Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwitongo, Oct 10, 2012.

 1. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wadau, hii ripoti ina akili. Isomeni mlinganishe na ya kisanii ya Nchimbi.

  Nawasilisha


  MUHTASARI WA TAARIFA YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOPELEKEA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI KILICHOTOKEA SEPTEMBA 2, 2012 KIJIJINI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA


  UTANGULIZI
  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni idara huru ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 129(1)(c) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya mwaka 2001. Jukumu kubwa la Tume ni kulinda, kutetea na kuhifadhi haki za binadamu nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo Tume imepewa mamlaka ya kupokea malalamiko (kwa njia mbalimbali) kutoka kwa mtu yeyote au kuanzisha uchunguzi wake yenyewe endapo itaona kuna uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

  Kwa kuzingatia majukumu hayo, Tume ilianzisha uchunguzi wake yenyewe baada ya vyombo vya habari kutoa taarifa ya tukio la kifo cha Daudi Mwangosi. Tume iliunda timu ya watu watatu iliyoongozwa na Mhe. Kamishna Bernadeta Gambishi akisaidiwa na maafisa wawili, Bwana Gabriel Lubyagila na Bwana Yohana Mcharo. Timu hiyo ilifanya uchunguzi wake kuanzia tarehe 13-19 Septemba, 2012.

  Katika uchunguzi uliofanywa, Tume ilizingatia zaidi masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. Hivyo basi, Tume ilitilia maanani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria mbalimbali za nchi na mikataba ya kimataifa na ya kikanda inayohusu haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.

  Kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya Tume Na. 7 ya mwaka 2001, baada ya uchunguzi huo kukamilika, Tume imeandaa taarifa yake na kuiwasilisha kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.

  Taarifa ya uchunguzi wa Tume imegawanyika katika sehemu kuu nne, ambazo ni:
  Maelezo ya viongozi, watendaji na wananchi waliohojiwa.

  Uchambuzi wa taarifa/vielelezo vilivyopokelewa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu.

  Kwa kuwa tukio la kifo cha Daudi Mwangosi liligusa hisia za jamii, Tume imeona ni vyema kukutana na wawakilishi wa vyombo vya habari ili kutoa taarifa yake.

  2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
  Katika uchunguzi wake Tume imebaini kuwa:

  Tarehe 02/09/2012 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliruhusiwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi (OCD) kufanya mikutano ya ndani na kuzindua matawi mapya. Lakini jioni ya tarehe 01/09/2012 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), alizuia CHADEMA kufanya mikutano iliyoruhusiwa na OCD ambaye ni "Officer In-charge" wa polisi wa eneo husika kama sheria inavyotaka.

  Viongozi wa CHADEMA walikuwa na mazungumzo na Mkuu wa Polisi Mkoa Upelelezi (RCO) na kuruhusiwa kufungua matawi yao bila ya kuwa na mikutano ya hadhara.

  Msajili wa vyama vya siasa aliwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa.

  Wakati shughuli za uzinduzi wa tawi la Nyololo ukiendelea, RPC alifika katika eneo hilo na kuamuru viongozi wa CHADEMA wakamatwe; na kuwa wafuasi wa CHADEMA walipinga kukamatwa kwa viongozi wao.

  RPC aliamuru kupigwa kwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika ofisi za tawi hilo la CHADEMA.

  Baada ya mabomu ya machozi kupigwa, wananchi walitawanyika na kukimbia ovyo; na kuwa marehemu Daudi Mwangosi alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye inadaiwa alipigwa bomu na kufa hapo hapo.

  Daudi Mwangosi aliuwawa umbali wa takriban mita 100 kutoka ilipo Ofisi ya CHADEMA tawi la Nyololo.

  Katika tukio hilo wananchi kadhaa walijeruhiwa kwa mabomu, wakiwemo Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Bwana Godfrey Mushi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Bibi Winnie Sanga na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mufindi, Asseli Mwampamba aliyekuwa akifanya jitihada za kumuokoa marehemu Daudi Mwangosi.

