LINITATIZALO TANGU ZAMA....yupo mwenye jibu mwanana????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LINITATIZALO TANGU ZAMA....yupo mwenye jibu mwanana?????

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Anyisile Obheli, Aug 5, 2011.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wayebusi hodi naja, Waperizi sichukie,
  Mkaananii kwako naja, Nawe Kushi unisikie,
  Mwamori andaa hoja, Nzuri na nizisikie,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Nauliza tangu zama, majibu sijayapata,
  Nisijeleta dhahama, na jibu kutopata,
  Angalizo la mapema, kwa wale wenye utata,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Chonde chonde waungwana, jazba tuweke mbali,
  Tukwepe kusuguana, elimu ikawa mbali,
  Midomo tukaishona, na likawa chungu swali,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Nimehoji tangu zama, majibu hayaridhishi,
  Milo yote kutokwama, kutafuna hamuishi,
  Chapatti mwazisukuma, na uji mkijinakshi,
  Ramadhani ni mfungo am mwabadili kula.

  Milo mitatu ya mchana, mwaipeleka usiku,
  Tena mwasutama mchana, mwaomba fika usiku,
  Ili kuulipiza mchana, kwa masaa ya usiku,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Tena mwaanza futari, pale saa za jioni,
  Tena mkiwa munkari, kujikunjua usoni,
  Na mmejaa tafakari, zile za daku sahani,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Mwakandamiza majimbi, tena vyakula vizito,
  Bila kusahau tambi, ili tumbo liwe zito,
  Mwajilaza kwanye kumbi, na mkitoa hewa nzito,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Mwisrael namaliza, Masadukayo kwaheri,
  Jazba kuzipunguza, mwanakureshi tafadhari,
  Mfilisti we chomoza, sitaki zako kejeri,
  Hivi kweli mnafunga, au mwabadiri ratiba.
   
 2. S

  Senior Bachelor Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mimi pia litatizwa, dhimaye lishindwa jua
  Ramadhani ikabezwa, kila ilipowadia
  Utadhani wakimbizwa, jioni ikiwadia
  Ramadhani megundua, ni zaidi ya mfungo.

  Jioni kikaribia, wanawaza kufuturu
  Uji ni wa kuanzia, tumbo kuliweka huru
  Zafuata na bagia, na viazi vya Luguru
  Kumbe Ramadhani bwana, ni zaidi ya mfungo.

  Usiku wote tafuna, tumbo likae sawia
  Jua zikichomozana, mbavu zote zi sawia
  Hapo mchana kichuna, hakuna sababu kulia
  Ulaji wa Ramadhani, ratiba tu badili

  Lakini mimejifunza, dhimaye sio chakula
  Msingi matendo kwanza, na sio hiyo ratiba
  Basi! Swaumu ikiwa kali, kwa nini wanalalama?
  Ramadhani ni ibada, si adhabu asilani

  Gulioni ukienda, tajua ni Ramadhani
  Bei zote zimepanda, badala ya kushukani
  Kuelewa lanishinda, walaji meongezeka?
  Tutazame Ramadhani, kwa kiimani zaidi.

  Najua nimekanganya, unaweza sielewe
  Nakubali funga hiyo, na ninaiamini pia
  Lakini waifanyao, wasiifaanye adhabu
  Raamadhani Kareem, waungwana natakia.
   
Loading...