Swali la Ugomvi: Kwani Lowassa Kawa Mganga wa Kienyeji?

This is character assassination, uovu WA Lowassa Ni WA kufikirika au kudhaniwa tofauti na uhalisia.

Mleta hoja SI bure naona karogwa na waganga WA kienyeji.
 
Mie nafikiri ili tufikie Neema tunayoitaka Watz, Mungu kaona ngoja kwanza atupitishe kwenye laana! Laana yenyewe ni kumshabikia Fisadi bila kujiuliza......!
 
Hii ya Lowasa kukaa ikulu miaka mitano tu mnaitoa wapi? akiamua kukaa miaka kumi mtafanyaje? Na baada ya hapo mtandao wao wakiamua Rais anayefuata ni Rostam mtafanyaje? (Naamini mnajua jinsi nguvu ya mtandao wao inavyoweza kuwabadilisha mkaanza kumsafisha 'Rostam for 2025').

Kwani siye malofa huku uswahilini si ndiyo tutaendelea kuwa wapiga kura au wataleta wa Kwao au unahofu nao watageukia magoli ya Mikono?.

Mkuu acha hofu huu ni mwanzo tu wa Nguvu ya Umma-kinachohitajika ni watu kama akina Mzee Mwanakijiji kuendelea kuwapa nafasi ya kufikiri wale ambao bado hawajaamka zoezi ambalo zaidi ya miaka kumi iliyopita MMM ameifanya kwa nguvu zake zote na ni Mungu tu ndiye anayeweza kumlipa.

Bado mimi na amini tuna vijana watakao tufikisha kwenye neema kama watasimia haki na kutumia nafasi hii ya Vuguvugu na mwamko wa wananchi-mfano.Mhe.Zitto na Chama chake ACT -Wazalendo badala ya kuelekeza nguvu kwenye Uraisi kama kweli wanataka kuwa Chama makini wangelekeza nguvu yao ndogo waliyokuwa nayo kwenye Udiwani ,lakini kwa vile Chama Tawala ina mkono wake kwenye uanzishwaji wake basi nao wamo kwenye Ugombea wa kiti cha Uraisi.

Hii ni ajali kama ajali zingine na mianya na changamoto itakayopatikana baada ya Oct.2015 kila mtanzania atakuwa na Mtazamo tofauti kuhusu hatima yetu kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji you are wasting your time! Tanzanians have spoken: Rais wetu ni LOWASSAAAAAAAAA!!!!!!!!!!
 
Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...

Imeandikwa ndani ya Kitabu kitakatifu kuwa Mtu anyeongea sana ni muongo .
 
Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...
Tatizo lako hapa,umeandika maneno meeengiii...! Lkn hayana maana hii ndo sababu ya kuambiwa unachosha. Halafu Mzee Mwanakijiji Dunia Tz isingekuwa hivi km watu wote wangekuwa na akili na mawazo yako..! Unachokera watu siku hizi,unaandika kwa kuwafanya watu wengine km hawana akili. Tunajua lowassa ana mapungufu,lkn nani mkamilifu kati ya wote!!?? Ukitaka kujua uwezo wetu wa kufikiri,gombea ww hata ubunge tu ndo utajua nani ana akili kati yetu.
 
Last edited by a moderator:
Mpango wa katiba mpya ni matakwa ya wananchi ambayo Lowassa anayaunga mkono kwa sasa kupitia ukawa.

Hao watuhumiwa mfano babu Seya na wengine unaweza kunithibitishia bila shaka kwamba walifungwa kwa makosa halali? Njoo utuambie

Hao

Jukumu la kuthibitisha bila shaka ni la mahakama. At least kama aliona haki haikutendeka angesema ataishawishi mahakama ili kesi isikilizwe upya. Kutoa watuhumiwa wa jinai gerezani ndo mamlaka yaliyopitiliza ya rais tunayoyalalamikia kila siku. Siku nyingine akimtoa Rostam gerezani (kama atafungwa) mtawezaje kulalamika?
 
Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...