  Kutokana na hayo yote, Tume imejiridhisha kuwa tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

  2.1 Uvunjwaji wa Haki za Binadamu
  Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights of 1948), Mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa (International Covenant on Civil and Political Rights of 1966) na Mkataba wa mataifa ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples Rights of 1981), Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki zifuatazo:
  Haki ya kuishi,
  Haki ya kutoteswa na kupigwa,
  Haki ya usawa mbele ya sheria na
  Haki ya kukusanyika na kutoa maoni.

  CHADEMA ni chama cha siasa ambacho kina usajili wa kudumu. Chini ya sheria ya vyama vya siasa (Cap. 258 RE. 2002), vyama vya siasa vyenye usajili vimeruhusiwa kufanya maandamano na kuwa na mikutano ya kujitangaza baada ya kutoa taarifa kwa "Afisa wa Polisi" wa eneo husika. Baada ya taarifa kutolewa chama husika kinatakiwa kipewe ulinzi na "security agencies" (mawakala wa usalama).

  2.2 Ukiukwaji wa Misingi ya Utawala Bora

  Ili pawepo utawala bora mamlaka zote za serikali ni lazima zifuate utawala wa sheria. Uchunguzi umebaini kuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda tarehe 02/09/2012 katika utekelezaji wa majukumu yake alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa "Officer In-charge" wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

  Aidha, hatua ya Msajili wa vyama vya siasa, Mhe. John Tendwa kuwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa ilikiuka misingi ya utawala bora kwani maelekezo yaliyotolewa ndani ya barua hizo yanakinzana na sheria ya takwimu Na. 1 ya mwaka 2002 inayotoa fursa kwa wananchi kuendelea na kazi zao wakati wa sensa pia ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) Kifungu cha 11(a) na (b) inayotoa fursa kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa.

  Ibara ya 8(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelezea kwamba Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Haki ya Kijamii, aidha ibara 18(b) na (c) ya Katiba inaeleza kuwa kila mtu anayo haki ya kufanya mawasiliano (kutoa maoni/habari) na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake. Haki hii imekiukwa kwa kiasi kikubwa na Jeshi la Polisi katika tukio la Nyololo Mufindi kwa kuwa waandishi wa habari na wafuasi wa CHADEMA walizuiwa na Polisi kufanya shughuli zao za kupata habari na za kisiasa. Huu ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa kuwa hali hiyo inazorotesha au inafifisha uhuru wa habari.

  3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO

  Kwa kuzingatia Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya mwaka 2001 Kifungu cha 15(2)(c) na 28 Tume inapendekeza yafuatayo:

  Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya ziwe makini na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utalawa bora vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali kwenye maeneo yao. Aidha, kamati hizo zihusike moja kwa moja na usalama wa wananchi na mali zao kwa kujadili masuala yote ya kiusalama kabla hatua hazijachukuliwa na vyombo vinavyotekeleza sheria.

  Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waepuke malumbano na vyombo vya dola kwa kutii maagizo yanayotolewa na vyombo hivyo bila shuruti. Pale wanapogundua kuwa pana uonevu au upendeleo ni vyema busara ikatumika ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.

  Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa waepuke kufanya maamuzi au matendo yanayoibua hisia za ubaguzi au upendeleo miongoni mwa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kisheria. Mfano, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya CHADEMA kwa sababu ya sensa wakati huo huo Chama cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wakifanya uzinduzi wa Kampeni huko Zanzibar. Aidha, rai ya Msajili wa vyama vya siasa haikuzingatiwa kwa upande wa CCM Zanzibar huku CHADEMA walishurutishwa na Polisi kutii rai hiyo.

  Demokrasia ya mfumo vya vyama vingi iheshimiwe na kulindwa.

  Elimu ya vyama vya siasa na sheria ya Polisi kuhusu vyama vya siasa itolewe kwa askari polisi ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa.

