Swali la Ugomvi: Kwani Lowassa Kawa Mganga wa Kienyeji?

Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...

mnafikiri tatizo la nchii hii ni louwasa la hasha tatizo langu mimi ni ccm itoke..
Sina haja ya kukupa sababu we angalia tu stage tuliuo kuwa nayo 1980 na sasa
 
Umeandika utumbo mreeeeeeeef kama wa kuku hauna ladha yoyote.

Uandishi kama huu kuna wenyewe wa kuandika na wakaupatia inakera hata kusoma haina hata nakshi.

Kazi kama hizi za kuandika articles ndeeeeeeeeefu na zikaweza kuvutia mtaalam ni lara 1

Nenda MMU ukafundwe Mzee Mwanakijiji ustuletee mambo yako ya kijijini hii town #MAZAFANTAAAAAAA WEEEE !!.
 
Last edited by a moderator:
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Inawezekana katuloga ehee huyu mzee mamvi hila me nmeshtuka
 
Mzee Mwanakijiji, with all due
respect, naheshimu mchango wako.

Niliwahi kusema humu, hakuna ubishi kuwa Magufuli is good!, lakini tatizo ni CCM. Kitendo cha wewe kuendelea kumpinga Lowassa bila kuwaeleza wafuasi wako wamchague nani, kunatafsiriwa ni kuipigia kampeni CCM kwa mlango wa nyuma!.

Kama Lowassa hafai, then nani?!.

Ili tukuelewa, sema basi na Magufuli hafai, hivyo sasa wewe msimamo wako ni kwa Chifu Lutalosa Yemba wa Chama cha ADC. Machmillan Lyimo wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Fahmi Dovutwa wa Chama cha UPDP, Janken Kasambala wa NRA, Hashim Rungwe wa Chauma au Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo?.

Kwa vile lengo letu ni kwanza ni kuitoa CCM madarakani, na kwa hali ilivyo, Dr. Slaa wako hakuwa na uwezo huo, mwenye uwezo huo ni Lowassa, hivyo wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii, despite all the odds, watamsupport Lowassa, na wale wengine ambao hawakubaliani na ujio wa Lowassa, ili kutowakatisha tamaa, wameamua kujinyamazia, sasa wewe ambaye umeisha tuaminisha sana kuwa CCM haifai, what are you really doing now at this dying moments?.

Niliwahi kusema humu, kama Lowassa ni mpango wa Mungu, then tarehe 25 October, Mungu ndiye atakayemuingiza Lowassa ikulu!, alilolipanga Mungu, binadamu hawezi kulipangua!.

Kwa waliomdhania Mzee Mwanakijiji,ni Mwenzetu, kasomeni nyuzi hizi.

Kwenye msafara wa Mamba, na Kenge wapo!- It is Either with Us or ...

Malaika akijiunga na mashetani, anageuka shetani?,

Nani hatari zaidi kati ya malaika aliyegeuka shetani, Au

Mzee Mwanakijiji, Tafadhali...! - Jamii Forums

Mzee Mwanakijiji, wengi tunakushangaa! -

Mzee Mwanakijiji utakonda sana si kwa sababu una presha

Naomba kukiri wazi, kwa ratings zangu za jf, Mzee Mwanakijiji ndio mwana jf maarufu kuliko mwanajf mwingine yoyote, kuna wengi wengi wamejiunga kwa sababu yake, tena sisi wengine tulikuwa hadi tunalipia kusoma baadhi ya mada zake na mimi ni miongoni mwa niliomshauri invicible tulipie hadi 50,000 kwa mada!, huyo ndiye aliyekuwa Mwanakijji wa enzi hizo, lakini huyu Mwanakijiji huyu mpiga debe wa CCM..akija kuleta tena mada ya kuuza kweli kuna mtu atalipia?!.

kiukweli inauma!.

Paskali

Akishindwa kuitoa madarakani itakaa madarakani milele?
 
