Taarifa kwa umma toka kwa Lema (MB), apinga jeshi la polisi kutumiwa kisiasa

Lema analilia kama mtoto wa chekechea maneno mengi..

Tanzania kuna wabunge zaidi ya 300 kila mmoja awe anatoa taarifa kwa umma si itawa nchi ya maigizo
Kwani taarifa kwa umma unatakiwa utolewe na nani...Lowassa, UVCCM.... pekee ndiyo wana haki ya kutoa taarifa kwa umma
 
Lema, alivyokuwa na upeo mdogo eti anataka wale wote walimpigia kura waende mahakamani, anajua kama hawana kazi ndio maana anasema hayo maneno

hajataka watu wote waende mahakani, ila ametoa taarifa kuwa kachaguliwa na watu 56,000. na iwapo just 10% ya watu hao ambao ni sawa na 5,600 wakiamua kwenda kusikiliza kesi ya mbunge wao, mahakamni watakuwa wengi sana. shauri linapoahirishwa na kila mtu kutawanyika kurudi nyumbani, mtu asiyefikiria vizuri kama wewe utasema wanaandamana wakati wao wanatembea kurudi nyumbani baada ya kesi waliyoifuata kusikilizwa.
 
Kesi haimhusu Lema peke yake ndiyo maana kati ya walioshitakiwa ni pamoja na mwanasheria wa Tanzania....na serikali imetenga bil 14 kwaajiri ya kesi za kupinga matokeo sasa niambie hizo bil 14 ni kodi za mama yako au kodi ya Lema....acha kukurupuka na isitoshe mwisho wa siku wananchi wa Arusha ndiyo watakao takiwa kutoa ushadi kama lema alituka ama alah sasa kama utakuwa unawazuia kuinga watafatiliaje.............au wafatilie kupitia magazeti ya Uhuru, Habari leo

unajua crshwise kuna mijitu humu ndani objectivity haina. ni kuropoka tu. kwani sheria gani imekataza watu kuhudhuria mahakani?
 
I do hate hawa jamaa wanaotumiwa kama vibaraka kwa manufaa ya watu wachache nina hasira sana na hawa polisi uchwara.. Mh. Lema tupo pamoja mpaka kieleweke.
 
hapo iko aja ya kimsingi kuangalia mwenendo mzima wa kesi. Je uko ugomvi binafsi baina ya Lema na OCS Zuberi au jeshi la polisi au uko mkono wa chama cha siasa kutaka kesi hiyo ionekane kuwa ni ya kawaida isipoudhuriwa na watu wengi. Au ndio dhana ya kuwafundisha wananchi kutii sheria bila shurti. Sote tutafakari kwani haya ni mapambano kutafuta haki na demokrasia ya kweli
 
Kuna haja ya wanazuoni kujitokeza na kutoa msaada wa kimantiki kabisa kwa jeshi la polisi ili kutambua na kuelewa kwa kina majukumu yao. Inaonekana kuna mapungufu ktk jeshi la polisi jambo linalopelekea kufanya kazi kwa presha na bila kuwa na mwelekeo wowote ktk maendeleo ya Nchi.
 
hapo iko aja ya kimsingi kuangalia mwenendo mzima wa kesi. Je uko ugomvi binafsi baina ya Lema na OCS Zuberi au jeshi la polisi au uko mkono wa chama cha siasa kutaka kesi hiyo ionekane kuwa ni ya kawaida isipoudhuriwa na watu wengi. Au ndio dhana ya kuwafundisha wananchi kutii sheria bila shurti. Sote tutafakari kwani haya ni mapambano kutafuta haki na demokrasia ya kweli
Kwani Zuberi ndio kamshitaki? Kwanini hawa CDM wanataka kugeuza hii kesi ionekane kama Polisi ndio wanamuonea Lema?
 
hajataka watu wote waende mahakani, ila ametoa taarifa kuwa kachaguliwa na watu 56,000. na iwapo just 10% ya watu hao ambao ni sawa na 5,600 wakiamua kwenda kusikiliza kesi ya mbunge wao, mahakamni watakuwa wengi sana. shauri linapoahirishwa na kila mtu kutawanyika kurudi nyumbani, mtu asiyefikiria vizuri kama wewe utasema wanaandamana wakati wao wanatembea kurudi nyumbani baada ya kesi waliyoifuata kusikilizwa.

