Swali la Ugomvi: Kwani Lowassa Kawa Mganga wa Kienyeji?

Hii ya Lowasa kukaa ikulu miaka mitano tu mnaitoa wapi? akiamua kukaa miaka kumi mtafanyaje? Na baada ya hapo mtandao wao wakiamua Rais anayefuata ni Rostam mtafanyaje? (Naamini mnajua jinsi nguvu ya mtandao wao inavyoweza kuwabadilisha mkaanza kumsafisha 'Rostam for 2025').


Ndugu...,

Watanzania sio wajinga hivyo..., hakuna namna Lowassa anaweza kuingia na kukaa Ikulu kwa nguvu zake bila kupigiwa kura .. Na wagombea wote wa uraisi wanagombea kupitia vyama vyao na kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ikiwa Lowassa atapata uraisi, kitakacho mpa nafasi nyingine ya pili baada ya miaka yake 5 ya kwanza , ni UTENDAJI WAKE WA KAZI .., pamoja na chama/umoja wa vyama vilivyomuingiza madarakani ... Hawezi kupuuza kuara zilizompa DOLA...

Nchi hii ni ya vyama vingi, endapo EL na team yake watachukua Dola , upinzani (CCM) utakuwa macho kumkosoa na kuwajulisha wananchi ubaya wake na team yake katika kutawala...

Take it fro me, HAIPO NAFASI TENA KATIKA NCHI HII MTU KUONGOZA/KUTAWALA APENDAVYO katika wakati huu wa mabadiliko makubwa DUNIANI ya MAENDELEO YA MAWASILIANO . . .
 
Kuna waganga wengine wana dawa hata za kuwafanya watu wawe Freemasons...na wanapata wateja vile vile!


Mzee wangu Mwana KIJIJI . .

Pole kwa UZEE na UCHOVU (sijui uchovu wa nini..)
Kama ni wewe umeandika haya maneno hapa ..., basi na wewe ni MSHIRIKINA ...
Hivi huoni kweli sababu ya watu kumkimbilia EL ..?!
My friend .., Tanzanians are tired of CCM ..., ushirikina wako haukusaidii hata kuona hili . . ?!
Kwa hiyo kwa unavyoyaona mambo leo, hata waliokuwa wakiimba "TUNA IMANII NA LOWASSAAA . . " ndani ya mkutano Mkuu wa CCM mbele ya JK ..., nao wamelogwa na u freemason ...?!
Kwa hiyo ile hoja yenu kuwa EL anamwaga mapesa kila kona..., IMEPOTELEA WAPI SASA . . ?
Sasa Mwanakijiji, wewe na wenzako msiomtaka EL ..., tuleteeeni mapema sababu za sisi wengine kutaka MABADILIKO . . , hebu semeni, Lowassa ni FREEMASON ? au AMETUHONGA na katuhonga kiasi gani . . ?!
 
Peleka hii Meseji kwa familia yako ila sisi tumeisha kata uamuzi wa kumpatia huyo mganga wetu wa mabadiliko. LOWASSA NI RAIS WA AWAMU YA TANO.
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

huyu mzee kuna uzi aliwah sema hana chuki na lowasa wala hajawah kumwita jina baya huyu lowasa lakn leo anamwita mganga wa kienyeji,sijui mchawi,sijui nn........
ebu msome ktk moja ya maneno yake hapa chini akijitetea






Kama wengi "wanaomwamini" wapo sisi wachache tunawasumbua nini? Kama hoja zetu hazitishii safari isiyoeleweka kwanini muone ni lazima tukae kimya au tuunge mkono tu? "Wengi" wanaweza wasithubutu kuwaambia ukweli kwani "wengi" wanaweza kuwa wamenogewa na togwa ya matumaini yasiyokuwepo na hivyo hawataki kufikiri au wanaogopa kusema hadharani kile wanachofikiria kwani wataonekana "wasaliti" na wasiounga mkono mabadiliko. Hoja ya "wengi" ni miongoni mwa hoja muflisi. Hitler alipotafuta power ilifika mahali ungeweza kuamini Ujerumani nzima walikuwa wanampenda; Idi Amin vile vile, hata Slobodan Milosevic na wengine wengi ambao historia baadaye ilikuja kuwahukumu vikali.

Wachache (katika jamii hizo) waliothubutu kusema dhidi ya watawala waliotaka madaraka kwa nguvu ambayo tumeiona kwa Lowassa ndio walikuwa maadui wa "state" kwani walionekana hawataki "mabadiliko" wakati "wengi" wanaunga mkono. Ukimya wa wachache unawapa ruhusa wengi kutawala wapendavyo. Bahati mbaya sijawahi na Mungu anipe neema sitowahi kusukumwa na hisia za "wengi". Maana wengi wakipotoka, wamepotoka bwana!

