Syria watungua ndege ya Israel

Syria watungua ndege ya Israel

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
40,343
Reaction score
33,503
Ni breaking news,asubuhi na mapema leo drone kutoka syria iliingia anga la golan inayokaliwa na israel,kutafuta waasi wa syria.
Israel wakaitungua,na pia wakashambulia uwanja wa ndege wa T-4 ilipotokea drone.
Syria wakafyatua makombora ya kutungulia ndege na kuipiga ndege ya israel ambayo imeangukia israel japo ruban kapona japo majeruhi.
Israel wanalipa kisasi mida hii wanashambulia damusca na syria wanajibu mapigo kwa kufyatua makombora kuelekea golan.

====================

Ndege vita ya Israeli imeanguka baada ya kutunguliwa na Jeshi la Siria(Syrian Ant-AirCraft) baada ya shambulizi dhidi ya maeneo(Targets) ya Irani ndani ya Siria.

Marubani wa wili waliokuwa ndani ya ndege vita F-16 walifanikiwa kutoka ndani ya ndege na kutua salama kwa parachuti Kaskazini mwa Taifa la Israeli, inasemekana wamefikishwa hospitalini.

Israeli imesema ndege vita F-16 imefanya mashambulizi kadhaa kwa kujibu mapigo kitendo cha Irani kumshambulia Israeli kwa Drone ambayo walifanikiwa kuidhibiti.

Siria wamefanya shambulizi hilo kutokana na kitendo korofi cha Israeli.

Jeshi la Israeli limesema helicopter ya jeshi ilifanikiwa kudhibiti Drone ya Irani iliyosafiri kutoka Siria na kupenya mpaka Israeli.

"Drone hiyo iliingia eneo la Israeli na ikawa mikononi mwetu", Brig Gen Ronen Manelis Msemaji wa Jeshi la Taifa la Israeli (IDF).

Jeshi la Israeli (IDF) limesema kwa kujibu mapigo wakaamua ku-target harakati za Irani(Inasemekana ni military base) ndani ya Siria. Jeshi la Israeli likaendelea kusema mpango uliopangwa kufanyika ndani kabisa ya eneo la Siria umefanikiwa.

fbef942f6d95eb6e2a799373b10e67b9.jpg

Sauti za tafadhali zilisikika kwenye maeneo ya Israeli Kaskazini na kwenye vilima vya Golan kutokana na shambulizi la anga lililofanywa na Siria.

Wakazi wa maeneo karibu na tukio wamesema wamesikia milipuko kadhaa kwenye maeneo karibu na mipaka ya Jordan na Siria.

6b7f5c8365a07558effa7fd66fd9a340.jpg

Chombo cha habari cha Taifa la Siria kimenukuu chanzo cha habari kwa kusema ulinzi wa anga umefanya shambulizi kujibu mapigo kitendo korofi cha Israeli dhidi ya military base siku ya Jumamosi.

Irani na Urusi ni washirika wakubwa wa Raisi wa Siria Bashar AL Assad, ambao mjeshi yao yamekuwa yakipambambana na Waasi tangu 2011 nchini Siria.

11/2017,Usalama wa Magharibi waliiambia BBC kwamba Tehran (Irani) wameanzisha permanent military base nchini Siria.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameonya kwamba Israeli haitakubali huo mpango kufanikiwa.

f8edde6fecfd5b1ebbc6275ef8cb416b.jpg

Source:Israel jet crashes amid Syrian fire - army
 
Ni breaking news,asubuhi na mapema leo drone kutoka syria iliingia anga la golan inayokaliwa na israel,kutafuta waasi wa syria.
Israel wakaitungua,na pia wakashambulia uwanja wa ndege wa T-4 ilipotokea drone.
Syria wakafyatua makombora ya kutungulia ndege na kuipiga ndege ya israel ambayo imeangukia israel japo ruban kapona japo majeruhi.
Israel wanalipa kisasi mida hii wanashambulia damusca na syria wanajibu mapigo kwa kufyatua makombora kuelekea golan,

developing story
Haya Waarabu Na Waisrael wa Tanzania njooni muanze Na nyie muanze Vita yenu JamiiForums
 
Habari zinasema israel imeshambulia target 12 ndani ya syria,akitarget majeshi ya iran,watakua wana maanisha hezbollah,
uwanja wa ndege wa israel Ben gurion umefungwa kwa kuhofia mashambulizi ya makombora toka syria,
Netanyau yuko IDF HQ kujadiliana na makamanda kuhusu masahibu yaliyowakuta kufuatia uchokozi wa syria kutungua ndege yao,
 
