Swali..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali..!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Anyisile Obheli, Jun 9, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  X-Paster hodi nakuja, Jinius sichukie,
  Tumaini kwako naja, Sadeeq unisikie,
  Hafif andaa hoja, MziziMkavu nisikie,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Nauliza tangu zama, majibu sijayapata,
  Nisijeleta dhahama, na jibu kutopata,
  Angalizo la mapema, kwa wale wenye utata,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Chonde chonde waungwana, jazba tuweke mbali,
  Tukwepe kusuguana, elimu ikawa mbali,
  Midomo tukaishona, na likawa chungu swali,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Nimehoji tangu zama, majibu hayaridhishi,
  Milo yote kutokwama, kutafuna hamuishi,
  Chapatti mwazisukuma, na uji mkijinakshi,
  Ramadhani ni mfungo am mwabadili kula.

  Milo mitatu ya mchana, mwaipeleka usiku,
  Tena mwasutama mchana, mwaomba fika usiku,
  Ili kuuulipiza mchana, kwa masaa ya usiku,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Tena mwaanza futari, pale saa za jioni,
  Tena mkiwa munkari, kujikunjua usoni,
  Na mmejaa tafakari, zile za daku sahani,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadiri kula.

  Mwakandamiza majimbi, tena vyakula vizito,
  Bila kusahau tambi, ili tumbo liwe zito,
  Mwajilaza kwanye kumbi, na mkitoa hewa nzito,
  Ramadhani ni mfungo ama mwabadili kula.

  Tumaini namaliza, X-Paster tafadhari,
  Talmud kupunguza, Sadeeq tahadhari,
  Maralia we chomoza, sitaki zako kejeri,
  Hivi kweli mnafunga, au mwabadiri ratiba.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ramadhani si chakula, bali ni jina pima
  na kama ni chakula, hapo siwezi pima
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jun 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bisimilahi naanza kwa Jina la rahmani.
  Mola aliye muweza, Anaye tupa ihsani
  Anipe uwezo kwanza, Kukujibu ukumbini

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu

  Mwezi huu wa fadhila, Na mwezi wa ihsani
  Sio mwezi wa chakula, Kushindilia tumboni
  Au mwezi wa kulala, Kukoroma kitandani

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu

  Mwezi huu wa ibada, Na kusoma Qur'aani
  Ni mwezi wenye faida, Nyingi ziso na kifani
  sio mwezi wa kawaida, Ni mwezi wenye thamani

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu

  Fadhila zake ni nyingi, Zinazovuka mipaka
  Twajitahidi kwa wingi, Kamba ya Mungu kushika
  Na Swalah ndio msingi, wa dini yetu hakika

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu

  Mungu Amesharidhika, Uislamu ndio dini
  Milele tahifadhika, Kitabu cha Qur'aani
  Tafuta na utachoka, Makosa ndani huoni

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu

  Mwezi huo wa baraka, Wa amani na imani
  Ninamuomba Rabuka, Pepo iwe maskani
  Ni mwisho wa kuandika, Nimefika kikomoni

  Ramadhani ni ibada, Sote yatulazimu
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nafurahi kuipata, hii threat ya leo
  namimi sitaiacha, itabidi nichangie
  ramadhani yatatiza, kwangu kupata majibu
  ramadhani huhamisha, masaa ya kula msosi

  wengi tunajiuliza ,kwanini yanatokea
  siku zile za mfungo, vifafa vinapungua
  mfungo ukishaisha, ajali nyingi kuanza
  ramadhani huhamisha, masaa ya kula msosi

  nimeshapata majibu, majini nayo hufunga
  pale yanapofungua, njaa ya damu huwaka
  ndo maana ajali nyingi, vifafa na maajabu
  wanadamu na majini, hufunga wote pamoja


  mwezi wa kuiba nyota, hasa wakikupa daku
  humwaga majini mengi, chuma ulete kazini
  mchana kupiga soga, jioni ni mahesabu
  mwezi wa changa la macho, siri kubwa yafichika

  ni mwezi wa maagano, shetwani na wanadamu
  mwezi kuabudu nyota, mwezi nayo maruhani
  kuipanga mikakati, ya kuuongeza majini
  mwezi huu ni hatari, shetwani kuabudiwa


  uhamishaji masaa, kula msosi mzito
  magimbi tambi chapati,mihogo na vitumbua
  vyote hivi kusanyia, kwenye hili tumbo moja
  matumbo kuunguruma, kwa misosi shindiliwa


  siku zile za mfungo,nyumba ndogo hufukuzwa
  mfungo ukishaisha, nyumbandogo karibia
  sehemu zile za beach, condom hadi gunia
  zote hizi hutumika, kufungua huu mwezi

  nawashauri wenzangu, kuwa ni changa la macho
  mwamedi kawazingua, hamtakuja elewa
  mwapata njaa ya bure, hakuna hata thawabu
  mungu mnayemwabudu, kweli ananichekesha.
   
