T.I D agombewa na wafungwa

Mbeba Maono

Senior Member
Jun 24, 2008
108
7
Oh! poor TID jamani, ndo atakaa ndani mwaka mzima. sijui watakuwa wameshamnyoa nywele tayari? hivi huyu jamaa mbona kosa lake hili angekuwa makini asingefungwa? nina maana kama ange hire a lawyer kumuwakilisha, mbona asingefungwa? sijui atakuwa amekata rufaa tayari, au atakuwa anajua limitations za kukata rufaa? manake kwa kosa lake naona kama mwisho wa kukata rufaa ni siku saba, akizidi hapo ndo hataruhusiwa. hebu jameni, msiwe mnajiamini sana, kama una kosa, jifanye mjinga, mchukue mwanasheria, mpe fee yake na atakufanyia mambo yako. kwenda na msululu wa magari kule mahakamani ukijifanya wewe ni mwana mziki au mtu yeyote maarufu, hakumshitui kabisa hakimu au jaji, na siajabu ukajikuta umeongeza matatizo na ukawa tagetedi zaidi kwasababu ya hilo. ni shilingi ngapi angemchukua wakili pale jamani, hata milioni isingezidi, lakini kukaa mwaka mmoja jela, kule kwenye chawa na kunakonuka mikojo, hakuna girlfriend wako kwahiyo unaweza ukajikuwa wenzio wanakulegeza kiaina, ukitoka nje watu wanakuona kama sio yule wa zamani, manake unenguaji wako wa kiuno unakuwa umebadilika.

sasa mnaona, mtu anaenda kufyeka majani ya ng'ombe wa askari wa gereza na kupiga pushap na shuruba kibao mle ndani. I tell you, jela mwezi mmoja ni sawa na miaka ishirini, je mwaka mmoja je? kusema ukweli namwonea huruma. angekuwa labda ni mwana mazoezi na mpigana karate na kong fu kama mimi ningesema sawa, lakini siku ile anaingia kwenye gari wenzie walimwambia ni mtoto wa mama wakamkaribisha sana. jifunzeni kuwatumia wanasheria. mahakama sio kama watu wanavyoliona jengo kwa nje. waulizeni waliowahi kushitakiwa.
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,156
Kuna gazeti leo limeripoti kuwa ni mgonjwa huko jela. Pole sana TID. Lakini anapaswa kujua kuwa ustar wake haumfanyi awa mwanadamu bora kuliko wengine
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,925
10,426
Tena kijana amebadilika sana amelewa sifa ambazo zimemfanya we mjinga....mnajua kuwa hivi karibuni alikuwa anakwapua simu kwenye meza ambapo huwa na washirika na watu wengine wanakunywa.....na anajisifia kuwa "nimepiga kazi kubwa sana leo"niliposikia kuwa amekuwa hivyo nikajuaa huo ni mwisho wake maana sasa hana flow ya pesa kama alivyozoeaa...umebakia umaarufu...na anakula unga sijui itakuwaje hukoo.....ok ndio maisha leoo juu kesho chini....ajikakamue tuu atamaliza....Nasikia kampiga "mtoto familia bora"......
 
Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,745
7,757

...wallahi sasa nimeamini walosema 'hujafa hujaumbika'

Kuna mtu aliwahi kunambia "shukuru mungu kama utamaliza maisha yako yote hujafungwa japo kwa usiku mmoja selo ya aina yeyote!", kwani Jela imeumbiwa binadamu kama mimi na wewe! wala si suala la kumbeza mwenzako akiwekwa Lupango, huenda lako linakuja kwa namna wala usokuwa unaitegemea. Mw'mungu atuepushie hilo, wala sio sifa kujinadi, '...nilisha wahi fungwa mie!'

'Jela, Jela ni mbaya, jela jela ni mateso!' -FM Academia,wana jelajela.
 
Mzozo wa Mizozo

JF-Expert Member
May 26, 2008
426
9
Aah,

Kwa nyepesi nyepesi ni kwamba Dogo yupo poa na mpaka jana alikuwa hajanyolewa nywele zake na he is coping with his new environment.

Kilichomfunga si kupiga mtoto wa familia bora wala nini, ni dharau za xhali ya juu...na hasira zaidi ya Mheshimiwa aliemfunga ilikuwa ni pale kijana alipoonekana kwamba kadharau mahakama. I navyosemekana kapewa barua kuitwa mahakamani mara nyingi lakini hakuona umuhimu wa kwenda pale.

Ni sheria tu imefuata mkondo.
 
okon

JF-Expert Member
Mar 16, 2008
305
91
Acheni wafungwa nao waimbiwe zeze na nyota yangu, kila siku muimbiwe nyie tu huku uraiani, ooh!
 
Last edited:

Mpiganaji

Member
Oct 10, 2007
15
0
Aah,

Ni sheria tu imefuata mkondo.

Pamoja na sheria kufata mkondo wake, inasemekana aliyepgwa ni ni mtoto wa mkuu wa msafara wa mkuu wa nchi. na yule hakimu alivuta mkwanja toka kwa TIJ na baada upande wa pili kujua wakaende kumsemea mbovu hakima kwamba wameshajua kavuta, hakimu kaogopa ndio siku ya siku hukumu ikatolewa bila hata option ya kulipa fine, maana kwa kesi hizo kifungo huja baada ya kushindwa kulpa fine. mdingi alidhamiria kabisa kijana aende ndani.
 
omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
139
Nasikia kampiga "mtoto familia bora"......