  4.0 HITIMISHO
  Jukumu la kulinda amani na utulivu ni wajibu wa kila mtanzania, mkulima na mfanyakazi, viongozi wa serikali na watumishi wa umma wote wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Tume inatoa wito kwa watanzania wote kuheshimu haki za binadamu na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utalawa bora. Kwa kufanya hivi Taifa letu litaendelea kuwa na amani na utulivu. Tume inatoa rai kwa jeshi la polisi kutekeleza wajibu wake mkuu wa ulinzi na usalama wa raia bila kutumia jazba.

  Kuwepo kwa vyama vya siasa ionekane kuwa ni kukuwa kwa demokrasia na sio kuwa ni upinzani kwa chama tawala.


  ....................................................
  Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri R. Manento


  MWENYEKITI
  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


  OKTOBA 10, 2012
   
 2. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mh hayo,tunashukuru kwa taarifa,mbona sioni tofauti sana na ile ya MCT?
   
 3. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Isome vizuri, utaona hii imeandaliwa kisomi na kwa uwazi kabisa. Wamenukuu vipengele vya sheria ambavyo Tendwa na kina Kamuhanda wamechemka. Nimeipenda sana. Naamini hata wadau mkiisoma mtaona ina mantiki kuliko ule "uji" tulionyeshwa kwa nguvu na kina Nchimbi!
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Very good! Safi kabisa!
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yale Yale tofauti ni ukweli kwenye repot hii japo haina mapendekezo ya kuwawajibisha wahusika
   
 7. e

  emike JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tindu lissu was right,angalieni tofauti ya quality kati ya report ya jaji mstaafu mh manento na yule wa tume ya nchimbi!!!!
   
 8. Nambukwa

  Nambukwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 243
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kwahiyo??:eyebrows::eyebrows:
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kilichotusaidia kwenye report hii ni huyu mtuhumiwa muhimu ambaye mara zote amekuwa akisahaulika wala hatajwi na si mwingine bali ni Bwana John Tendwa.

  Mkutano waliofanya CCM Bububu na hawakuingiliwa nao ni msumari mwingine kwa hawa Wauwaji, mimi nadhani report hizi hata ningekabidhiwa mimi kazi ya kuziandaa nisingepata shida yoyote. kila kitu kiko open n clear, labda tu kama Watanzania tumezoea kekundu keusi ndio muendelee kusubili jipya.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Baada ya hizi tume kitu gani kitafuatia au ndio itaishia watu kulalamika tu.
   
 11. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Hii nayo ni mbovu kama ilivyo japo haikeri kama ile ya Nchimbi, hii imewekwa kifupifupi mno, ni kama vile iliwahoji watu wawili watatu na kuhitimisha uchunguzi!

  Hii imeweka mkazo kwenye upande wa haki za kikatiba, kitu ambacho kinanifanya nijiulize kama kulikuwa na haja ya kuunda tume/kamati kwa suala ambalo tayari liliisha fafanuliwa vizuri tu na katiba, wangeenda kupitia vifungu vya katiba na ku highlight kwenye vile vilivyovunjwa tu!

  Kwa kifupi wametuletea kilekile tulichokuwa tukikielewa muda mrefu kabisa, hakuna kipya! Sote tunaelewa haki ya msingi ya kuishi, tuliiona ikivunjwa makusudi kabisa pale Nyololo, ingetosha tu kutoa waraka/kauli rasmi ya taasisi hizo zinazo husika na usimamiaji wa haki za binadamu.

  Naweza tu kuwapongeza kwa kuukwepa ukakasi uliojionyesha kwenye ripoti ile ya Nchimbi, na ya MCT as well.
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Pia katika ripoti yake imemshutumu vikali Msajili wa vyama John Tendwa kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi ya upendeleo.

  Source: Ch ten bulletin 7 pm
   
 13. h

  hans79 JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Ripoti?
   
