Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,021
- 2,478
1. Hapo zamani mtaji wa TTCL uliporwa na kina Mwandosya na kupelekwa kampuni mpya ya Airtel, ambayo sasa ni kubwa kuliko TTCL, na mshindani wa TTCL.
2. Kuna wakati, kila mwaka serikali ilikuwa inaleta bilioni 1.8+ kwa ajili ya network operations and maintenance, kazi inayosimamiwa na Head of network operations and maintenance(HNOM), lakini fedha hizo zinabanwa, zinatumika maximum 20%, halafu 80% "inarudishwa Wizarani" kila mwaka, lakini haifiki Wizarani.
3. Wakandarasi wa SASKATEL kutoka Canada, kwa ajili ya kuendesha TTCL,walianzisha muundo wa uongozi ambao ulileta vikwazo vingi vya uwajibijaki kati ya makao makuu na mikoa (prohibitive accountablity framework).
4. Mkurugenzi wa TTCL, Dr. Kamugusha Kazaura, alipoingia TTCL hakuzifanyia kazi institutional power struggle politics, na hivyo zikamwondoa kizembe. Lakini, pia ameacha amesaini mkataba na kampuni ya kukodisha minara inayoitwa Helios, mkataba ambao hadi sasa unaifanya TTCL kudaiwa deni kubwa kuliko mapato yake ya mwaka mzima.
5. Mkurugenzi wa TTCL, Waziri Kindamba, alipoingia akafuta mfumo wa uwajibikaji, na akawa anaendesha kampuni kikachero. Akaajiri watu anaowataka yeye bila kupitia Idara ya Utumishi. Wakosoaji wake wengi wakafunguliwa majalada ya uhujumu uchumi, na wengine kuhamishwa pembezoni mwa Tanzania. Kati ya kesi za kipolisi za kubumba zilizofutwa kwa agizo la Rais Samia, baadhi ziltengenezwa na Kindamba kupitia TTCL. Akawa anatamba kwamba yeye ni mwamba kwa kuwa Rais Samia ni Shemeji yake, yaani ameoa dada yake Samia. Hatimaye yakamshinda, sasa ni RC huko Tanga kwa waimba taarabu naye akiwa mwimba mashairi jukwaani.
6. Mkurugenzi wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga, ni miongoni mwa watu ambao wako vizuri "upstairs." Akipokea taarifa ya uchunguzi anaisoma dakika tatu, kuisahihisha, na ikikamilika anachukua hatua. Tatizo alianguka kwenye makorongo ya watangulizi wake. Lakini pia hakuwa na uthubuti wa kufanya Management by Walkig Around the Unit (MBWA TU)
7. Sasa hivi mashirika ya serikali kama vile Tanesco yanafanya malipo ya mamilioni kupitia Vodacom, Airtel, etc, wakati TTCL ya serikali ipo. Kuna tenda kama vile bandwidth management iliyokuwa imetolewa kwa Liquid Telecoms na baadaye wakanyanganywa, na TTCL wanao uwezo mkubwa wa kuitekeleza. Zote hizi ni fursa za kuiitegemeza TTCL lakini serikali haijaipa TTCL kipaumbele.
8. Tangu 2005, enzi za billimg system ya SOBS, hadi leo enzi za billing system inaitwa CVBS, TTCL haijawahi kuwa na Billing System iliyo na uimara, wala iliyo huru dhidi ya fraud, na financial leakages za kila siku.
9. Mapato mengi ya TTCL yanavuja kupitia mfumo wa kununua mafuta kwa kutumia vituo vya mafuta vya serikali. Huko kuna upigaji wa hatari. Na fraud scheme inayotumika bado inawawangisha vichwa hata wasimamizi wa vituo hivyo. Kuna umafia wa hatari unaendelea kupitia vituo hivyo.
10. Changamoto kubwa zaidi ni mtazamo wa Rais Samia kuhusu TTCL. Anasema imeshindwa biashara ya simu, na hivyo ifanye mambo mengine kama vile kusimamia mkongo wa Taifa. Lakini, hakuna Taifa duniani linaruhusu telecoms sector ianguke mikononi kwa sekta binafsi kwa silimia mia. Kiusalama hili ni tobo hatari. Lakini pia, TTCL wanaweza wakiwezeshwa na kusimamiwa vizuri.
11. Mapendekezo:
(a) Malipo ya mamilioni yanayofanywa na serikali kupitia Vodacom, Airtel, etc, wakati TTCL ya serikali ipo, yafanyiwe kazi.
(b) Wahusika wote waliosababisha deni la matrilioni ya Helios dhidi ya TTCL wasakwe na kubebeshwa zigo. Takukuru, FIU na interpol wapo kwa ajili hiyo.
(c) Tender ya bandwidth management, inayonyozungushwa mitaani na dalali mmoja wa kizanzibari, kwa sababu tu ya kutafuta asilimia kumi, isitishwa, wapewe TTCL, kwa utekelezaji.
(d) TTCL ifanye re-organisation ili kuborseha mfumo wa uwajibikaji (accountability framework)
(e) TTCL itafute billing system inayozuia fraud na financial leakages.
(f) TTCL ipewe Mkurugenzi mwenye kufanya kazi kwa mtindo wa "MBWA TU", yaani Management by Walking Around the Unit.
Nawasilisha
Mama Amon
Mkurugenzi Mtendaji
Dawati la Utafiti la Mama Amon (DUMA)
"Sumbawanga Town"
S.L.P. P/Bag
Sumbawanga
26 Sep 2023