Hivi kweli watu 5,600 Lema anataka waende mahakamani wakafanyaje? kweli hizi akili za kunguru sijawai kuona toka nianze kufuatilia kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge sijawai kusikia mbunge akiwataka waliompigia kura waende mahakamani..

yaani watu waache kazi zao wakashinde mahakamani, anajuaje kama wote waliompigia kura ni Chadema?
 
ipo siku itakula kwake,binadamu muogope kama ukoma Gadaffi yuko wapi,ilichomekwa kijiti mkunduni licha ya kujificha kwenye mtaro wa maji machafu raisi mzima kila kitu kina mwanzo na mwisho kwanza zuberi ninani?mbele ya jamii usilete za kulete za bagamoyo huku utaumia sisi tunakuonya.
 
Nuhru Gandhi, Nelson Mandela, Luther King all went through the same harasment, but they have brough changes in the world. Lema dont gi it up. yoa are a real politician, one day the history will tell.
 
Hivi kweli watu 5,600 Lema anataka waende mahakamani wakafanyaje? kweli hizi akili za kunguru sijawai kuona toka nianze kufuatilia kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge sijawai kusikia mbunge akiwataka waliompigia kura waende mahakamani..

yaani watu waache kazi zao wakashinde mahakamani, anajuaje kama wote waliompigia kura ni Chadema?

Ulitaka waende wangapi?
 
Heshima kwako Chogo Matata.

Mkuu kuna watu wako tayari kutetea ujinga mradi ujinga huo uwe umefanywa na mtu wanayedhani ni shujaa wao.

Nimeongea mara nyingi bahati mbaya sijui sieleweki au lugha niitumiayo imejaa ukakasi.Nilisema na nitaendelea kusema bila kujali nitaeleweka vipi Godbless Lema ni mbunge wa Arusha mjini.

Kachaguliwa kwa kura nyingi au kwa maneno rahisi kura zake zilitosha kabisa lakini Mheshimiwa Lema badala ya kuwatumikia wapiga kura wake amelifanya jimbo la Arusha mjini eneo la harakati kwa kuwatumia vijana wasiokuwa na ajira katika harakati zake.

Mheshimiwa Godbless Lema kashtakiwa mahakama kuu mjini Arusha badala ya kupamabana na kesi amekuwa akihamasisha vijana wa vijiweni wasiokuwa na ajira na wanye ajira zisizo rasmi kumsindikiza mahakamani.

Eneo la mahakama kuu mjini Arusha ni dogo sana kuhimili wingi wa washabiki wake.Nia na madhumuni ya Mheshimiwa Lema ni kutumia kesi ya kupinga ubunge wake kama sehemu ya kampeni kwakuwa anajua mwisho wa kesi ni nini.

Niseme bila kutafuna maneno Mheshimiwa Lema kafanikiwa sana kuwavuta wasiokuwa na akili na wasiojua kwamba kuwepo kwao mahakamani hakutasaidia lolote kama wakili wa Lema atashindwa kumwakilisha mteja wake vyema.

Ukodishaji wa pikipiki zilizotundikwa bendera za chama maana yake nini au ni sehemu ya utetezi wa Mheshimiwa Lema ? Ukusanyaji wa vijana wahuni ambao mara zote wanasababisha msongamano usio wa lazima kila kesi inapohairishwa maana yake nini ?

Mabishano ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote kila kesi inapotajwa inamlazimu Lema kutoa ufafanuzi wa kisheria kwa wapambe wake,Tangu lini Lema kasoma sheria,Je huku si kuingilia uhuru wa mahakama ?

Nilisema kabla mkusanyiko ni mkubwa Lema na wapambe wake wanajua hilo lakini kwa maksudi ya wazi wanaamua kuyaacha magari yao wanaamua kutembea kwa miguu umbali wa zaidi ya kilometa tatu/nne wakisindikizwa kwa nyimbo za kejeli kwa mlalamikaji na pikipiki je hii ni sawa.
 
  • Thanks
Reactions: Omr
Hivi kweli watu 5,600 Lema anataka waende mahakamani wakafanyaje? kweli hizi akili za kunguru sijawai kuona toka nianze kufuatilia kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge sijawai kusikia mbunge akiwataka waliompigia kura waende mahakamani..

yaani watu waache kazi zao wakashinde mahakamani, anajuaje kama wote waliompigia kura ni Chadema?

