Syria watungua ndege ya Israel

Syria watungua ndege ya Israel

Role Multirole fighter, air superiority fighter
National origin United States
Manufacturer General Dynamics
Lockheed Martin
First flight 20 January 1974
Introduction 17 August 1978
Status In service
Primary users United States Air Force
25 other users (see operators page)
Produced 1973–2017, 2019–[1]
Number built 4,573 (July 2016)[2]
Unit cost
F-16A/B: US$14.6 million(1998)[3]
F-16C/D: US$18.8 million(1998)[3]
Variants General Dynamics F-16 VISTA
Developed into Vought Model 1600
General Dynamics F-16XL
Mitsubishi F-2
Mkuu hii kitu kumbe ni pesa nyingi sana na ina mbwembwe nyingi sana dah kwaiyo zikidunguliwa mbili tu ni cash ya maana !!! kweli kila kitu na zama zake hii kitu ilitamba sana Iraq !!!!!
nadhani sasa itakiwa inarushwa kwa kuvizia maana mlenga shabaha kuwa akiweza mara moja lazima aweze mara ya pili na ya tatu
View attachment 693622
single seat dah lazima wakune kichwa leo !!!
ila ujuwe sisi wa Africa tupo na mungu wao wapo na technology lazima wale wa Africa wanaotaka kufukuzwa huko Israel dua zao zimeanza kufanya kazi au !
Mkuu hizo 4th generation fighter jets zishapitwa na wakati,sasa hivi kila nchi kubwa inahamia kwenye 5th generation ambazo ni stealth,zinaweza kusupercruise bila kutumia afterburner (kwa sasa yenye uwezo huu ni F22 tu ya Mmarekani),zinakua na mfumo wa hali ya juu wa jamming,nk.

Mfano wa 5th generation kwa sasa ambazo zipo kazini
1.F22 Raptor imeanza tangu 2005 (USA)
2.F35A Joint strike imeanza 2017 (USA)
3. J20 imeanza mwaka 2018 (China)

Ambazo zipo kwenye majaribio ni Su-57 ya Mrusi inatarajiwa kuanza kazi 2019/20.
Pia F35B bado ipo kwenye majaribio.

Nchi zenye project zao wenyewe za hizo 5th gen ni pamoja na Japan,South Korea, Turkey,India(wakishirikiana na Russia),nk.
 
Silaha hizi zote hatutashuhudia kamwe zikitumika kikamilifu ktk vita kati ya Taifa na Taifa. Ibilisi shetani anawatengenezesha wanadamu Silaha hizi kwa maandalizi ya ile vita kubwa mno ya Armageddon (Soma Biblia Kitabu cha Ufunuo wa Yohana). Je, tufanye nini? OKOKA!
Okoka kw kujitangaza au kijiita uendeelee na matendo mabaya .
 
@zekokuyo
hii ishu mimi nimeiona bado niko kwa bed saa 6:30 asubuhi,
mimi mzito wa kuanzisha thread ila napenda kuchangia tu,sasa nikawa nasubiri watu wailete kimya,
imefika karibu saa tano bado kimya,nikakumbuka leo wikiend nikajua bado mmelala ndo nikajisa kuipost.
Naona IDF spox amesema yaishe,wasikuze hii ishu,
labda wamegundua mrusi anawazunguka watatafuta utaratibu mwingine,kwa mfano labda kummaliza assad au putin,au wanasubiri watu wajisahau ili washitukize kupiga kama kawaida yao.
Au wamegundua actually wao waliovereact,ilitosha wao walipoidodosha drone,kwani drone hata zao huingia syria zikadodonshwa mambo yakaisha.
Pengine wamegundua syria alikuwa na haki ya kufanya defence dhidi ya shambulizi etc.
Najaribu kutafuta madhara yaliyoletwa na shambulizi la pili la israel syria bado taarifa hazipatikani,
zipo za juu juu mfano pale T-4 airbase inasemekana israel wameharibu observation tower na baadhi ya drone za hezbullah.

Wiki chache zilizopita iran walitoa drone 100 kwa hezbollah huko syria.
Hizo ni zenye uwezo wa kushambulia na inawezekana drone ya leo ilikuwa inakwenda kushambulia waasi wa syria walio katika mpaka wa syria na israel
Nenda Reuters,Haarez,New York Times,Sputnik utakuta taarifa za hilo shambulizi la pili.
 
Msome ze kokuyo hapo juu wacha kujitoa ufahamu. Ma-air defence systems ma4 yashageuzwa vumbi acha unazi wa kijinga huku mnateketea kama kuku wa nyama machinjioni.
wapi dogo hajarudi tena alituma missile nne nazo zimemalizwa kabla ya kufika kwenye target. Israel kwa kuogopa mpaa anamuoba mrusi aingilie. Mwambie arudie tena kama kamaliza air defence kweli.
 