 5. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  1 - Kwa Myahudi ili Kuuponya mwili wake ni lazima achukue vumbi la udongo ndani ya kivuli cha choo cha nje, changanya na asali halafu kula" Gittin 69a.

  2 -Akitoka mtu nje ya mlango wa choo hapaswi kufanya ngono mpaka asubiri kwa muda wa kutosha kutembea nusu maili, kwa sababu pepo wa choo yuko pamoja naye kwa wakati huo, kama akifanya hivyo (akifanya ngono), watoto wake watakuwa kifafa. "83- Gittin 70a.


  3 -Mwanamke ambaye alikuwa anafanya ngono na mnyama anastahiki kuolewa na kuhani wa Kiyahudi. Mwanamke ambaye anafanya ngono na pepo pia hustahiki kuolewa na kuhani wa Kiyahudi Yebamoth 59b

  Ooovyoooo!
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nakupa pole sideeq, kwa kutuletea soga
  wenzio twaleta point, we watuletea hewa
  kati yetu sisi sote, yupi kwetu myahudi
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimya

  ukiingia vitani, usikimbie risasi
  kwa kulipua jirani, badala ya mpiganwa
  we ukiishiwa point, hukimbilia yahudi
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimyaa
   
 7. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  1 - Myahudi ni lazima ale kiapo cha uongo wakati goyim anapouliza kama vitabu vyetu vin kitu chochote dhidi yao."Szaaloth-Utszabot, The Book of Jore Via 17.
  2 -Akum (asiye Myahudi) ni kama mbwa. Ndiyo, Maandiko Matakatifu yanasema tumuheshimu mbwa zaidi kuliko wasio-Wayahudi. "Ereget Raschi Erod, 22 30
  .......atafutaye hupata.
   
 8. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  sideeq wahangaika, kama vile mfa maji
  hakosi kutapatapa, lazima miguu arushe
  hatuongei yahudi, ongelea ramadhani
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimya

  kitabu cheni koran, kinaruhusu uwongo
  kudanganya makafiri, unapoyaconvert
  kutetea wislam, uongo waruhusiwa
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimya

  jihad itatukuzwa, na hawa wana wa kambo
  uwongo utatukuzwa, ili kudanganya umma
  wakirsto wayahudi, wakamatwe wauawe
  kama hawatakubali, hii dini ya mtume

  dunia inashangazwa, ugaidi ongezeka
  kitabu chawafundisha, kujilipua mabom
  kumpigania mola, waweza kujilipua
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimya

  mihadhara inazidi, kona nyingi daslamu
  kuhubiri maugomvi,chuki kwa dini zingine
  mmeikosa elimu, kumkichwa kombolewa
  kama waishiwa point, bora unyamaze kimyaaaaaa
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sadeeq ewe pole,
  na tena nakupa pole,
  ilombatana na ole,
  kutuletea gobole.

  angalizo nimetoa,
  na sikutaka potoa,
  zaidi ilimu toa,
  talmud acha toa.

  si mahali pa hasira,
  bali ni hoja kuchora,
  iache ikikukera,
  usiruke kama chura
   
 10. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  X-Paster e ndiyo,
  sijaridhika nduguyo,
  bado nahitaji moyo,
  kuyajua ulonayo,

  na mimi siyo kilaza,
  ilimu nimekatiza,
  quran lipomaliza,
  maswali nikayajaza.

  ni wa Mungu utukufu,
  ye zaidi mtakatifu,
  mwenye kufufua wafu,
  ye tena ni mwaminifu,

  usiletee thawabu,
  zaidi nataka jibu,
  je kufunga ni wajibu,
  ama ni ka taratibu
   