Lema hajaita mtu, na wanaoenda ni walompigia kura bila kujali tofauti zao. Na mashahidi ni wapiga kura wenyewe walokuwepo kwenye hiyo mikutano ya kampeni anayoshutumiwa lema kuwatukana hao greens. Sasa watamteteaje kama hawajui muendelezo wa kesi kaka?

Kuhusu hayo maandamano ni hivi..

1. Watu walokuwa mahakamani walikuwa wengi sasa saa ya kutoka lazima waonekana mafungu (ikaonekana ni maandamano.)
2. Walokuwa mahakamani wasingeweza kusubiriana atoke mmoja mmoja. Ingewachukua siku nzima au mbili mpaka waishe mahakamani.
3. Kutoka mahakamani mpaka ofisi ya Lema sio mbali hivyo, so Lema aliamua kutembea kwa mguu (yuko huru ni jimbo lake). Kumbuka kuna kina mama wanatembea kilometres wakitafuta maji na dispensary, so hakuna ubaya mbunge kutembea kidgo.
4. Barabara alopita Lema kuelekea ofisi ndio exit road toka mahakamani, hata wewe ungekuwepo ungepita hapo hapo kaka.
5. Ukipita au kukutana barabara moja na mtu unaempenda au ulemchagua haunyimwi kumsabahi au kumshangilia.

Kwa hayo machahce nilowaza kwa upeo wangu mdogo na mnaouita wa "mvuta bangi" bado polisi hawana grounds yeyote wa ku-rule out kuwa kulikuwako maandamano.

Pia Ofisini Kwa Lema ni ofisi ya wanajimbo walomchagua Lema so
1. Wana ruhusa wa kufika pale muda wowote wa kazi kukutana na mbunge wao
2. Lema kama mwenye ofisi ana uwezo wa kualika mgeni yeyote haswa waajiri wake (wapiga kura wake)
Kwa hayo machache pia Polisi hawana uwezo wa ku-rule out kuwa kaalika watu kwa njama.

Kama wafuasi na wote walofika mahakamani hawakuwa hata na fimbo wala viwembe mifukoni, basi walikuja kwa AMANi kushiriki haki yao ya kikatiba. Sioni ground yeyote ambayo polisi ina ruhusa ya kuwanyima haki yao, zaidi wangetakiwa kuwalinda mpaka shauri liishe lakini cha ajabu polisi ndio walikuwa na silaha ready to kill or surpress wananchi. Nani mkorofi hapo?

Kuhusu kuwaita wafuasi kuwa nii wakaa vijiweni.

1. Ni kweli wengi wetu nikiwamo mimi ni wa vijiweni (hustahili kutukumbusha)
2. Tungekuwa wapi pengine? Tungelala home?
3. Tungekuwa shamba lakini mbolea za ruzuku na pembejeo ndio mnalipwa nazo ninyi mnaotutusi leo. Mashambammewapa maswahiba wenu wazungu na viongozi. Unafahamu ya morogoro.
4. Vijiweni atleast tunajadili ya msingi na kupeana deal japo ndogo. Inatusaidia kununa sukari(2300tshs) na chumvi tunarudisha home kwa wazee wetu walotesekea ilokuwa EAC lakini now mnawatukana.
5. Kijiweni ninapopiga viatu rangi na elimu yangu ndio panaponiwezesha kumsomesha mdogo wangu na kumtibu bibi. Wakati ninyi na ndugu zenu mnasoma nje au ndani kwa mkopo 100% na kutibiwa nje au ndani kwa priviledges.

Vijiwe ni vingi kuliko ofisi na ndio vinatulisha. Je hali ikibadilika ukarudi kijiweni utafurahi nikikutenga na kukudharau eti kisa wewe uko kijiweni? Mtu ni Utu.


Kwa niaba ya wapenda maendeleo wote nawasilisha
 
Kitu ambacho sijafahamu ni kama Arusha nako kuna hii kitu ya ulinzi shirikishi na polisi jamii.

Kama hizo shughuli zipo, ni nani anayezihamasisha na kuzi-cordinate kama ocd anawaita wananchi panya?



Mkuu, huku hakuna kitu kinaitwa ulinzi shirikishi wala polisi jamii! Uhusiano wa wananchi na polisi ni mdogo sana.

Hili la kuwaita watu panya limenigusa sana. Ni udhalilishaji wa hali ya juu. Nashauri kama ushahidi upo, wamshtaki mahakamani. Ya mungu mengi. Hakimu anaweza kuushangaza ulimwengu kwa kumtia ndani hata miezi sita tu.