Sawa...lakini ni wajibu wa mwandishi kuwa mbunifu kuvutia wasomaji wasiboreke wanaposoma chapisho lake. Wewe kama mwandishi huwezi epuka hilo kisa tu unadhani kuwa ulichoandika kina mashiko. Kuna waandishi wengi tu wanaandika machapisho yenye mashiko lakini ni wabunifu na simulizi zao zinavutia kusoma. Wewe MMM kama umekosa kipaji hicho, husilaumu wasomaji wako kwa kushindwa vutiwa chapisho lako, sababu tu limekosa ubunifu na linaboa, hata kama ulichoandika kina mashiko!
 
Mmesahau kuwa siasa ni imani? Watanzania waliiamini CCM kwa muda mrefu, lakini CCM imeshindwa kukidhi matarajio yao. CCM, haiaminiki tena na kwa kweli hata yenyewe inajua haiaminiki (sikilizeni kampeni zao!). Kwa jinsi CCM ilivyoongoza, ilikuwa inashangaza sana watanzania kuendelea kuipigia kura.

Watanzania wanataka mabadiliko, wameshindwa kuyapata ndani CCM waacheni wayatafute nje ya CCM.

Kwa hiyo pengine issue hasa wala sio Lowassa. Kwa namna watanzania walivyoichoka CCM, hata kama CDM/UKAWA wangemsimamisha Mzee Mwanakijiji kugombea urais, bado tungeshuhudia the same determination kutoka kwao.

Mungu anataka kutenda jambo kwa Tanzania, anataka kujibu maombi ya muda mrefu ya watanzania!
 
Uzi wako unaboa hauvutii kusoma..nimeishia para ya kwanza tuu.....hivi kwa akili yako ilivyo finyu unatushauri tuendelee kuichagua ccm pamoja na kututia umaskini wote huu????...ww utakuwa miongoni mwa wazee...maana twawezeshwa pamoja na ku edit utabiri wao walisahau kufuta kipengele cha wanaoipenda ccm na kusema ni wazee na wasio na elimu....ww elimu najua unayo ila uzee ndo umekufanya uipende ccm...poleee....
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Wewe mzee unajitoa fahamu bure; Uraisi ni taasisi sio mtu mmoja na watu wameamua kuangalia upande wa pili bila kujali anayebeba hiyo bendera awe Lowassa au ng'ombe mzee wameamua hivyo. Wala usijipe moyo Lowassa anashindwa uchaguzi huu bila mizengwe kutawala kwa kuwa huyo unayempigia debe hana jipya wala nyenzo ya kumuwezesha kuyatimiza anayoahidi wakati taasisi yake imeikataa katiba ya wananchi yenye maadili ya uongozi na ulinzi wa rasilimali za nchi.
 
ha ha haaa.....Magufuli amekuja vipi hapo? haujajibu hoja

Ni mwizi kama wezi wengine waliko CCM
Mkuu sawa ni mwizi nani siyo mwizi? Si ccm si ukawa wote ni dugu moja period. Tz bado ina safari ndefu sana ukombozi ni ndoto ni Neema YA Mungu tu!
 
Yani sisi ni kama LOWASA na LOWASA kama sisi hutaweza kutulazimisha tumchukie mtu ambaye hatuoni ubaya wake

Tatua mkataa mtu yoyote eti kwa sababu wewe una chuki zako binafsi
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM
Umeshatuambia sana kuhusu Lowassa na ubaya wake,nadhani kiungwana imetosha zaidi ya hapo uanchofanya ni kutuvunjia heshima na kulazimisha Matakwa yako,acha watu waamue wenyewe!!!

Kwa maelezo yako naona na wewe either ni mganga au Mamajusi maana umeshatabiri kwamba Lowassa tutamwacha na kwamba tutajuata na kusema kwamba "tulipotoshwa"
UWE NA UHAKIKA,MIMI SIYO MMOJA WA WATAKAOJUTA KUMPIGIA KURA LOWASSA HATA KAMA HAKISHINDWA!!!
MARK MY WORDS,I WILL NEVER REGERET,I COULDNT CARE LESS,I will vote for EDWARD NGOYAI LOWASSA
 
Back
Top Bottom