 11. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,720
  Likes Received: 8,272
  Trophy Points: 280
  Waungwana asalaam, ukumbini nimefika
  nimekamata kalam, karatasi nimeshika
  ila nakosa faham, ni nini cha kuandika,
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  si kama nataka vita, bali nakwepa majungu
  Sikulala na kuota, au kutumwa na Mungu
  ninapatwa na utata, na moyo una machungu
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Labda niulize swali, Anyisibe na wenzako
  wewe huwa ukiswali, na kuomba Mungu wako
  wao huja na maswali, kuuliza nia yako
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Swali la pili jamani, pole kama nakukwaza
  kufunga huwa ya nini, umeshawahi kuwaza
  watu wote kila dini, sauti zao hupaza
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Nasema kweli ibada, ya kunyenyekea kwake
  baba, mama hata dada, yatupasa kwenda kwake
  tukidhaifisha mwili, roho inasonga kwake
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Waweza funga staftahi, ama mlo wa mchana
  ukaomba asubuhi, jioni ukala pina
  ukiamua kuwahi, nia yako ndo ya mana
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Usinikashifu mimi, sipofanya utakavyo
  usiitukane dini, ili niheshimu yako
  kufunga nafunga mimi, njaa bado ije kwako
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.

  Nilishasema tangia, nini maana kufunga
  jambo linakusumbua, ama unaomba kinga
  ibada umeamua, kila mwezi nitafunga
  Kufunga kweli ibada, hata Wakristo tunayo.
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  nipo kutaka ilimu,
  wala sitaki laumu,
  zaidi taka fahamu,
  kuuondoa ugumu.

  Compaq nimekupata,
  wala hakuna utata,
  nadhani hujanipata,
  hili swali siyo tata,

  mkristo ni wake uhuru,
  kufunga na kushukuru,
  tena wala si kufuru,
  anafunga kwa uhuru.

  wengine wana lazima,
  siyo baba wala mama,
  sharia kuwasakama,
  kwao tena ni lazima.

  Compaq mi nakuomba,
  na sikufungi kwa kamba,
  endelea kuyachimba,
  uyajue kwa kuomba.

  hili swali bado liko,
  na majibu yangaliko,
  sijalidharau lako,
  limeongezea msako.
   
 13. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tupatie hiyo aya basi, kama mimi ninavyokupa ya Talmud:
  Jews may use lies ("subterfuges") to circumvent a Gentile.Baba Kamma 113a
  Tupe aya kama ninavyokupa mimi hapa:
  "Even the best of the gentiles should all be killed Minor Tractates. Soferim 15, Rule 10
  "Samson said to the servant who held his hand, "Put me where I can feel the pillars that support the temple, so that I may lean against them." Now the temple was crowded with men and women; all the rulers of the Philistines were there, and on the roof were about three thousand men and women watching Samson perform. Then Samson prayed to the LORD, "O Sovereign LORD , remember me. O God, please strengthen me just once more, and let me with one blow get revenge on the Philistines for my two eyes." Then Samson reached toward the two central pillars on which the temple stood. Bracing himself against them, his right hand on the one and his left hand on the other, Samson said, "Let me die with the Philistines!" Then he pushed with all his might, and down came the temple on the rulers and all the people in it. Thus he killed many more when he died than while he lived. (From the NIV Bible, Judges 16:26-30)"
  Samson alijitolea maisha yake kwa ajili ya watu wake!
  Mipango inafanyika ili siku moja nianze kuja ichambua Talmud katika kona za Dar es salaam.
  *Uudandao (Talmud) ndio ukubwagao.
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hivi kinatumiwa na watu gani hicho ki-talmud? maana mi huwa sikwelewi nalo,
  hivi kina wafuasi kwa tanzania, jambo jema ukiichambua qurani ili waelewe kuwa kuna uhsiano baina yao
  na majini ili kusaidia kazi yahya, lakinikwa hiyo talmud, ataaa, qurani yenyewe hujaimaliza kuirahisisha kwa wafuasi wake unakimbilia talmud kazi kweli kweli! kha!!!
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Talmud ndio nini, mimi nashinda elewa,
  talmud dini gani,mwenzenu siielewi
  au ni y awahahudi, au pia ya wahindu
  mwenye majibu jamani, naombeni ayalete

  dar es salaama yote, masinagogi hayapo
  kama yale yalojengwa, kwa wayahudi ziraeli
  hatuna masinagogi, talmudi hatuhusu
  umeshaishiwa point, unaleta talmudi

  sideeq ninakuomba,nionyeshe sinagogi
  lakutumia talmudi,ili nije kuelewa
  wakristo tafadhali, hatutumii talmudi
  kwahiyo haituhusu, kalete hoja ingine
   
 16. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #16
  Jun 12, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hodihodi naingia, kijiweni pokeani
  Sikia wangu usia ,we Yahudi namba wani
  Sikughilibu rupia, Karaha ya duniani
  SILIMU EWE YAHUDI; MI KWAKO NAKUUSIA

  Ipi raha ya dunia?, silimu sifanye shaka
  Wapata akhera pia, malipoyo takufika
  Ndio dini Islamia ,Ni adhimu isi shaka
  SILIMU EWE YAHUDI; MI KWAKO NAKUUSIA

  Wengine wamo kundini, Uyahudi kujikisi
  Yahudi si yao dini, mafatani wajihisi
  Kikabila pia duni , ajabu wajirahisi
  SILIMU EWE YAHUDI;MI KWAKO NAKUUSIA

  Kwa kabila we yahudi?, au dini watwambia?
  Sio uvumba si udi, wakutafuta kimbia
  Ulaya kwao yahudi, hawataki asilia.
  SILIMU EWE YAHUDI;MI KWAKO NAKUUSIA
  *
  Zohar (I, 160a):"Rabbi Jehuda said to him [Rabbi Cezkia]: 'He is to be praised who is able to free himself from the enemies of Israel , and the just are much to be praised who get free from them and fight against them. 'Rabbi Chezkia asked, 'How must we fight against them?' Rabbi Jehuda said, 'By wise counsel thou shalt war against them' (Proverbs, ch. 24, 6). By what kind of war? The kind of war that every son of man must fight against his enemies, which Jacob used against Esau - by deceit and trickery whenever possible. They must be fought against without ceasing, until proper order be restored. Thus it is with satisfaction that I say we should free ourselves from them and rule over them."
   
 17. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #17
  Jun 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yahudi ni kitu gani,
  ama ni kabila gani,
  utweleweshe jamani,
  tuijue kwa makini,

  umekimbia swali,
  umekwenda sana mbali,
  sijifanye wewe mkali,
  utakutana wakali,

  ya topiki namba moja,
  hujayajengea hoja,
  kutuletea viroja,
  talmud siyo hoja.
   
 18. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hutuambia ni dini , kwa wengine ni kabila
  Yahudi yu mashakani,hapajuwi pa kushika
  Halakha yasema dini ,kabila hukubalika
  SILIMU EWE YAHUDI;MI KWAKO NAKUUSIA

  Wakabwabwaja wazushi , kwa kujitia mazonge
  Bileshi ya matamshi , warudi kisengesenge
  Uyahudi si ucheshi, chuki kwao ni vidonge.
  SILIMU EWE YAHUDI;MI KWAKO NAKUUSIA
  *To communicate anything to a goy about our religious relations would be equal to the killing of all Jews, for if they knew what we teach about them they would kill us openly." - Libbre David 37.
   
 19. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Samahani nikichangia bila lugha ipasavyo hapa. Namwomba sana mtaalamu wetu wa dini ya Uyahudi na kitabu cha Talmudi atueleze:
  Je kile Libbre David ni nini?? Je ni sehemu ya Talmud?? Ni lugha gani?

  Maana kwa njia ya kupiga google nimekuta madai eti nukuu hii ni uwongo mtupu hakuna sehemu kwa jina hili
  (au jina la kufanana) katika Talmudi popote duniani!

  Sasa naomba jibu:

  a) Nukuu yako, mkuu, inapatikana katika toleo gani ya Talmudi?
  b) wewe umeikuta wapi (yaani Talmudi kwako nyumbani - toleo gani? AU mahali kwenye intaneti kwa kopi-paste - wapi?? AU sauti ya malaika kwako wakati gani? malaika gani?)
  c) Je unakubali ya kwamba jina "libbre David" inaonekana zaidi kama Kiitalia lakini haiwezekani kuwa lugha ya Kiyahudi? Unaonaje?
   
 20. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  na asiondoke bila kutoa majibu hapa, kwa upande wangu mie nashukuru kwa ufuatiliaji wako mkuu, maana kha hii talmud nimejaribu atupatie wapi kaitoa bila mafanikio amekuwa anaruka viunzi sana
   
Loading...