Ni jukumu la wachache - au hata mmoja tu - kupaza sauti nyikani hata kama wenye kusikia na vipepeo, mchwa, siafu na nyuki! Kuliko kuhesabiwa miongoni mwa wengi waliopotea ni bora niachwe miongoni mwa wachache wabezwao. Hili kwa kweli halinisumbui.

NB: Sina chuki dhidi ya Lowassa; sijawahi kumtukana, sijawahi kumuita jina lolote lisilompasa, sijawahi kumdharau au mbele ya watu wengine (nje ya mitandao). Ninamheshimu sana tu kilichopo ni kuwa nina tofauti kubwa za msingi kati ya mwelekeo wake wa kiuongozi na kile ninachoamini kiongozi anapaswa kuwa na nimejipa jukumu la kuwaonesha wengine hili. Kama wengine wanavyomuunga mkono hadharani na kwa kila njia ni jukumu letu na sisi wengine kumpinga mkono hadhrani na kwa kila njia.

Usikwazike. Msikwazike.

MMM
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji, kuna agenda ya siri, kwaani Mgombea huyo hataweza kutimiza majukumu yake kama inavyoeleza katiba yetu ibara ya 37 (5) “ ENDAPO KITI CHA RAIS KITAKUWA WAZI KUTOKANA NA RAIS KUFARIKI DUNIA, KUJIUZULU AU KUPOTEZA SIFA ZA UCHAGUZI AU KUTOMUDU KAZI ZAKE KUTOKANA NA MARADHI YA MWILI AU KUSHINDWA KUTEKELEZA KAZI ZAKE ZA URAIS BASI MAKAMU WA RAIS ATAAPISHWA NA ATAKUWA RAIS KWA MUDA ULIOBAKI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5 ILIYOBAKI".

Hivyo Rais wetu ajaye anaweza kuwa JUMA DUNI HAJI.

Hata hata ukitaka watu wafikirie hilo hawataki kufikiria; manake ni kuwa atakuwa kiongozi kutoka CUF.... implication yake hiyo nayo inatisha!
 
Lowassa kwenda kwa mganga wa kienyeji wala sio tatizo ila tatizo kubwa ni kwamba lowassa sio muadilifu na anatuchonganisha kwa udini hafai kuwa Rais hata kuwa mkiti wa kijiji hafai
 
Mzee Mwanakijiji, Tanzania hii kila mtu anayo haki na uhuru wa kuamua mambo yake bila kuingiliwa, mradi havunji katiba, sheria wala kanuni za nchi. Katika masuala ya siasa na uchaguzi kila mtu anaweza kuelekea upande wowote. wapo ambao ni bendera kufuata upepo na wapo ambao wameamua kwa uthabiti kuwa upande fulani kwa ubaya au kwa uzuri. hata wewe unazo sababu za kuwa uoande wa Magufuli kwa sasa, hata kama haukuwa upande wa Kikwete zamani (or am I imagining this?). Hakuna mtu mwenye haki ya kumhoji mwenzake kwa nini ameamua kuwa upande fulani..

Sasa mbona wengine mnanihoji upande wangu kwa kuwa naamini kuwa Lowassa hafai kama kiongozi? Au haki hii ya kuwa upande wowote bila hata sababu ya msingi inawahusu wanaomtaka Lowassa tu lakini wanaompinga Lowassa hawana?
 
we mwenyewe mganga jinsi unajikoroga unasikitish unajifanya unaakili kuliko watanzania wanaoona mambo kwa jicho la mbali rudi nyumbani au endelea kulamba makalio ya wakubwa unachosha na hadithi za wagagagigigoko
 
Atamaliza waganga wote Duniani lakini katu asilani hawezi kuingia ikulu yeye ataishia kuiona tu kwenye vyombo vya habari hapa ni magufuli tu
Mumezoea ana kupanga watu wa kuingia ikulu eti chama cha familia eti usalama wa taifa nani dunia hii alishinda nguvu ya umma wachawi wa msoga nyie
 
Mzee Mwanakijiji,

Nianze kwa kusema, mimi ni mmoja wa wasomaji wako wa makala za kwenye magazeti na kwenye mitandao. Kwa kuwa mpaka muda huu ninavyoandika ujumbe huu, bado sijaacha kusoma makala zako japo dalili zinaanza kuonesha, naweza KUTAMAUKA halafu nikaacha kusoma makala zako. Siku nikipata nafasi ya kukuandikia na kuielezea hoja yangu ya kumuunga mkono Lowassa (ambaye sikuwahi kumuunga mkono hapo nyuma), kwa kirefu kihistoria na Kibiblia nitafanya hivyo ila kwa sasa nikuulize swali moja; Wewe ungependa akina nani wangekuwa wagombea wa urais mwaka huu?

Asante.

