Kule kwetu mganga wa kienyeji alikuwa akiipiga tu ngoma mtaani, mchawi yeyote atakayesikia mlio wa ngoma lazima aibuke kutoka huko aliko kuifuata ngoma, kwa hiyo baada ya muda mfupi tu mtakuta wachawi wameizunguka ngoma wanacheza, basi wanakamatwa kama kuku wa kisasa, na anaanza kunyolewa nywele mchawi mmoja baada ya mwingine
Baada ya Zitto na Kitila kuvuliwa uongozi, mtaona wachawi wengi tu wanaibuka wenyewe, hata wale waliokuwa sio maarufu, ili mradi wameusikia mlio wa ngoma. Kamateni huyu mwingine!
Kumlinganisha mwanamapinduzi John Okello na hili saliti ni sawa na kuyadhalilisha mapinduzi matakatifu ya Zanzibar!Huyu na genge lake la wasaliti ni zaidi ya ma-Yuda eskariote!
Ndugu yangu na mdogo wangu Nyakarungu sina sababu yoyote ya kumung'unya maneno katika hili, hii kazi unayofikiria kwamba unaweza kuifanya umeshashindwa kabla haujaianza. Huu muda unaotaka kupoteza pengine ungepaswa kuutumia kwa ajili ya shughuli nyengine za uzalishaji mali lakini bahati mbaya umechagua shughuli itakayokupotezea muda wako bure. Ni bahati mbaya sana kwamba katika karne hii na wakati huu kuna vijana waliobahatika kusoma hadi viwango vya vyuo vikuu kwamba wanawaza kupata uongozi kwa kujinasibisha na ukabila ama udini. Ni afadhali ungejenga hoja nyingine pengine ungeeleweka lakini hili la kujenga hoja katika dhana ya ukabila haitawasaidia kuwafikisha popote. Na mimi nina uhakika mojawapo ya mikoa ambayo hautaungwa mkono kabisa ni nyumbani kwetu Mara na ukitaka kupata uhakika wa hili nakuomba ukaanzie hii operation yako nyumbani Mugumu kisha ndipo uende mahali kwingine.
Huyu Brigedia Nyakarungu ana wadhifa gani humo cdm?
akili yenye ujauzto........:disapointed:akili ndogo....
Kijana imesema mengi afu yanamaaana sana kwa mtu mwenye akil zake timamu na asie fungamana na siasa za maji taka,mie Kiboko mkuuu naungana naww katka hili,vijana weng mmeshikwa maskio hasa na utendaj wa kigoi goi wa huyo DJ akil ndogo,mie simuin hata kdogo na ndo maaana watanzania walio weng bdo hawaaamin katka siasa za upinzan zaid ya kuwahabikia huku kwenye social media,amken hebu tuyatafute hayo mabadiliko kwa hawa wezi wanafk wanaotumia mwanya wa kuijua chadema mapema kutuibia pesa na kutusababishia vifo sisi wenyewe huku wakilitupia lawama jesh la polis na chama tawala,amken vjana wenzangu achen kuuuyumbishwa na misemo yak ya kishetani.....chadema haiwez shika dolo ikiwa chima ya watu hawa hakika naapa
Mbowe,Slaaa,Lissu na mzeee Mtei