Usicheke mkuu hao marekani na korea unasikia sijui fulani kasema na mwenzake akajibu vile.
Kama wake wenza

Ila syria na Israel hakuna maneno hawa ni wanaume wa shoka
Marekani na Korea waswahili sana mkuu waache waendelee kupeana mipasho! Ila hawa Israel na Syria kama wakurya hawachelewi kuzichapa
 
Nadhani Nchi Kama Israel Kuisambaratisha Syria itatumia Mda wa Masaa Matano 5 hrs, Sawa Na Asilimia 30%, Ya Mda ilioutumia Mwaka 1967 Kuzisambaratisha Nchi za Jumuia ya Kiarabu Zilizoungana Pamoja Kuwapiga Mafundi Hao Wa Technology DUNIANI na Kupelekea Kulifanya Taifa la Palestina Kuwa Watu wasio na Makao Maalumu, Watumwa na Wakimbizi Mpaka Hivi Leo,
Nadhani Kitakachoifanya Israel isifanye yale iliyoyafanya 1967 Ni Jumuia ya Umoja wa maTaifa na Dunia Kiujumla Itasema Nini, Ukizingatia Mzozo wa Mashariki Ya Kati bado Haujapatiwa Ufumbuzi.
Unadhani Marekeni KuwAkumbatia Hawa Jamaa ni Kwa Sababu gani, Hawa wayahudi walikuwa na Na Nini cha Kumpa Marekeni Mpaka awabebe Kiasi Hiki?
Ikumbukwe pia Israel ndo Nchi Pekee ambayo Raia wake Wote ni Wanajeshi Bila kujali jinsia. Mafunzo ambayo kwa Mwanaume ni Miezi 30 Kambini Huku Wanawake ni 24.
Mrusi nae Ni Namna ya Kumtafuta Marekeni wala siyo Israeli Kama wanavyosema.
hahaha acha kuishi kwa historia Israel walipigana na Hezbollah juzi juzi tu vita imechukua miezi na mpaka wanasuluhishwa hawakushinda Israel hawana kitu Jeshi lao linafadhiliwa na Marekani siku Marekani wakiacha kuwafadhili hata sisi Watz tunawadunda
 
hahaha acha kuishi kwa historia Israel walipigana na Hezbollah juzi juzi tu vita imechukua miezi na mpaka wanasuluhishwa hawakushinda Israel hawana kitu Jeshi lao linafadhiliwa na Marekani siku Marekani wakiacha kuwafadhili hata sisi Watz tunawadunda
Ni Sawa na Leo useme Tanzania Imeshindwa kuwasambaratisha Alshababu Ilihali Hufikirii Tofauti na vita ya Nchi na Nchi ni Kwamba Haya Makundi ya Kigaidi ama Kijasusi Hayana Kambi Malumu wala Makao Maalum, Hivi Unadhani Kweli yangekuwa na Makao na Kambi Maalum ni Vigumu Nchi Kama Nigeria kuwasambaratisha BokoHaramu? Nadhani nimejibu Swali lako, by the way Hebu tucheki Hili Picha Kwa Vile Inshu Kama Hizi za Kushabikia sana coz wanaoumia ni Raia wa Kawaida. Kama Vile Picha la 1978/1979
 
wapi dogo hajarudi tena alituma missile nne nazo zimemalizwa kabla ya kufika kwenye target. Israel kwa kuogopa mpaa anamuoba mrusi aingilie. Mwambie arudie tena kama kamaliza air defence kweli.
Kwakweli naamini israel hatopeleka pua baada ya netanyau kusema kuwa iran na syria wanachezea moto,,,iran kasema hizo ni kauli za kipuuzi .
 
UPDATES:

Mpaka sasa Israeli imeshambulia air defenses tatu pamoja na maeneo mengine 9 yanayosadikiwa ni kwa ajili ya shughuli za kijeshi za Iran.

Syria wakajibu kwa kurusha makombora ya ulinzi karibia 24
6c985fb331b9d085f941f28bf04273d7.jpg


Russia imesema kwamba inataka pande zote kutulia huku ikisisitiza Uhuru wa Syria lazima uheshimiwe

Marekani imepongeza msimamo wa Israeli dhidi ya Iran na makundi yake ambayo inayaunga mkono.

Wakurdi nao watungua helicopter ya Uturuki na Erdogan amesema yeyote atakaehusika atalipa gharama kubwa

PS: Kwa taarifa za sasa zinasema kwamba asubuh Syria walirusha makombora 10 dhidi ya ndege 2 za Israel Ila moja ilianguka baada ya Rubani kueject (japo haijajulikana alieject kutokana na hayo makombora au nini). Jeshi la Israel limesema kwamba kuna vitu rubani alikosea vilivyofanya kushambuliwa kirahisi kwa ndege yake huku ikionya kwamba Iran na Syria zinacheza na moto

Elungata Bujibuji Root Baazigar dudus fundi25 Nalendwa


Ndo nimeona hii ase, tatizo ni kuwa huyu mu Israel asije kulikuza hili likawa kubwa kuliko..
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Yani ndege ya miaka ya 1970 kudunguliwa mnafanya sherehe!!!![emoji2] Mbona Mturuki aliitumia ndege hiyohiyo kama ya Israel F-16 kuitungua ile ya Mrusi lakini walikaa kimya.

Hii wiki haiishi nakwambia lazima Israel atembeze kichapo kingine huko Syria.


Hahaha!, no wonder ulikuwa unasubiriwa kwa hamu hapa mahala. [emoji1]
 
Kwakweli naamini israel hatopeleka pua baada ya netanyau kusema kuwa iran na syria wanachezea moto,,,iran kasema hizo ni kauli za kipuuzi .
Wameisha ona mchezo wa Syria kuwawachia kila mara umeisha. Mchezo wa zamani umeisha, piga Syria afu wakuwachie the game is over. Israel hajui lugha isipokuwa ya nguvu. Hasubuti tena kwenda kushanbulia Syria.
 
Hii ni picha imepigwa syria 5olan ikionyesha raia wa syria wakiangalia mabaki ya ndege ya israel iliyotunguliwa leo.
Picha ya kwanza hapo juu ni mabaki ya ndege hiyo yakiwaka moto ndani ya israel.

Syria wanadai wamedodosha zaidi ya ndege moja,lakini bado haijawa confirmed.

DVqN4ztVMAM8gkk.jpg:small
Itakua zimeangushwa zaidi ya moja
 
Back
Top Bottom