Hapa nimegundua kwamba anachokifanya IGP na wenzake ni kazi bure. Lengo ni zuri lakini method wanayotumia ina makosa. Waanze kuwafundisha kwanza maofisa wao swala la utii wa sheria bila shuruti, ulinzi shirikishi na polisi jamii kabla ya wananchi.

Huyu Zuberi anatakiwa aondolewe kabisa kwenye jeshi la polisi kwa kuwa amepoteza sifa. Niupuuzi kabisa kwa kamanda wa polisi ambaye anadhamana ya kulinda wananchi ndani ya jiji kusema "anahofu" kwamba kuna "raia" anataka kumteka mwanae wakati anaishi kwenye nyumba yenye ulinzi muda wote. Polisi akishakuwa mwoga hafai tena.
 
Heshima kwako Chogo Matata.

Mkuu kuna watu wako tayari kutetea ujinga mradi ujinga huo uwe umefanywa na mtu wanayedhani ni shujaa wao.
Nimeongea mara nyingi bahati mbaya sijui sieleweki au lugha niitumiayo imejaa ukakasi.Nilisema na nitaendelea kusema bila kujali nitaeleweka vipi Godbless Lema ni mbunge wa Arusha mjini.Kachaguliwa kwa kura nyingi au kwa maneno rahisi kura zake zilitosha kabisa lakini Mheshimiwa Lema badala ya kuwatumikia wapiga kura wake amelifanya jimbo la Arusha mjini eneo la harakati kwa kuwatumia vijana wasiokuwa na ajira katika harakati zake.

Mheshimiwa Godbless Lema kashtakiwa mahakama kuu mjini Arusha badala ya kupamabana na kesi amekuwa akihamasisha vijana wa vijiweni wasiokuwa na ajira na wanye ajira zisizo rasmi kumsindikiza mahakamani.Eneo la mahakama kuu mjini Arusha ni dogo sana kuhimili wingi wa washabiki wake.Nia na madhumuni ya Mheshimiwa Lema ni kutumia kesi ya kupinga ubunge wake kama sehemu ya kampeni kwakuwa anajua mwisho wa kesi ni nini.Niseme bila kutafuna maneno Mheshimiwa Lema kafanikiwa sana kuwavuta wasiokuwa na akili na wasiojua kwamba kuwepo kwao mahakamani hakutasaidia lolote kama wakili wa Lema atashindwa kumwakilisha mteja wake vyema.Ukodishaji wa pikipiki zilizotundikwa bendera za chama maana yake nini au ni sehemu ya utetezi wa Mheshimiwa Lema ?.Ukusanyaji wa vijana wahuni ambao mara zote wanasababisha msongamano usio wa lazima kila kesi inapohairishwa maana yake nini ?.Mabishano ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote kila kesi inapotajwa inamlazimu Lema kutoa ufafanuzi wa kisheria kwa wapambe wake,Tangu lini Lema kasoma sheria,Je huku si kuingilia uhuru wa mahakama ?.Nilisema kabla mkusanyiko ni mkubwa Lema na wapambe wake wanajua hilo lakini kwa maksudi ya wazi wanaamua kuyaacha magari yao wanaamua kutembea kwa miguu umbali wa zaidi ya kilometa tatu/nne wakisindikizwa kwa nyimbo za kejeli kwa mlalamikaji na pikipiki je hii ni sawa.

Hivi mtu akiamua kutembea kwa kutumia miguu yake atakuwa amevunja sheria?Nnaona ulichoandika ni Kama unataka kuingilia uhuru na haki ya mtu.Wapotoshaji tunawajua,tunawapuuzia na tutazidi kuwapuuzia.
 
Mkuu FS.

Hivi kweli unaweza kumweka Lema kundi moja na Nelson Mandela,Luther King na Nuhru Gandhi duh kweli Tanzania tumefikia pabaya.


Nuhru Gandhi, Nelson Mandela, Luther King all went through the same harasment, but they have brough changes in the world. Lema dont gi it up. yoa are a real politician, one day the history will tell.
 
Hivi mtu akiamua kutembea kwa kutumia miguu yake atakuwa amevunja sheria?Nnaona ulichoandika ni Kama unataka kuingilia uhuru na haki ya mtu.Wapotoshaji tunawajua,tunawapuuzia na tutazidi kuwapuuzia.
Achana na Ngongo huyo!!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom