Taarifa kwa umma toka kwa Lema (MB), apinga jeshi la polisi kutumiwa kisiasa

Huo ndio ulinzi shirikishi toka CCM, Arusha inapakana na kwa Karibu sana na Kenya na Wasomali wanaingia wengi tu na kutoka. JK anasema tunaunga mkono Kenya na Mwema anasema tuko Imara huku akiwaomba wananchi kutoa taarifa kuhusu lolote litakaloonekana kutia wasiwasi wananchi.

Swali langu ni kwamba Panya wanaweza kutoa taarifa za hatari kwa Paka? Je, Panya wakitoa taarifa... Paka watafuatilia taarifa au watakula Panya kwanza? Je, Panya watakaribiana vipi na Paka ili watoe hizo taarifa? Je, Paka wanaangalia kweli hatari zilizopo ama wanatumia muda mrefu kuwinda Panya?
 
Polr sana mheshimiwa Lema na wana Arusha wote wanaopigania haki na demokrasia ya kweli. Changamoto za ukombozi mara zote huwa ninyingi na pengine ngumu kidogo katika kukabiliana nazo. Ushindi hupatikana tu kwa kujitoa.

Africa inakumbwa na tatizo moja kubwa na hili linaathiri sana ukuaji wa demokrasia na haki za binadamu. Tatizo hili nikuwa wanasiasa walioko madarakani wanategemea sana watendaji wa nchi ili waendelee kutawala.

Huwazawaidia vyeo kwa kubadilishana na utii uletao uovu katika jamii. Hiki ndicho kiini cha anguko la uwajibikaji Tanzania na Africa. Wapenda haki tuungane na wapigania haki kushinda dhuruma na uonevu huu.
 
Tena huyu jamaa asitibue vichwa vya watu kuna wengine wana wadudu vichwani wakitibuka hakuna anayeweza kumlinda Zuberi siyo hirizi wala hao walioko madarakani anaweza kutolewa kafara kwa namna nyingi sana ambazo hata atumie jeshi lote la polisi mkoani Arusha halitaweza kugundua nani amemdhuru, aache upumbqvu afanye kazi kama OCD na siyo ajifanye kama Kada wa magamba.

NB: Na wewe Mheshimiwa Lema hebu tafuta muda pia ujipange na kuweka mikakati ya maendeleo jimboni mwako maana watu haohao watakuchoka na watakutosa wakaacha vita yako na Zuberi.

Huwa napenda ubabe hasa kwenye serikali korofi na bishi kama hii ya magamba ila Mbunge wangu wakati mwingine siyo dhambi kuzungukwa na watu wenye busara na kupanga maendeleo ya jimbo na siyo muda wote unapopata nafasi ya kuzungukwa na watu unayaanzisha maandamano yasiyo rasmi.
 
Tuombe msaada wa JWT kwa sababu hawa polisi siyo watumishi wa uma bali watumishi wa nafsi zao. Haiwezekani tuendelee kuogopa mwili unaotobolewa na kijiti. Mara mia kuogopa virus vya ukimwi kuliko hawa polisi tunaokaa nao mtaani.

Poleni ARUSHA hii so vita ya Lema bali vita ya wanaarusha waliomchagua Lema.
 
tuombe msaada wa JWT kwa sababu hawa polisi siyo watumishi wa uma bali watumishi wa nafsi zao.haiwezekani tuendelee kuogopa mwili unaotobolewa na kijiti.mala mia kuogopa virus vya ukimwi kuliko hawa polisi tunaokaa nao mtaani.poleni ARUSHA hii so vita ya Rema bali vita ya wanaarusha waliomchagua rema.
Kwani Arusha kuna idadi kubwa ya polisi kuzidi raia? Kama siyo basi watu wachukue hatua ya kuwafanyizia kweli popote wanapoonekana mpaka washike adabu
Mkuu kuna wakati nilikuwa na hasira sana na polisi yaani nilikuwa nikisikia polisi kafa nashangilia kweli lakini kuna siku nikiwa kwenye mihangaiko yangu nilikuta polisi wakisherekea chadema kushinda jimbo la Arusha na hata siku tuna subiri matokeo pale manispaa polisi walikuwa wakituhamasisha tukomae mpaka kieleweke, mimi naona tatizo liko kwa baadhi ya wakubwa kama Zuberi na Andengenye na usalama wa taifa... sijui tufanyaje, hivi samaki mmoja akioza wote wameoza au tumchukue yule alie oza tumtupe.........
 
Ni vigumu sana kutofautisha jeshi la polisi na kundi la majambazi.
Wakati mwingine wananchi wanaona heri kukutana na majambazi kuliko polisi.
 
Wakuu nawakilisha taarifa rasmi kutoka kwa Mhe. G. Lema...
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Nawasalimu nyote.
Nimewaita kutoa taarifa juu ya kilichotokea juzi tarehe 28/10 /2011 baada ya kuhairishwa shauri la kesi ya uchaguzi iliyoko mahakamani dhidi yangu .
Tarehe 27/10/2011 kesi hii ilihahirishwa na Judge A . Mujuluzi kwani usikilizaji wake usingewezekana kwa kuangalia idadi ya watu walivyokuwa wamejaa pale mahakamani ,maagizo yalitoka kwamba shauri litakalofuata mahakama iwe imetayarisha vipaza sauti kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.
Lakini kwa bahati mbaya jambo hilo halikuwezekana kabisa kwa sababu ambazo baadaye Mh Judge alizitolea ufafanuzi mzuri na mawakil wa pande zote wakakubaliana kuendelea na shauri hilo bila vipaza sauti lakini kwa ahadi kuwa mpango huo unatekelezwa haraka na wakati mwingine wa kesi itakapokuja mahakami utaratibu huo utakuwa umekamilika.
Jambo la kushangaza siku hiyo wakati nafika mahakamani nilikuta polisi wengi sana na wamevaa nguo zinazoashiria tayari wako kwa mapambano na watu wakizuiwa kabisa kuingia mahakamani kuanzia geti kubwa na polisi walikuwa wanajaribu kuhoji kila mtu kuwa anakwenda kusikiliza shauri gani na kama mtu angejibu ni shauri la kesi ya uchaguzi basi halikuwa haruhusiwi kuingia mahakamani kuanzia geti la mwanzo wa mahakama.
Nilikata dhambi hii na uonevu huu kwa wapiga kura wangu nilimfuata OCD Bwana Zuberi Mwombeji kuongea naye juu ya jambo hili la kuzuia watu na alikataa kabisa na kusema “ hao watu wanaenda wapi kwani kesi inawahusu ? na yeyote atakaye vuka hawa polisi hapa hatakuwa chambo na kuniambia kuwa hata watu wakija maelfu na maelfu mahakamani lazima kesi hii initie kidole “ ( Zuberi) , tulibishana huku nikijaribu kutetea utu wangu na mamlaka yangu kama Mbunge , ikawa zogo mahakamani muda mrefu bila mafanikio mpaka nilipomuomba wakili wangu aingilie kati kisheria ndipo watu waliporuhusiwa kwenda kusikiliza kesi .
Baadaye baada ya kesi nilikuta wananchi waliokuwa nje ya chumba cha mahakama wakiwa na hasira huku wakilalamika na kwani kwa mara nyingine tena OCD Zuberi alikuwa amewaita tena wananchi PANYA na akiamuru polisi wa ngazi ya chini kwa kusema “sogezeni hao PANYA nyuma”
Lugha hii ni mbaya haikubaliki hata kidogo, niliongea na wanachi na na kukemea lugha hii kwa hasira baadaye nilielekea ofisini kwangu kwa miguu huku nikisindikizwa na polisi na watu wengi waliokuwa mahakamani na baadhi ya watu niliomba tukutane nao ofisini kwangu wengi wakiwa ni viongozi wa matawi na vijana naotarajia kuwa mashaidi katika kesi ya uchaguzi , niliongea nao ofisini kwangu nikawaaga nikaondoka na wachache niliwaacha ofisini kwangu na Katibu wangu na baadhi ya wageni wengine, baada ya muda nilipigiwa simu kuwa polisi wameingia ofisini kwangu na kukamata watu wote , nilimpigia simu Kaimu RPC kumueleza suala hili na yeye alisema ni bora nifike ofisini kwake tuongee jambo hili , nilipofika nilimueleza jinsi OCD anavyoendelea kufanya kazi kibabe, kwa shuruti za siasa na bila busara na kuhumiza watu bila sababu , alinisikiliza kwa muda usiopungua saa nzima na baadae nikifikiri nimeeleweka ghafla niliwekwa chini ya ulizi na kuambiwa nitoe maelezo na kushitakiwa kwa kosa la kuongea watu nje kabisa ya viwanja vya Mahakamani na ofisini kwangu .
Ninafahamu mipango yote ya siri na wazi iliyokusudiwa kwangu na wafuasi wangu , ndio maana sishangai kwamba vyama vingine vinaweza kufanya mikutano na maandamano bila kibali na kuchungwa na polisi na yeye OCD na polisi walipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hilo UVCCM kufanya mkutano na maandamano bila kibali,, Polisi walisema wanataarifa na wametoa onyo kwa viongozi waliohusika.
Lakini mimi Mbunge nimekatazwa hata kutembea kwa miguu kutoka mahakamani na ni lazima nipande gari hata kama nataka kutembea kwa miguu na hata kuongea na Wananchi mahakamani na ofisi kwangu ni kufanya mkutano bila kibali ? Jambo hili limenisikitisha sana lakini moyo wangu huko imara kwani naamini kila matatizo yanayotokana na kupigani haki au usawa matatizo hayo mara nyingi huwa ni mpango wa Mungu juu ya kusudi Fulani.
Kesi ya uchaguzi bado inaendelea, nilichaguliwa kwa kupata kura zaidi ya elfu 56. Wakija takribani asilimia kumi tu ya walionichagua ni watu zaidi ya 5,600. Watu hawa wakija kusikiliza kesi na baada ya kesi wakaamua kuondoka kwa kuelekea mjini na sehemu mbali mbali , je kundi hili la watu wataondokaje mahakamani ili msongamano huu usiitwe maandamano ? Hatuhitaji nguvu kubwa ya jeshi la polisi kutawanya watu wanaotoka mahakamani tunahitaji ulinzi wao na busara zao ili watu wasambae kwa amani “ kwani kusudi la mkusanyiko huu hautokani na nia mbaya bali ni kesi ya uchaguzi ambayo hauwezi kushanga kwanini kuna watu wengi mahakamani.
Matukio mengi ya uhalifu Tanzania huwa yatokei kukiwepo na msongamano wa watu tu bali yanatokea tu pale penye dhamira ya uovu bila hata msongamano , mara nyingi tunasikia taarifa za mabenki kuibiwa , watu kuvamiwa katika nyumba zao usiku na kuchomwa visu na kuporwa mali zao mambo haya huwa yanafanyika tena msongamano wa watu ukiwa usingizini, sio kweli kuwa kila msongamano wa watu ni maandamano au ishara ya vita na uovu ndio maana sokoni na sehemu za ibada huwa hakuna polisi wanaolinda kuepusha msongamano kwani kusudi la msongamano huo unajulikana maudhui yake. Haitoshi kutembea kwa miguu idadi kubwa ya watu kuita maandamano. Maandamo yanatafsiri pana sana.
Hakuna shaka ni siasa ambayo iko wazi juu ya kilichotokea tahere 28/10/2011 kwani sio mara ya kwanza kutoka mahakamani kwa miguu na kuja ofisi kwangu kwani tarehe 21/10/2011 tulitoka mahakamani kuelekea Ngarenaro kwa miguu tena kupitia njia ya polisi , mbona siku hiyo kutembea huko hakuitwa maandamano ? ama kwa vile OCD hakuwepo ? .
Ninatoa wito kwa serikali na viongozi wa jeshi la polisi sio afya hata kidogo mwakilishi wa wananchi kama mimi kuwa na uhusiano mbaya na Jeshi la polisi kwa sababu ya mtu mmoja.
Ndugu wananchi na wanahabari Wakati Fulani huko Nyuma OCD alituma kwa katibu wetu wa Mkoa Meseji kuwa mimi Mbunge nimeandaa mpango wa kumteka mtoto wa OCD na kumuua , Mimi pamoja na Mkiti wetu wa Taifa Mh Mbowe tulienda kumuona RPC na viongozi wengine kujadili na RPC alihaidi na kuona umuhimu wa kukaa pamoja na kujaribu kutafuta uhusiano mwema na suluhu jambo ambalo halikuwezekana mpaka leo kwa sababu pengine za msingi.
Sasa najiuliza nikiwa nimevamiwa usiku au nahitaji polisi kwa msaada wowote ule , je nitakuwa na ujasiri gani wakumuita OCD kwa msaada , kwangu mimi hofu niliyonayo dhidi yake kama kiongozi wa polisi ni kubwa kuliko kukutana na majambazi usiku , hata hivyo” LETS GO, LETS GOD”
Lakini kutafakari kwangu historia mara kwa mara inatia moyo kwamba hakuna harakati ambazo hazikuitwa ukorofi ,uvunjaji wa sheria , uhaini, na ukiukwaji wa taratibu , niweke wazi kwamba nitapinga ukandamizaji wowote ule mbele ya yoyote Yule mwenye silaha yoyote ile na mwenye magereza yenye mateso makali kuliko jehanamu bila woga , na sheria yeyote inayokiuka misingi ya
Kwa kweli nimejiandaa hata kupokea mauti japo najua Mungu anapenda niishi muda mrefu ili kutimiza kusudi lake , sitarudi nyuma katika harakati hizi za kupinga uonevu , dhuluma na ukandamizaji wa haki za binadamu nasubiri kwa hamu sana kuona mikakati yote iliyopangwa kinyume nami na wafuasi wote wanaopinga uonevu. Hata hivyo Nimeiandaa familia yangu kuwa tiyari wakati wowote kwa jambo lolote na kwa taarifa yoyote dhidi ya ukweli tunaoupigania.
Ndugu wanahabari kila mara huwa nawaambia wananchi kuwa dhambi mbaya kuliko zote Duniani ni UOGA. Lazima watambue kuwa wengine watateswa ,wengine watauwawa lakini wengine watafurahia haki na uhuru kamili tunaoupigania hata kama hatutakuwepo kwa sababu tu wengine walipitia mateso mbali mbali. Mimi natambua kuwa faida ya kuishi sio kuishi vizuri tu wewe na familia yako bali ni wewe kuwa sehemu ya mabadilikio ya watu wanaokuzunguka , katika kupigani UTU , HAKI , ustawi mzuri wa Jamii. Na kila mtu anayemuogopa Mwenyezi Mungu ataishi kufanya hivyo kama Mahatma Gadhi alivyopata kusema “The best way to find yourself is to loose yourself in the service of others”
Godbless Jonathan Lema (MB)
30/10/2011

