Taarifa ya Msiba...!

PJ tunaomba more info wapi kwa FT? ibada ya mazishi itakuwa kanisa gani some of us are living in Arusha and we would like to attend. thanks
iNFO ZITAKUWA AVAILABLE.
Kwa ufupi ni kwamba marehemu atasafirishwa kuelekea Njombe Iringa!
Kwa huku Arusha wanaishi USA, na ni wazi kutakuwa na taratibu za kuuaga mwili wa marehemu kati ya Jumamosi na JUMAPILI!.
HIYO ndiyo itakuwa nafasi ya pekee kwa tulio Arusha kuagana na shemeji yetu.
Tuko pamoja.
 
Our deepest condolences to Freetown. May God rest her soul in peace.
 
Mungu wangu!nimeshtuka karibia kutoa machozi.moyo umeniuma aisee,mara ya mwisho kuonana na Freetown alinionyesha picha za familia yake wakiwa na furaha sana.nimeumia sana,na namuomba Mungu ampe FT moyo wa subra na ailaze pema roho ya marehemu .Amen
Ooooh!
Too bad!...na inasikitisha!
Basi wewe una kumbukumbu mpya zaidi ya huyu mana, na yapasa umwombee ili akapumzike mahala pa salama!
 
Dah!! Nimepata mshtuko sana, Najua Freetown yuko katika wakati mgumu sasa hivi hasa pale unapompoteza mtu wako wa karibu uliyekuwa unaishi naye ni vigumu sana lakini la zaidi ni kumshukuru Mungu na kumwomba ampumzishe mahala pema shemeji yetu nakumbuka wakati tumekuja Arusha ndipo nilifahamihana na Freetown nampa pole sana kwa msiba uliomkuta tunamwombea sana hasa katika kipindi hiki kigumu anachopitia.

BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

TF.
 
FT Mungu akupe nguvu katika kulikabili hili wewe na binti zako wapenzi. Sisi kama binadamu hatuna namna ya kupunguza machungu yaliyomo mioyoni mwenu lakini yeye atupae pumzi atawaongoza. Mkabidhi yeye.

Pole sana
 
R.I.P mammy, na pole nyingi kwa FT na familia.
 

rip,pole sna mkuu
 
pole sana my best friend,
will call you just now


ngoja.....
 
Nakutakia moyo mkuu hasa kwa kipindi hiki kigumu!
 
Poleni sana na pole FT sana,the bible says SHUKURUNI KWA KILA JAMBO, jipe moyo Mungu atakuwa pamoja nawe
 
Pole sana FT, mwenyezi mungu akupe nguvu, ujasiri na subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mwenzio.
Mrs FT, RIP.
 
dah, Poleni wafiwa, pole freetown. May God give you strength.
 
RIP Mrs Freetown

Pole nyingi kwako Freetown Mungu akupe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
 
oooh inaumiza sana.
mungu amlaze mahali pema peponi,na pia amjalie ndugu yetu utulivu na ujasiri katika kipindi hiko kigumu.
 
Pole sana FT tunajua upo kwenye wakati mgumu sana kwa kuondokewa na mwenzi wako, Tupo pamoja na we kwenye maombi.
Ulimpenda sana lakini mwenyezi Mungu amempenda zaidi, apumzike kwa amani. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…