Taarifa kwa umma toka kwa Lema (MB), apinga jeshi la polisi kutumiwa kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa umma toka kwa Lema (MB), apinga jeshi la polisi kutumiwa kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngurati, Oct 30, 2011.

 1. n

  ngurati JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

  *

  Nawasalimu nyote.

  Nimewaita kutoa taarifa juu ya kilichotokea juzi tarehe 28/10 /2011 baada ya kuhairishwa shauri la kesi ya uchaguzi iliyoko mahakamani dhidi yangu .

  Tarehe 27/10/2011 kesi hii ilihahirishwa na Judge A . Mujuluzi kwani usikilizaji wake usingewezekana kwa kuangalia idadi ya watu walivyokuwa wamejaa pale mahakamani ,maagizo yalitoka kwamba shauri litakalofuata mahakama iwe imetayarisha vipaza sauti kwa ajili ya usikilizwaji wa kesi hiyo.

  Lakini kwa bahati mbaya jambo hilo halikuwezekana kabisa kwa sababu ambazo baadaye Mh* Judge alizitolea ufafanuzi mzuri na mawakil wa pande zote wakakubaliana kuendelea na shauri hilo bila vipaza sauti lakini kwa ahadi kuwa mpango huo unatekelezwa haraka na wakati mwingine wa kesi itakapokuja mahakami utaratibu huo utakuwa umekamilika.

  Jambo la kushangaza siku hiyo wakati nafika mahakamani nilikuta polisi wengi sana na wamevaa nguo zinazoashiria tayari wako kwa mapambano na watu wakizuiwa kabisa kuingia mahakamani kuanzia geti kubwa na polisi walikuwa wanajaribu kuhoji kila mtu kuwa anakwenda kusikiliza shauri gani na kama mtu angejibu ni shauri la kesi ya uchaguzi basi halikuwa haruhusiwi kuingia mahakamani kuanzia geti la mwanzo wa mahakama.

  Nilikata dhambi hii na uonevu huu kwa wapiga kura wangu nilimfuata OCD Bwana Zuberi Mwombeji kuongea naye juu ya jambo hili la kuzuia watu* na alikataa kabisa na kusema* “ hao watu wanaenda wapi kwani kesi inawahusu ? na yeyote atakaye vuka* hawa polisi hapa hatakuwa chambo na kuniambia kuwa hata watu wakija maelfu na maelfu mahakamani* lazima kesi hii initie kidole “ ( Zuberi) , tulibishana huku* nikijaribu kutetea utu wangu na mamlaka yangu kama Mbunge* , ikawa zogo mahakamani muda *mrefu bila mafanikio *mpaka nilipomuomba wakili wangu aingilie kati kisheria ndipo watu waliporuhusiwa kwenda kusikiliza kesi .

  Baadaye baada ya kesi* nilikuta wananchi waliokuwa nje ya chumba cha mahakama *wakiwa na hasira huku wakilalamika na kwani kwa mara nyingine tena OCD Zuberi alikuwa amewaita tena wananchi PANYA na akiamuru polisi wa ngazi ya chini* kwa kusema “sogezeni hao *PANYA nyuma”

  Lugha hii ni mbaya* haikubaliki hata kidogo, niliongea na wanachi na na kukemea lugha hii kwa hasira *baadaye nilielekea ofisini kwangu kwa miguu huku nikisindikizwa na polisi na watu wengi waliokuwa mahakamani *na baadhi *ya watu niliomba tukutane nao ofisini kwangu wengi wakiwa ni viongozi wa matawi na vijana naotarajia kuwa mashaidi katika kesi ya uchaguzi *, niliongea nao ofisini kwangu nikawaaga* nikaondoka* na wachache niliwaacha ofisini kwangu na Katibu wangu na baadhi ya wageni wengine, baada ya muda nilipigiwa simu kuwa polisi wameingia ofisini kwangu na kukamata watu wote , nilimpigia simu Kaimu RPC kumueleza suala hili na* yeye alisema ni bora nifike ofisini kwake tuongee jambo hili , nilipofika nilimueleza jinsi OCD anavyoendelea kufanya kazi kibabe, kwa shuruti za siasa na bila busara na kuhumiza watu bila sababu , alinisikiliza kwa muda usiopungua saa nzima na baadae nikifikiri nimeeleweka* ghafla niliwekwa chini ya ulizi na kuambiwa nitoe maelezo na kushitakiwa kwa kosa la kuongea watu nje kabisa ya viwanja* vya Mahakamani na ofisini kwangu .