Si afadhli ingekuwa ni hilo la familia bora tu.....tatizo vijana tukikutana viwanja tunadhani wote tuna ajira za ujanjaujanja tu....TID alipiga kubaya na mbaya zaidi alipopewa nafasi ya kujirudi akaendelea na upuuzi wake.....

Tanzanianjema
 
Kibunango

JF-Expert Member
Aug 29, 2006
7,984
1,589
Si afadhli ingekuwa ni hilo la familia bora tu.....tatizo vijana tukikutana viwanja tunadhani wote tuna ajira za ujanjaujanja tu....TID alipiga kubaya na mbaya zaidi alipopewa nafasi ya kujirudi akaendelea na upuuzi wake.....

Tanzanianjema
Ni vizuri sheria inapochukua mkondo wake, huu ni mwanzo mzuri kwa Tz ambayo inataka kufuta sheria na sio kupindisha mambo.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,744
3,796
Kunyolewa lazima ni suala la muda tu.atakuwa balozi mzuri kwa wasanii mara atakapotoka huko. Haipendezi kwenda huko,wala usiombee jirani yako akaenda ila inapobidi ni muhimu.Kuna watu wanaishi kama utaratibu wa maisha haupo.
 
Wakunyuti

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
380
12
Pamoja na sheria kufata mkondo wake, inasemekana aliyepgwa ni ni mtoto wa mkuu wa msafara wa mkuu wa nchi. na yule hakimu alivuta mkwanja toka kwa TIJ na baada upande wa pili kujua wakaende kumsemea mbovu hakima kwamba wameshajua kavuta, hakimu kaogopa ndio siku ya siku hukumu ikatolewa bila hata option ya kulipa fine, maana kwa kesi hizo kifungo huja baada ya kushindwa kulpa fine. mdingi alidhamiria kabisa kijana aende ndani.

Duh jamaa sasa ivi anaitwa TIJ= Top in JAil? hahah....kweli wabongo hamna maana.... namuonea huruma sana dogo..lakini at the same time nafikiri wasanii wengi watakua wamepata somo kubwa kwa hili.. na yale mambo ya ubabe ya Kikosi cha mizinga sijui na nako 2 Nakos yatapungua...maana jela hamna anayependa kwa kweli
 
Paullih

Member
May 12, 2008
85
13
Mnh mwanzoni nilidhani hili linazungumzika na ile kesi nikajua itakwisha nje ya mahakama. Wazazi wa upande wa TID wangejitolea kuwataka radhi wazazi wenzao nadhani mambo yangeisha haya! Mwakumbuka Dudubaya alimpiga Mr. Nice hadharani pale Diamond na kesi ikaenda mahakamani lakini ikaisha kiaina? May be na family ilijengeka kiburi kwa fedha inazodaiwa walimpa muheshimiwa, kama hii ni kweli.

lakini pia ni funzo kwa wandugu wanaopenda kujichukulia sheria mikononi. Akaze buti atamaliza tu mwaka mmoja.... Ishu ni wale akina Papii waliofungwa maisha.
 
Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,576
1,090
Aah,

Ni sheria tu imefuata mkondo.

Pamoja na sheria kufata mkondo wake, inasemekana aliyepgwa ni ni mtoto wa mkuu wa msafara wa mkuu wa nchi. na yule hakimu alivuta mkwanja toka kwa TIJ na baada upande wa pili kujua wakaende kumsemea mbovu hakima kwamba wameshajua kavuta, hakimu kaogopa ndio siku ya siku hukumu ikatolewa bila hata option ya kulipa fine, maana kwa kesi hizo kifungo huja baada ya kushindwa kulpa fine. mdingi alidhamiria kabisa kijana aende ndani.

Basi kama ni hivi hapa sheria haikufuata mkondo wake bali ni UFISADI na abuse of power ya watawala wetu. Hii vita ni ngumu jamani
 
Mzozo wa Mizozo

JF-Expert Member
May 26, 2008
426
9
Hebu naomba niambiwe kijana wetu nguo za Orange tayari anavaa, nywele je? nadhani itakuwa poa sana akirudi huku kama atakuwa mpyaaaaaaaa!
 
Mzozo wa Mizozo

JF-Expert Member
May 26, 2008
426
9
Originally Posted by Mpiganaji
Pamoja na sheria kufata mkondo wake, inasemekana aliyepgwa ni ni mtoto wa mkuu wa msafara wa mkuu wa nchi. na yule hakimu alivuta mkwanja toka kwa TIJ na baada upande wa pili kujua wakaende kumsemea mbovu hakima kwamba wameshajua kavuta, hakimu kaogopa ndio siku ya siku hukumu ikatolewa bila hata option ya kulipa fine, maana kwa kesi hizo kifungo huja baada ya kushindwa kulpa fine. mdingi alidhamiria kabisa kijana aende ndani.

Basi kama ni hivi hapa sheria haikufuata mkondo wake bali ni UFISADI na abuse of power ya watawala wetu. Hii vita ni ngumu jamani

nAYE KIJANA WETU ALIONYESHA DHARAU KWA MAHAKAMA BAADA YA KUTOKUONEKANA MAHAKAMANI MARA KWA MARA KESI YAKE ILIPOKUWA INATAJWA.

Sidhani kama kutokuonekana Mahakamani kwa Mshitakiwa kunashabihiana na Ufisadi na Abuse of Power
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom