataifa vile.ni ya hadhi ya juu na iliyo tukuka .ni ya mfano wa kuigwa .hongera manento jaji wa ukweli .big up .kwa mfano huu tutaendelea .
 
makamu mwenyekiti msaidizi wa hiyo tume ya utawala bora amechakachua report nzuri iliyotolewa kwa maneno mbofu mbofu.
 
Namshukuru Jaji mstaafu Manento kwa kujitofautisha na Jaji uchwara Ihema yule wa tume/kamati ya kipumbavu ya Nchimbi.
 
Hii ni ripoti ya akili hata kwa ufupisho wake. Kwani imejibu maswali ya msingi ambayo Ripoti ya Uchimvi imeshindwa hata kugusia. Kinachoshangaza ni kuwa wote waliangalia kitu kile kile!!!
 
Hii team ya Tume za haki za binadamu wamefanya uchunguzi kwa week moja tu (13-19 Sept) na walikuwa watu 3 tu!. Pamoja na kwamba tumepata muhtasari (naamini report nzima itawekwa hapa JF baadae) lakini mtu anaona kichwa na miguu clearly.

Tofauti na ile ya Jaji Ihema, hii report inasema ni kifungu gani cha sheria kilikiukwa na nani alifanya ukiukwaji huo.

Nasubiri kwa hamu report nzima.
 
Wana Jf, Nilishapoteza hamu kuangalia Tbc tangu aondoke Tido,lakini leo nikajisahau nikaangalia.Taarifa ya Tume ya haki za Binadamu imechakachuliwa kwa kiasi kikubwa na kituo hiki. Wanasema Tume imesema watu waliokuwepo ktk eneo la tukio walivunja haki za binadamu.hawakuwataja kabisa hao watu tofauti na Jaji Manento aliyewataja wahusika wa uvunjifu wa haki hizo.huu ni utumwa wa shetani CCM.
 
Hii ni ripoti ya akili hata kwa ufupisho wake. Kwani imejibu maswali ya msingi ambayo Ripoti ya Uchimvi imeshindwa hata kugusia. Kinachoshangaza ni kuwa wote waliangalia kitu kile kile!!!
Na kilichokuwa kinanikera mimi ni kwa mtuhumiwa muhimu John Tendwa kutokutajwa kwenye zile report mbili za awali, kichekesho leo Hussein Mwinyi amewasimamisha kazi vigogo wa Msd ili kupisha uchunguzi wa kashfa ya ARV bandia, nikajiuliza ni kwa nini hawa viongozi wa Polisi walibakia ofisini wakati wa uchunguzi? au tuna Serikali tofauti?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ni vema Tume ya Haki za binadamu wakatoa statement kusahihisha makosa ya TBC1 ili kulinda heshma ya hiyo taasisi (Tume).
 
Back
Top Bottom