  Ninafahamu mipango yote ya siri na wazi iliyokusudiwa kwangu na wafuasi wangu , ndio maana sishangai kwamba vyama vingine vinaweza kufanya mikutano na maandamano bila kibali na kuchungwa na polisi na yeye OCD* na polisi walipohojiwa na waandishi wa habari juu ya jambo hilo UVCCM kufanya mkutano na maandamano bila kibali,, Polisi walisema wanataarifa na wametoa onyo kwa viongozi waliohusika.

  Lakini mimi *Mbunge nimekatazwa hata kutembea kwa miguu kutoka mahakamani na ni *lazima nipande gari hata kama nataka kutembea kwa miguu na hata kuongea na Wananchi mahakamani na ofisi kwangu ni kufanya mkutano bila kibali ? Jambo hili limenisikitisha sana lakini moyo wangu huko imara kwani naamini kila matatizo yanayotokana na kupigani haki au usawa* matatizo hayo mara nyingi huwa ni mpango wa Mungu juu ya kusudi Fulani.

  Kesi *ya uchaguzi bado inaendelea, nilichaguliwa kwa kupata kura zaidi ya elfu 56. Wakija takribani asilimia kumi tu ya walionichagua ni watu zaidi ya 5,600. Watu hawa wakija kusikiliza kesi na baada ya kesi* wakaamua kuondoka kwa kuelekea mjini na sehemu mbali mbali* , je kundi hili la watu wataondokaje mahakamani ili msongamano huu usiitwe maandamano ? Hatuhitaji nguvu kubwa ya jeshi la polisi kutawanya watu wanaotoka mahakamani tunahitaji ulinzi wao na busara zao ili watu wasambae kwa amani *“ kwani kusudi la mkusanyiko huu hautokani na nia mbaya bali ni kesi ya uchaguzi ambayo hauwezi kushanga kwanini kuna watu wengi mahakamani.

  Matukio mengi ya uhalifu Tanzania huwa yatokei kukiwepo na msongamano *wa watu tu bali yanatokea tu pale penye dhamira ya uovu bila hata msongamano , mara nyingi tunasikia taarifa za mabenki kuibiwa , watu kuvamiwa katika nyumba zao usiku na kuchomwa visu na kuporwa mali zao mambo haya huwa yanafanyika tena msongamano wa watu ukiwa usingizini, sio kweli kuwa kila msongamano wa watu ni maandamano au ishara ya vita na uovu ndio maana sokoni na sehemu za ibada huwa hakuna polisi wanaolinda kuepusha msongamano kwani kusudi la msongamano huo unajulikana maudhui yake. Haitoshi kutembea kwa miguu idadi kubwa ya watu kuita maandamano. *Maandamo yanatafsiri pana sana.

  Hakuna shaka ni siasa ambayo iko wazi juu ya kilichotokea* tahere 28/10/2011* kwani sio mara ya kwanza kutoka mahakamani kwa miguu na kuja ofisi kwangu *kwani tarehe 21/10/2011 tulitoka mahakamani kuelekea Ngarenaro kwa miguu tena kupitia* njia ya polisi , mbona siku hiyo kutembea huko hakuitwa maandamano ? ama kwa vile OCD hakuwepo ? *.

  Ninatoa wito kwa serikali na viongozi wa jeshi la polisi sio afya hata kidogo mwakilishi wa wananchi *kama mimi kuwa na uhusiano mbaya na Jeshi la polisi *kwa sababu ya mtu mmoja.

  Ndugu wananchi na wanahabari Wakati Fulani huko Nyuma *OCD *alituma kwa katibu wetu wa Mkoa Meseji kuwa mimi Mbunge nimeandaa mpango wa kumteka mtoto wa OCD *na kumuua , Mimi pamoja na Mkiti wetu wa Taifa Mh Mbowe *tulienda kumuona RPC* na viongozi wengine kujadili na RPC alihaidi na kuona umuhimu wa kukaa pamoja na kujaribu kutafuta uhusiano mwema na suluhu jambo ambalo halikuwezekana mpaka leo kwa sababu pengine za msingi.

  Sasa najiuliza nikiwa nimevamiwa usiku au nahitaji polisi kwa msaada wowote ule , je nitakuwa na ujasiri gani wakumuita OCD kwa msaada , kwangu mimi hofu niliyonayo dhidi yake kama kiongozi wa polisi ni kubwa kuliko kukutana na majambazi usiku* , hata hivyo” LETS GO, LETS GOD”

  *Lakini kutafakari kwangu historia mara kwa mara* inatia moyo kwamba hakuna harakati ambazo hazikuitwa ukorofi ,uvunjaji wa sheria , uhaini, na ukiukwaji wa taratibu , niweke wazi *kwamba nitapinga ukandamizaji wowote ule mbele ya yoyote Yule mwenye silaha yoyote ile na mwenye magereza yenye mateso makali* kuliko jehanamu bila woga , na sheria yeyote inayokiuka misingi ya *

  Kwa kweli nimejiandaa hata kupokea mauti* japo najua Mungu anapenda niishi muda mrefu ili kutimiza kusudi lake ,* sitarudi nyuma *katika harakati hizi* za kupinga uonevu , dhuluma na ukandamizaji wa haki za binadamu nasubiri kwa hamu sana kuona mikakati yote iliyopangwa kinyume nami na wafuasi wote wanaopinga uonevu. Hata hivyo Nimeiandaa* familia yangu *kuwa tiyari wakati wowote kwa jambo lolote na kwa taarifa yoyote dhidi ya ukweli tunaoupigania.

  Ndugu wanahabari **kila mara huwa nawaambia wananchi kuwa dhambi mbaya kuliko zote Duniani ni UOGA. Lazima watambue kuwa *wengine watateswa ,wengine watauwawa lakini wengine watafurahia haki na uhuru kamili tunaoupigania* hata kama hatutakuwepo kwa sababu tu wengine walipitia mateso mbali mbali. Mimi natambua kuwa faida ya kuishi* sio kuishi vizuri tu wewe na familia yako bali ni wewe kuwa sehemu ya mabadilikio ya watu wanaokuzunguka , katika kupigani UTU , HAKI ,* ustawi mzuri wa Jamii. Na kila mtu anayemuogopa Mwenyezi* Mungu ataishi kufanya hivyo kama* Mahatma Gadhi alivyopata kusema* “The best way to find yourself is to loose yourself in the service of others”*

  Godbless Jonathan Lema (MB)

  30/10/2011

  *
   
 2. n

  ngurati JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 221
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  On the other side, Nassari katoa onyo kwa mkuu mpya wa mkoa wa arusha, kamwambia aje arusha kwa step. Kama alizoea bagamoyo kuna bahari, arusha kuna milima. Inasemekana mkuu huyu wa mkoa alikwenda Meru akasema bendera za Chadema zishushwe hataki kuziona.
  Lema kamuonya Aache kutumika kisiasa, otherwise arusha itamshinda mapema sana.
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sitashangaa siku moja kusikia OCD Zuberi amempiga risasi mh. Lema. Kama amefikia hatua ya kumpakazia kwamba anataka kumteka mwanae, huyo zuberi anaweza kufanya lolote baya dhidi ya Lema ama wananchi wa Arusha ili afikie malengo yake binafsi.