Hii ni issue ya kitoto sana kwa Israel. Kipigo watakachokipata magaidi na wafadhili wao watajuta uchokozi wa kitoto walioufanya. Eti makombora yamelenga ndege, ikadondokea Israel, na rubani hajafa au kukamatwa. That alone gives you a clue uwezo wa hawa jamaa. Wakati nyie mnapeleka binadamu forefront kujilipua, wao ni protection ya life ya watu wao kwanza. Hamuoni tafauti?
 
wow, what can i say.., your head is sick
 
Hii ni issue ya kitoto sana kwa Israel. Kipigo watakachokipata magaidi na wafadhili wao watajuta uchokozi wa kitoto walioufanya. Eti makombora yamelenga ndege, ikadondokea Israel, na rubani hajafa au kukamatwa. That alone gives you a clue uwezo wa hawa jamaa. Wakati nyie mnapeleka binadamu forefront kujilipua, wao ni protection ya life ya watu wao kwanza. Hamuoni tafauti?
Ingekua rahiz hvyo mmarekan angekua ameishaimaliza syria lkn mpk leo ni zaid ya miaka 6 bado wanapigana tu hapo ndo wanasaidiana na mataifa makubwa yote dunian kuipiga syria
 
cf7e8740e4af681a5c9e9bd762c4f5d7.jpg

Ndege vita ya Israeli imeanguka baada ya kutunguliwa na Jeshi la Siria(Syrian Ant-AirCraft) baada ya shambulizi dhidi ya maeneo(Targets) ya Irani ndani ya Siria.

Marubani wa wili waliokuwa ndani ya ndege vita F-16 walifanikiwa kutoka ndani ya ndege na kutua salama kwa parachuti Kaskazini mwa Taifa la Israeli, inasemekana wamefikishwa hospitalini.

Israeli imesema ndege vita F-16 imefanya mashambulizi kadhaa kwa kujibu mapigo kitendo cha Irani kumshambulia Israeli kwa Drone ambayo walifanikiwa kuidhibiti.

Siria wamefanya shambulizi hilo kutokana na kitendo korofi cha Israeli.

Jeshi la Israeli limesema helicopter ya jeshi ilifanikiwa kudhibiti Drone ya Irani iliyosafiri kutoka Siria na kupenya mpaka Israeli.

"Drone hiyo iliingia eneo la Israeli na ikawa mikononi mwetu", Brig Gen Ronen Manelis Msemaji wa Jeshi la Taifa la Israeli (IDF).

Jeshi la Israeli (IDF) limesema kwa kujibu mapigo wakaamua ku-target harakati za Irani(Inasemekana ni military base) ndani ya Siria. Jeshi la Israeli likaendelea kusema mpango uliopangwa kufanyika ndani kabisa ya eneo la Siria umefanikiwa.

fbef942f6d95eb6e2a799373b10e67b9.jpg

Sauti za tafadhali zilisikika kwenye maeneo ya Israeli Kaskazini na kwenye vilima vya Golan kutokana na shambulizi la anga lililofanywa na Siria.

Wakazi wa maeneo karibu na tukio wamesema wamesikia milipuko kadhaa kwenye maeneo karibu na mipaka ya Jordan na Siria.

6b7f5c8365a07558effa7fd66fd9a340.jpg

Chombo cha habari cha Taifa la Siria kimenukuu chanzo cha habari kwa kusema ulinzi wa anga umefanya shambulizi kujibu mapigo kitendo korofi cha Israeli dhidi ya military base siku ya Jumamosi.

Irani na Urusi ni washirika wakubwa wa Raisi wa Siria Bashar AL Assad, ambao mjeshi yao yamekuwa yakipambambana na Waasi tangu 2011 nchini Siria.

11/2017,Usalama wa Magharibi waliiambia BBC kwamba Tehran (Irani) wameanzisha permanent military base nchini Siria.

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameonya kwamba Israeli haitakubali huo mpango kufanikiwa.

f8edde6fecfd5b1ebbc6275ef8cb416b.jpg

Source:Israel jet crashes amid Syrian fire - army
 
Si mbaya maana kesho tutaishambulia Syria
 
Back
Top Bottom