mzizimkava waboa, kutuletea hoja kavu
ni kama umekula mihogo,mikavu pale magomeni
uje ujibu kwa hoja, na si kwa longo longo
kama hujui mashairi,wapishe wanaojua
sawa ndugu X-Paster, hongera kutukumbusha,Kama kutunga rahisi, Wangeweza wengi sana
Kama kweli mhandisi, Ungepanga vyote vina
Mbele ya kadamnasi, Watia aibu mwana
Kujuwa kwingi kusema, Vina vyako havifani
Mmmmh!
Anyisile sikuwezi, wajua kung'ang'ania
nilishakupa uwazi, mbona walialia
nikakutungia tenzi, bado hijakuingia
ramadhani kwao dini, wewe yakuhusuni!
Krismasi na pasaka, wewe uzikumbukapo
ukatoa na sadaka, wao ni kama hawapo
hawahoji zako zaka, ulapo nyama za kopo
ramadhani kwao dini, wewe yakuhusuni!
Masuala ya imani, waachie wenye nayo
kama kuhubiri dini, si njia uiendayo
piplipili ya shambani, ikiwasha mimi sipo
ramadhani kwao dini, wewe yakuhusuni!
Hata nimechoka sasa, siioni yako nia
naomba kuaga sasa, mwenzako naenda oa
utabishana kwa sasa, jibu litasaidia
ramadhani kwao dini, wewe yakuhusuni!
na elimu kupeana, wala si kutukanana,Haya kwaheri kijana, Kwaheri ya kuonana
Kwa usiku na mchana, Si ila kuambizana
Akipenda Rabana, takuja onana tena
Kiasi kukumbushana, Kwa amri ya Rabbana
na elimu kupeana, wala si kutukanana,
na nakuaga kijana, siache salimiana,
ujumbe fikidhiana, tena wenye maana,
Jehova kupe busara, hekima isipunguke
sideeq wahangaika,kutuletea porojo
kitu moja nakuomba, mwezi utakapoanza
sisahau kunambia,uniungishe magimbi
mihogo na nyanyachungu,bila sahau mbatata
takuuzia bei cheee,ili uchukue vingi
ushindilie kwa daku,usiku kucha bugia
changanya changanya vitu,kwenye ilo tumbo moja
asubuhi kuinama ili uswali vizuri
sipati picha ikoje,kwenye icho chumba chenu
cha kuswalia mtume,kwani wengi huinama
matumbo yakishajaaa, kwa daku la jana yake
utapata magensium,upunguze kuvimbiwaaaa
Haya kwaheri kijana, Kwaheri ya kuonana
Kwa usiku na mchana, Si ila kuambizana
Akipenda Rabana, takuja onana tena
Kiasi kukumbushana, Kwa amri ya Rabbana
Sikupi wangu muhogo, sikia mwanahizayaUbungoubungo said:sideeq wahangaika,kutuletea porojo
kitu moja nakuomba, mwezi utakapoanza
sisahau kunambia,uniungishe magimbi
mihogo na nyanyachungu,bila sahau mbatata
takuuzia bei cheee,ili uchukue vingi
Ni kwa lipi haswa mpaka kuomba sana, uliza kwanza kabla ya kudandia train kwa mbele...!Nakuona jinsi ulivyofurahi baada ya kuomba sana mjadala uishe, kwan mlikua mmekamatwa pabaya.
Unampa mtu tano hata ushairi hajui!Kula tano
Tena ni yeye daima, hakuna wa kulingana,Watu wananufaika, kusoma mambo ya dini
wengi wanafaidika, makala zenye thamani
Ndugu wanashughulika, kutuletea yakini
Akuepushe na mashaka, huwe na matumaini
umuombe Subhana, Aondoshe kisirani,
Akuongoze kijana, pamoja na wana-ndani,
si usiku si mchana, dua ziwe mdomoni,
Akuepushe na mashaka, huwe na matumaini
Tuepuke na ghadhabu, Ghadhabu za Rahmani
tuepuke na adhabu, ya moto na kaburini
tuwawekee adabu, wazazi na majirani
Akuepushe na mashaka, huwe na matumaini
Unampa mtu tano hata ushairi hajui!
Kwa hiyo wewe fani yako ushairi au sio!? lol!Duuu!!!! blaza unadhani wale wachambuzi wa mpira kwenye tv na radio huwa wanaweza kucheza kama wanavyoshabikiaga au kukosoa?
Isitoshe sio lazima nijue, kwani kila mtu na fani yake.
X-Paster hodi nakuja, Jinius sichukie,
Tumaini kwako naja, Sadeeq unisikie,
Hafif andaa hoja, MziziMkavu nisikie,
Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.
Hili swali ni noma, tena laumiza ubongo,
nimesachi kila kona, mbagala, Ilala, Ubungo,
Wakujibu sijaona, wakimbia na hoja fyongo
Limeulizwa swali, anyisile ataka juzwa,
Kufunga hii Ramadhani, ni nini? la mkwaza,
Ratiba i-change kwa nini?, ndo swali lilo ulizwa.
Ratiba yabadilika, mchana kwenda usiku,
Milo mitatu kadhalika, futuri, saa sita na daku,
Swali li wazi hakika, ajibiwe apate fahamu.
Mjukuu wa kimokole
Kwa hiyo wewe fani yako ushairi au sio!? lol!