  Kwa namna nchi hii vyeo vinatolewa kiholela holela, tusubiri kusikia zuberi kapandishwa cheo na ndicho anatafuta kwa nguvu zake zote.

  Lakini asisahau kwamba malipo yote ni hapa hapa duniani, atalipwa haki yake siku moja.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Aseee!!
  Very touching, sijui polisi wanapata wapi jeuri namna hii...wanajitoa fahamu kama vile wao sio binadamu.
  Itafika wakati magari wanayotumia hawa viongozi yatachukuliwa na watalazimika kutembea kwa miguu kama wapiga kura.

  that day will come, soon or later.
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Makamanda wa Arusha nawaaminia. Magesa mulongo ni kibaraka wa magamba na inasemekana alihusika kwenye tamko la uvccm mkoa wa pwani kujinasibu kwamba raisi ajaye hatatoka kaskazini. Bila shaka kaletwa huko kwa kazi maalum.
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Pamoja sana Kamanda!

  IGP anasubiri nini kumwondoa OCD asiyeutambua hata heshima na utu wa wanadamu? Afukuzwe haraka sana, kitendo cha kuwaita wanadamu wenzake PANYA is absolutely unacceptable behavior!

  Mwombeji lazima atambue kuwa asingekuwa OCD bila watu. Mwombeji lazima atambue kuwa Lema alichaguliwa na wananchi, siyo kama yeye aliyeteuliwa na mtu moja tu kwa utashi wake!

  Mungu yupo, hizi dhuluma zina mwisho!
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo huwa narudi kwenye hoja yangu kwamba polisi wetu wengi ni failures shuleni, sasa watawezaje kutekeleza shughuli zao kwa mujibu wa sheria na kanuni wakati wanajiona kama wao kuwepo polisi ni favour? Ndipo wanaishia kufanya mambo mengine ambayo ni ya kipumbavu kabisa.
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Stand Strong Brother haya yatapita tu, sijui watazificha wapi nyuso zao muda ukifika.

  Pole Mheshimiwa Mbunge
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama kuna sehemu mbaya ya kufanyia ubabe basi Arusha inaongoza. Huyo Zuberi aachane kabisa na hizi hila uchwara- atashindwa vibaya. Bosi wake Said Mwema anazunguka nchini akihimiza ulinzi shirikishi lakini yeye Zuberi analeta umafia wa 1947!

  Report ya corruption mwaka huu inaonesha polisi iko juu kwa rushwa, kama wananchi wataendelea kupoteza imani na chombo hiki basi ujue nchi inaelekea kubaya. Na mambo yanavyoenda inaelekea tuko direction hiyo.
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tuko pamoja makamanda....
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  zuberi hawezi kujua hilo analolifanya kwa sasa, kuwaita wananchi panya ni kuonyesha kiwango cha chini sana cha weledi na busara.

  Lakini mimi sishangai hii ni kawaida yao. Massawe ambaye ni RPC Tanga alikuwa hivi hivi akiwa ocd tarime, wakati wananchi wakitarajia afukuzwe kazi wakashangaa akipandishwa cheo na kuteuliwa kuwa RPC.

  HAYA NDIO MAAJABU YA SERIKALI YA CCM.
   
 12. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  If steps are not in advance and so quickly Arusha will soon devop into a battle ground!!In the past (I dont know ) Arusha wa used to be called Geneve of Africa!! But may be if measures are not taken it will be soon cossovo of Africa,..

  Jamani hebu kila mtu atimize wjibu wake kwa mujibu wa sheria ., polisi weka usalama , mbunge himiza maendeleo na wananchi tufanye kazi kwa bidiii!

  I LOVE ARUSHA I DONT WANT TO SEE IT BEEN RUINED!
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kitendo cha polisi mwenye wajibu wa kulinda raia na mali zake kuwaita raia hao 'Panya' hakikubaliki hata kidogo. Kwangu mungu inaonesha ni jinsi gani polisi wanawaona wananchi wa kawaida - sio watu, ni panya! Na ndio maana hata pale polisi inapouwa raia wasio na hatia hakuna kinachofanyika - panya kafa!

  Kwa kuunganisha, judge mkuu wetu (Othman) anatakakazi ya Occampo. Nadhani watanzania tunayo haki ya kufanya campaign asipate hiki cheo. ICC pamoja na mapungufu yake lakini bado ni kimbilio kwa nchi zenye viongozi wanaita raia 'Panya' kama hawa wa Tanzania.

  Kama polisi wataendelea kuuwa raia (na watandelea) jee huyu Othman akiwa huko ICC atanyanyua mguu? Amefanya nini kuhakikisha raia wa watanzania wanapata haki wakati akiwa judge mkuu? Naona hiki cheo anapigiwa upatu ili akishapata ndio sisi panya tusipate mahali pa kukumbilia.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kitu ambacho sijafahamu ni kama Arusha nako kuna hii kitu ya ulinzi shirikishi na polisi jamii.

  Kama hizo shughuli zipo, ni nani anayezihamasisha na kuzi-cordinate kama ocd anawaita wananchi panya?
   
 15. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kiukweli huyu Zuberi anachokifanya sicho, kwanza kuudhalilisha utu Wa mwanadamu kwa kuwaita PANYA. Ghadafi aliwaita wananchi wake mende na panya je sasa hivi yupo wapi?.

  Pili huyo Zuberi anavunja sheria za Jamhuri ya Muungano Tanzania kwa kuwazuia wananchi kuingia mahakamani kwa nia ya kusikiliza kesi. Tatu huyu Mbunge Lema tumemchagua sisi Wananchi Wa Mkoa huu wa Arusha, kumdharau yeye ni sawa na kutudharau wananchi.

  Afande Zuberi jihadhari sana kutumika (kama kond..m)sababu unazidi kujenga chuki kati ya Wananchi na jeshi la polisi. Tafadhali kamanda kumbuka wahenga walinena"Mtu hupamba kaburi lake mwenyewe"Soma alama za nyakati sababu sisi wananchi unaotuvua utu wetu na kutuita panya ipo siku utatujua Kama ni panya kweli au la!!!?

  Pls fanya kazi yako ya jeshi la polisi Kama inavyotakiwa, epuka kutumika vibaya hatupendezwi na utendaji wako ktk kututumikia sisi waajiri wako.
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  hata gadaffi aliwaita raia wake panya, lakini yeye ndiye aliyegeua panya kwa kujifichi kwenye makalavati kama panya wafanyavo, mungu mkubwa!!

  Aangalie asigeuke panya akajichimbia kwenye mashimo mambo yakianza
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  aisee, inasikitisha kwakweli, looh! hiyo jeuri ya huyu bwana zuberi ina mwisho mbaya sana kwake,
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tumia akili yako vizuri na usome taarifa ya mbunge kwa umakini.

  Wapi mh. Mbunge kasema anataka kwenda paradiso? Na hata hivyo huna uwezo wa kumhukumu kwani wewe si Mungu.

  Lini umesikia wananchi wa Arusha wanaomba msaada wa chakula? Maandamano wanafanya, mahakamani wanakwenda, kazi wanafanya na familia zao wanazitunza vizuri.
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wataalamu wa sheria naomba mnisaidie. Hakuna uwezekano wa huyo ocd zuberi kufunguliwa mashitaka mahakamani kwa kuwatukana na kuwadhalilisha wananchi?

  Mara nyingi nimekuwa nikishuhudia raia wengine wakishtakiwa kwa makosa kama hayo, je polisi wao wana kinga katika hili?
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,606
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Kwani Arusha kuna idadi kubwa ya polisi kuzidi raia? Kama siyo basi watu wachukue hatua ya kuwafanyizia kweli popote wanapoonekana mpaka washike adabu
   
Loading...