My Take: Namna Polisi wanavyoshiriki kuibaka demokrasia ni dhahiri wana maslahi makubwa kwenye siasa za Tanzania. Mahakama Kuu iombwe kuingilia kati hizi HARAKATI za ki- Al Shabab zinazofanywa na Polisi ya Tanzania dhidi ya raia wake. Mwenendo huu ukemewe kabisa
 
Yaani watu wa arusha tutabakia na ushabiki tu kila siku maandamano au mahakamani shida ya mbunge wetu anapenda sifa sana na sifa zenyewe ni za kijinga mara gari aweke namba ni jina lake yani mambo ya ajabu si uwe kama mnyika au zitto.

Wanahoja za msingi juu ya wapiga kura wao hata unaposema upo tayari kufa kwa ajili ya kutetea haki yako wewe na familia yako hivi hata leo hii ukifa kwasababu ya siasa unategemea utaiona hiyo paradiso kwasababu ya siasa never tena sahau habari hiyo kwanza chunguza uliletwa duniani kwa dhumuni lipi usidandie mambo ya mungu na siasa uchwara ambazo hazimtambui mungu

Mkuu tunakuomba upooze kidogo. Mambo ya namba zenye jina lake ndiyo walitakiwa Polisi, tena traffic wamwite wamweleze, na labda wangemwandikia barua.

Sidhani Mkuu kwamba hiyo ndiyo "justification" ya kumsingizia bunge kuwa anapanga mipango ya kuteka nyara watoto wa OCD. OCD mzima unakuwa huwezi kweli kulinda familia yako mpaka utamke haya tena hadharani? Mwishowe atalalama kuwa Mbunge anamtaka mkewe?

Ni nani alikudanganya kuwa Mungu hayuko kwenye jambo lolote? Taja lolote lile? Hebu tupe orodha ya ambayo Mungu huwepo Mkuu na ambayo hayupo!
 
Kamanda Lema nakukubali sana mkuu...Mtu mwenye IQ kubwa utamjua tu kutoka katika kila neno litokalo kinywani mwake, IQ yako iko juu. Mungu akutangulie mkuu...... LETS GO....
 