 14. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Ninachoona katika hii ripoti ni weledi wa hali ya juu na kusimama kwenye misingi ya sheria na kuweka unafiki, kujikomba na kujipendekeza pembeni. Cha kushangaza Manento na Ihema wote ni majaji lakini Ihema katika ripoti yake hajapitia hata kifungu kimoja cha sheria zaidi ya mambo ya jumla jumla. Big up Amir Manento umelinda heshima yako.

  Sasa kazi kwa Kamuhanda na Karani Tendwa kujipima wenyewe. Kasoro pekee katika ripoti hii ni kuwa haijaamuru Kamuhanda na Tendwa wakamatwe na kufunguliwa mashtaka ya kukiuka katiba ya nchi mchana kweupe. Kwa ujumla ripoti imemvua nguo Nchimbi na kamati yake ya Kitchen Party. Kweli CCM ni janga la kidunia na viongozi wake style ya akina Nchimbi
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  olyset net

  Na wewe unatubore bana, tume ya haki za binadamu iko siku zote na iko kisheria, na haisubili kutumwa kitu kuchunguza, wewe umeshazoea kujaza taarifa yenye page 80 halafu utumbo mtupu, ni nini ambacho wewe hujaelewa hapo?

  Unadhani Jaji Manento ni wale majaji wa Voda Fasta?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye RED siyo kazi yao. wao wamemaliza jukumu lao na report wanaiwasilisha katika Mamlaka husika, wao Mamlaka husika ndio wanaopaswa kuchukuwa hatuwa.

  Hapa Tendwa anapaswa kuachia ofisi mara moja na mwenzake Kamuhanda na washitakiwe kwa mauwaji, kuna watu wanashindwa kummulika Tendwa kwenye mauwaji haya lakini huyu Mzee ni shetani, nadhani hamjamsahau adithi za huyu kuhusu Washiri kule Arumeru.
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Bora report hii imeweka wazi baadhi ya mambo hasa ubabe wa polisi na upendeleo wa Tendwa!

  Ni aibu kwa tendwa yeye ana jua kuzuia chadema tu huku ccmweli wana tamba!
   
 18. C

  Cipro Senior Member

  #18
  Oct 10, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nadhani huu ni muhtasari tu wa report. hatua za nini kifanyike kwa wakina kamuhanda na wenzake labda itakwepo kwenye taarifa kamili.tuwapongeze kwa taarifa yao.
   
 19. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,964
  Likes Received: 6,736
  Trophy Points: 280
  Tume hii na ile ya MCT, zote zimemtia kitanzini RPC Kamuhanda, na zimeeleza ujweli namna tukio la kuuawa Mwangosi lilivyotokea. Lakini kwa mshangao mkubwa ile ya akina Makunga na mwenzake Jaji Ihema, eti inadai hakuna ushahidi kuwa Polisi wamehusika na mauaji ya Mwangosi, pamoja na picha zote zilizoonyesha muuaji! Sasa ndiyo tunaelewa kwa nini Tundu Lissu alieleza hadharani kuwa ujaji wa Ihema ni feki! Ila ambacho kimewashangaza wengi ni kwa vipi Mhariri maarufu kama Makunga amekubaliana na huo 'utumbo' ulioandaliwa na jaji Ihema!!
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Labda nilikuwa namaanisha wangeshauri hawa jamaa wafunguliwe mashtaka...

  Lakini ukisoma vizuri hiyo ripoti unaona kabisa kuwa kila siku jeshi la polisi linakandamiza utawala bora kwa kuzima haki ya kuandamana na kutoa maoni lakini ni kama hakuna msemaji wa wananchi kwa kuwa mfumo wa mahakama umemezwa na serikali kuu. Anyway nitashangaa sana kama Kamuhanda na Tendwa watabakia ofisini na kupata mishahara inayotokana na kodi zetu mwishoni mwa mwezi huu
   
Loading...