Kuacha kusoma kwako makala za Mzee Mwanakijiji hakuondoi uhalisia wa kile anachokisema. Kama hutasoma makala zake wapo watakaosoma, na baada ya oct 25 tutajua kati ya ninyi na MMM yupi mkweli.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu...,

Watanzania sio wajinga hivyo..., hakuna namna Lowassa anaweza kuingia na kukaa Ikulu kwa nguvu zake bila kupigiwa kura .. Na wagombea wote wa uraisi wanagombea kupitia vyama vyao na kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ikiwa Lowassa atapata uraisi, kitakacho mpa nafasi nyingine ya pili baada ya miaka yake 5 ya kwanza , ni UTENDAJI WAKE WA KAZI .., pamoja na chama/umoja wa vyama vilivyomuingiza madarakani ... Hawezi kupuuza kuara zilizompa DOLA...

Nchi hii ni ya vyama vingi, endapo EL na team yake watachukua Dola , upinzani (CCM) utakuwa macho kumkosoa na kuwajulisha wananchi ubaya wake na team yake katika kutawala...

Take it fro me, HAIPO NAFASI TENA KATIKA NCHI HII MTU KUONGOZA/KUTAWALA APENDAVYO katika wakati huu wa mabadiliko makubwa DUNIANI ya MAENDELEO YA MAWASILIANO . . .

Hujui chochote wewe,UNAFIKIRI nchi ni KUKAA KUJADILI Vijiweni!!Uganda Museveni ni mwaka wa 32 huu,KAGAME(Third term).NKURUNZINZA(Third term),CUF,NCCR,CHADEMA(Third term).
 
The cost of keeping ccm & Magufuli in power far outweigh the cost of electing UKAWA & Edward Lowassa.
The cost ratio ELUKAWA:MAGUFULICCM is 1:1000000
 
Wana JFNimefatilia kwa muda mrefu kwa kujitambulisha Mimi ni CCM wa kweli. Nawaomba wa CCM pamoja na wa CDM wote tupo katika familia moja pamoja kwenye mitandao hatujuani vizuri ndiyo maana wengine wanaficha sura wengine wanaficha majina. Tutambue ya kwamba mwisho wa siku ni lazima tutakuwa na Rais wa awamu ya tano. Kwa mtazamo wangu na Hali halisi ilivyo lazima atakuwa Kati ya Magufuli au Lowasa. Maana ushindani unaonekana. Tulivyo lelewa katika maadili ya dini zetu hasa za Kikristo na Uisilamu. Wote tunaamini Mwenye uwezo wa Mwisho ni Mungu pekee wa kutupatia kiongozi sisi Kama watoto wa Mungu hatuna sababu ya kufarakana bali tuwe watu wa kukubali. Mimi Kama CCM naomba Mungu apite Magufuri pia najua watu wa Chadema au Uk wanaomba Mungu awe Lowassa. Kila mmoja anayo haki ya kuomba hivyo. Jambo moja ambalo kila mmoja wetu kila mmoja kuheshimu mawazo ya mwingine. Watakao fanikiwa jukumu lao siyo kubeza wengine Bali ni kupongezana kwa ajili ya kujenga taifa letu bila hivyo tutavunja Amani na pia maendeleo ya taifa letu.Kama sisi CCM tutashinda lazima tuwapongeze wenzetu kwa kushiriki uchaguzi na kukubali matokeo. vilevile na sisi tukishindwa tuwapongeze wenzetu kwa ushindi na mwisho wote tuungane kujenga nchi yetu. Tusibaki kuhubiri Amani bila kukubali yatakayo tokea.Tanzania ni ya wote . Nawasihi wana JF tusiwe chimbuko la watu wasio wastaarabu matusi na kejeli ni za watu wahuni.Bila kuficha mimi naitwa Kaizirege Camara sina haja ya kuficha ukweli watanzania Tunahitaji kubwa mfano wa kuigwa tusiwe watu ambao mchana tunaonekana waungwana usiki wahuni. Mwisho viongozi wa Dini wasaidie watu kurudi katika misingi ya dini kwa kuhubiri tabia na habari njema ni zaidi ya Macho yanavyo ona ajuaye kila mmoja ni Mungu pekee.Kwa Mara ya kwanza Mimi huo ndiyo mchango wangu na wote nawatakia mafanikio mema katika mchakato Hutu wa uchaguzi.Nitaonekana tena tarehe 26.10.2015 kwa kupongezana atakaye shinda. Amani iwe kweli.
 
Wengi wetu tunadhani mabadiliko ni smooth process. Maadam tumeamua kufanya mabadiliko na tuyafanye sasa bila kusubiri.
Yanaweza kuwa mabadiliko machungu, lakini pia yanaweza kuwa matamu. Tumeyavulia nguo lazima tuyaoge.
Muhimu ni kwamba mabadiliko haya yanafanyika kwa njia salama ya box la kura. Baada ya miaka mitano Tanzania itakuwa imetengeneza uwanja Sahihiwa ushindani ktk siasa.
 
Back
Top Bottom