Igp Mwema ni vema amwondoe Mwombeki Zuberi mapema pale maana kwa haya anayoyafanya anafifisha kabisa ustawi wa Polisi Jamii, wakati wa kampeni last year nilikuwa pale jamaa ni ana zaidi ya personal hatred dhidi ya Lema
 
Kuhusu siasa uchwara muulize rostam wacheni ushabiki jibuni hoja yani lema kila analoongea ni sahihi maana yeye hakosei ni malaika musutumike kama karai la zege nyumba ikiisha linatupwa tumieni akili sio masaburi



Ukibishana na sisi Tunaosapoti Andiko La Lema na demokrasia ulosema tunawaza kwa masaburi na wewe utakuwa "masaburi trained". Maana mbwa bila kuwa trained haezi elewa orders anazopewa na binadam.

Hoja Kubwa hapo ni Polisi waache yafuatayo
1. Kuonea raia
2. Wasiite binadam PaNYA
3. Wasilinde na kutetea chama kimoja tu cha siasa
4. Na sio kila watu wakusanyikapo wajue ni maandamano. Saa ingine weza kuwa ni msiba.
Na pia raia mwenye haki ya kikatiba ya kusikiza shauri lolote mahakamani asizuiwe kuingia eti tu kwa sababu chama fulani kimesema.
 
Jenga utamaduni wa kupitia kwanza jamvini kuona kama unachonuwia kupost hakijatupiwa na wadau wengine. Habari hii ilishawekwa humu tokea saa 7 mchana na Ngurati.
 
Igp Mwema ni vema amwondoe Mwombeki Zuberi mapema pale maana kwa haya anayoyafanya anafifisha kabisa ustawi wa Polisi Jamii, wakati wa kampeni last year nilikuwa pale jamaa ni ana zaidi ya personal hatred dhidi ya Lema

Ameahidiwa cheo hivyo yupo kazini.

Nakubali pia kwa Arusha kunawatu watachukua hilo personal na wala siyo kazi, mwishowe wataipersonalise pale fursa inapotokea
 
Hapa ndipo huwa narudi kwenye hoja yangu kwamba polisi wetu wengi ni failures shuleni, sasa watawezaje kutekeleza shughuli zao kwa mujibu wa sheria na kanuni wakati wanajiona kama wao kuwepo polisi ni favour? Ndipo wanaishia kufanya mambo mengine ambayo ni ya kipumbavu kabisa.

Uliwahi kufuatilia polisi ya Tanganyika waliwahi kushinda kesi ngapi..... mahakamani? Mpaka wakanyanganywa jukumu hilo likarudi kwa Mwanasheria wa Serikali..... failures wazoefu kazini.... Naomba kama mna records nipatie za Kova na Zuberi...!!!
 
cku 1 taifa litakombolewa hata gaddafi alisema wanaompinga ni panya! huyu jamaa kalewa madaraka mwisho wake uko karibu
 
Nafarijika nikiwa Muasisi wa Chadema na Mwenyekiti Taifa wa kwanza, (mstaafu) kwamba Mhe. Godbless Lema ameonyesha ujasiri thabiti katika kupinga uonevu wa wanyonge na ukandamizaji wa demokrasia unaoonekana kuidhinishwa na Serikali ya nchi yetu. Mhe. Lema ameonyesha uzalendo uliotoka moyoni na kujitolea kwake kutumikia umma. Mungu atambariki na kumlinda.

Tamko lake kwa waandishi wa habari lime-cover kikamilifu misimamo ya CHADEMA kama ninavyoielewa na kuiamini, na nina hakika Kamati Kuu ya Chama itaridhia.

Hata hivyo, nionavyo mimi binafsi, Tanzania tunaelekea njia inayohatarisha amani na uhuru wa watu wetu; hasa pale Polisi wanapojiingiza kutekeleza maagizo ya chama tawala na kupindisha sheria na taratibu tulizojiwekea na zinazohakikisha kwamba Mahakama zinakuwa na uhuru kamili kuamua kesi zilizo mbele yao.

Kwa maoni yangu, vituko vya Arusha kuhusu Chadema na maagizo kwa Polisi yanayoashiria kwamba yana baraka za Serikali, yanastahili kujadiliwa na viongozi tuliwachagua, kama jambo la dharura, na tamko kutolewa kuhusu uhuru wa wanachama wa vyama vya siasa kuandamana na kukutana. 'ROLE' ya Polisi katika shughuli za vyama vya siasa ni lazima ifafanuliwe kama uongozi unadhamiria kwa dhati kudumisha amani.
 
Back
Top Bottom