Sylvester Rwegasira wa TRAWU hatunae tena

Sylvester Rwegasira wa TRAWU hatunae tena

RIP Rwegasira,

Nani ataweza kufuata nyayo zako? Wengi wenye nafasi wamekuwa mbwa wa mafisadi, kazi yao kuwang'ata wakulima na wafanyakazi wanyonge wanaodai haki zao!
 
Jamani wanaJF nimesikia kuwa Rwegasira wa TRAWU katutoka, huyu jamaa alikuwa kipenzi cha migomo pale Mamlaka ya Reli, Je migomo hiyo ilikuwa inachochewa na CDM?

Je CDM wanausikaje na kifo hiki?

"Two things are infinite: the universe and human stupidity; and I'm not sure about the the universe."

Albert Einstein
 
Kanywe kikombe kwa babu, maradhi ya ubongo hayo mdogo wangu
 
migomo ni kurudisha nyuma maendeleo.......chadema ni wapenzi wa migomo!
ila kusema wanAHUSIKA NA KIFO, KIDOGO SI SAHIHI SANA
 
Tumpotezee huyu jamaa na habari zake za udaku!
 
Nimesikitishwa sana na msiba huu,huyu bwana alkuwa strong dhid ya utendaj mbov wa trl.Umefilisika akil ndg,sasa hapo cdm yahusika vp?
 
Wabunifu 24 kuchuana Wiki ya Mitindo ya Kiswahili
ban.blank.jpg


Dina Ismail​

amka2.gif
WABUNIFU 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili wanatarajiwa kuonyesha kazi zao katika maonyesho ya tatu ya ‘Swahili Fashion Week’ ambayo kwa mwaka huu yatafanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 4 hadi 6.
Maonyesho hayo yenye lengo la kuwaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maeneo hayo, kwa mara ya kwanza kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali.
Mwandaaji wa maonyesho hayo, Mustafa Hassanali anasema kwamba pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu Swahili Fashion Week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya Mswahili kutoka mwambao wa Afrika mashariki.
Anasema wanafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa Swahili Fashion Week, ambao watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali katika tamasha hilo ambalo pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya Kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.
Mustafa anaongeza kuwa mbali na maonyesho ya mavazi pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazowashirikisha wabunifu wa mavazi.
“Pia Swahili fashion Week mwaka 2010 imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyoonyeshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anayechipukia”, anasema Hassanali.
Aidha, katika kunogesha zaidi, mradi wa kupambana na malaria, Voices 11 umejitokeza kuchangia katika wiki ya mavazi ya Kiswahili ‘Swahili Fashion Week 2010’ ambapo wabunifu wake watatu watashiriki katika kuonyesha mavazi kwenye wiki hiyo.
Meneja Habari na Utetezi wa mradi huo, Fauziyat Abood, alisema kwamba wameamua kushiriki katika tukio hilo wakiamini kwamba wataweza kufikisha ujumbe kwa Watanzania kwa namna moja ama nyingine na hasa ikizingatiwa wapo katika kampeni ya kitaifa ya kupambana na malaria nchini.
Alisema kupitia maonyesho hayo wabunifu watatu, Mtoko Design, Francisca Shirima na Diana Magesa, ambao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni ambayo kwa hakika yatafikisha ujumbe kwa watu mbalimbali ambao watajitokeza katika wiki hiyo.
“Wabunifu hao wameandaa mavazi ambayo yatatoa picha halisi ya kampeni ya Malaria Haikubaliki, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki katika jukwaa bora la maonyesho ya mavazi katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa hisani ya Malaria Haikubaliki”, alisema Fauziyat.
Wabunifu watakaoonyesha mavazi katika Swahili Fashion Week kwa mwaka huu ni pamoja na Ailinda Sawe, Manju Msita, Kemi Kalikawe, Christine Mhando, Shellina Ibrahim, Farha Naaz Sultan, Gabriel Mollel, Robi Morro, Asia Idarous, Zamda George, Khadija Mwanamboka,
Jamilla Vera Swai na Made by Africa. Wabunifu kutoka Kenya ni Sonu Sharma, Moo Cow, KiKoromeo, John Kavike na Kooroo, na kutoka Uganda ni mbunifu Stella Atal.
Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na Home of Swahili Fashion week Southern Sun, Origin Africa, USAID Compete, EATV, East Africa Radio, Malaria Haikubaliki, Baraza La Sanaa Tanzania(BASATA), Ultimate Security, Monier 2000, Colour Print ltd, Global Outdoor Ltd, Amarula, Vayle Springs Ltd, ZG Films, Darling Hair, Danish make up designs, Nipashe, Bilicanas, Perfect Machinery LTD, 1 & 1 internet solutions, Sengi Tours, Ifashion na 361 Degrees.
 
...............bwana amempenda zaidi that's all.........................hatuna haja ya kutafuta mchawi.
 
wabunifu 24 kuchuana wiki ya mitindo ya kiswahili

ban.blank.jpg

dina ismail​

amka2.gif
wabunifu 24 kutoka nchi zinazoongea lugha ya kiswahili wanatarajiwa kuonyesha kazi zao katika maonyesho ya tatu ya ‘swahili fashion week’ ambayo kwa mwaka huu yatafanyika katika viwanja vya karimjee jijini dar es salaam kuanzia novemba 4 hadi 6.
Maonyesho hayo yenye lengo la kuwaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya kiswahili ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maeneo hayo, kwa mara ya kwanza kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali.
Mwandaaji wa maonyesho hayo, mustafa hassanali anasema kwamba pamoja na maonyesho ya mavazi, mwaka huu swahili fashion week itakwenda sambamba na tamasha la maonyesho ya bidhaa mbalimbali zenye asili ya mswahili kutoka mwambao wa afrika mashariki.
Anasema wanafungua milango zaidi kwa ajili ya watazamaji wapya wa swahili fashion week, ambao watapata fursa ya kununua bidhaa mbalimbali katika tamasha hilo ambalo pia litahamasisha ubunifu zaidi katika bidhaa zinazokwenda sambamba na maisha halisi ya jamii ya watu wanaoongea lugha ya kiswahili kwa kukutana pamoja na kubadilisha mawazo na kujifunza uzoefu mpya katika masuala yanayohusiana na sanaa kwa ujumla.
Mustafa anaongeza kuwa mbali na maonyesho ya mavazi pia kutakuwepo aina tofauti za burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vya muziki, uchoraji wa hina, usukaji mikeka, sambamba na semina za aina tofauti zitakazowashirikisha wabunifu wa mavazi.
“pia swahili fashion week mwaka 2010 imeandaa aina tofauti za zawadi zitakazotolewa mwaka huu kwa lengo la kutambua na kuthamini vipaji vya aina mbalimbali vitakavyoonyeshwa, ikiwa ni pamoja na zawadi ya mwaka kwa mbunifu anayechipukia”, anasema hassanali.
Aidha, katika kunogesha zaidi, mradi wa kupambana na malaria, voices 11 umejitokeza kuchangia katika wiki ya mavazi ya kiswahili ‘swahili fashion week 2010’ ambapo wabunifu wake watatu watashiriki katika kuonyesha mavazi kwenye wiki hiyo.
Meneja habari na utetezi wa mradi huo, fauziyat abood, alisema kwamba wameamua kushiriki katika tukio hilo wakiamini kwamba wataweza kufikisha ujumbe kwa watanzania kwa namna moja ama nyingine na hasa ikizingatiwa wapo katika kampeni ya kitaifa ya kupambana na malaria nchini.
Alisema kupitia maonyesho hayo wabunifu watatu, mtoko design, francisca shirima na diana magesa, ambao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni ambayo kwa hakika yatafikisha ujumbe kwa watu mbalimbali ambao watajitokeza katika wiki hiyo.
“wabunifu hao wameandaa mavazi ambayo yatatoa picha halisi ya kampeni ya malaria haikubaliki, hii ni mara yao ya kwanza kushiriki katika jukwaa bora la maonyesho ya mavazi katika ukanda wa afrika mashariki kwa hisani ya malaria haikubaliki”, alisema fauziyat.
Wabunifu watakaoonyesha mavazi katika swahili fashion week kwa mwaka huu ni pamoja na ailinda sawe, manju msita, kemi kalikawe, christine mhando, shellina ibrahim, farha naaz sultan, gabriel mollel, robi morro, asia idarous, zamda george, khadija mwanamboka,
jamilla vera swai na made by africa. Wabunifu kutoka kenya ni sonu sharma, moo cow, kikoromeo, john kavike na kooroo, na kutoka uganda ni mbunifu stella atal.
Swahili fashion week 2010 imedhaminiwa na home of swahili fashion week southern sun, origin africa, usaid compete, eatv, east africa radio, malaria haikubaliki, baraza la sanaa tanzania(basata), ultimate security, monier 2000, colour print ltd, global outdoor ltd, amarula, vayle springs ltd, zg films, darling hair, danish make up designs, nipashe, bilicanas, perfect machinery ltd, 1 & 1 internet solutions, sengi tours, ifashion na 361 degrees.



kwani threads zingine za kupost hayo mambo yako umezikosa???? Kumbuka wewe nawe ipo siku yako angalia usije zikwa maziko ya punda.
 
RIP Rwegasira, hakika TRAWU wamepoteza kichwa muhimu.
Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihidimiwe!!! tena amefariki muda mchache kabla ya kutoa tamko

Hakika katika orodha ya wapigani taifa limepoteza kiongozi shupavu kweli kweli, siku zote nilikuwa natamani sana aje kuwa katibu mkuu wa TUCTA naamini serikali ingepata joto ya jiwe ila mungu hakupendezwa juu ya hilo na kuamua kumita mja wake mapema kwa kuwa yeye amempenda zaidi
 
R.I.P Rwegasira,daima tutakukumbuka kwa utetezi wako kwa wanyonge!
 
R.I.P Mtanzania wa ukweli!!!! Tumuenzi kwa kukataa manyanyaso na ubadhirifu wa mali za umma
 
Back
Top Bottom