Mzee mwenzangu naomba uje na uzi mwingine mzuuri kama "huu" ila sasa huu mwingine utueleze na madhaifu au mazuri ya Wagombea wengine. Nadhani huyu sasa tumemuelewa vizuri na tunakushukuru sana. Nitapenda ufanye hilo kwajili ya maisha ya baadae ya Tanzania. Lowasa imetosha mkuu. Asante sana

Hao wengine hatawazungumzia kwa sasa kwani wako kambi moja.
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Jamaa anatia aibu sanaa
 
Attachments

  • 1443599453206.jpg
    1443599453206.jpg
    26.2 KB · Views: 116
Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa "ulipo tupo!"! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe "mabadiliko" na kuwa "mabadiliko" ni yeye na unakosa jibu zaidi ya "Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu"; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya "nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!"

Andiko refu co[SUB]2[/SUB] .Mwaka 2015 baadhi ya waandishi waliambulia ukuu wa wilaya.na wewe tafuta.
Nini kwa nini kila andiko lako ni Legwanani?wewe tu ndio unayejua kuchagua kiongozi bora wengine hatujui?
Hata akishindwa japo sio rahisi hatakuwa wa kwanza wala wa mwisho kushindwa.
Huyu unaye mpigia chepuo yeye ni malaika?

Humu kila siku unaandikwa kuwa hizi ni zama za mabadiliko[kurudisha katiba ya wananchi] wewe uko tanzania au ulaya?

Mwanakijiji Economic Hit Men mwenye kutumia ujuzi wake kuwatumikia Wazungu anafikiri sisi sote ni wehu mazuzu hatujui kinachoendelea.... Kilio chako cha muda mrefu umeshindwa kutueleza UFISADI wa Lowassa! Umejaribu ku spin kuwa Hana Uwezo lakini miaka yake 2 tu as a PM ameweza kudeliver kuliko wengine wote! ... Mwanakijiji Unajidhalilisha tu ... Fuatilia Uzi Wangu nitakao uanzisha soon ili upate kujua kwanini Tuna Mtaka Lowassa na si mwingine ... Uvatican usikutie Upofu .. tuko wengi tunaojua Game lenu ...
 
Lowassa hajaja CHADEMA ili kuwa mpinzani bali amekuja ili kuchukua dola na kuwa mtawala.
Hahitaji kuwa na uzoefu wa upinzani wakati na kuja kufanya kazi ya utawala!
 
Hivi kumbe kuna watu zero kiasi hiki. Hawatambui kuwa watanzania ambao hawanufaiki na wizi wa ccm wanatapatapa hali mbaya ndo maana wananatafuta pa kujishikiza kuondokana na mkoloni mweusi wa ccm muasisi wa matusi na kejeli za wapinzani mbele ya watu wenye akili timamu na kuwanyonya wananchi haki zao kama kunguni haiwezekani kuwa wafungwa kwenye nchi yetu najua kwa uchafu huu ipo siku. Mfano: vyoo matundu nane yamejengwa kwa msaada wa crdb bank mkoani dodom makulu kwa milion 25 tu je? Bilioni 325 zilizoibwa ni sawa na matundu ya vyo mangapi kwa shu le ngapi? Kama sio shule za mikoa kumi. Huo ni wizi wa mara moja je? Tukiongeza richmond, epa, melemeta na doans na nk. Acha ujinga leo ccm hawataki katiba inayesa viongozi wabadhilifu wachunguzwe mali zao kama za halali kama sivyo wafilisiwe. Awe lowasa awe anna mgwira kupitia katiba tutawanyoosha sio ccm waliokumbatia katiba inayowalea viongozi ambayo ndo inayopendekezwa. Watanzani ifike mahali acha ushabiki pembeni chagua viongozi wenye mifumo mizuri ya kikatiba utawala wa kisheria. Hamjifunzi kwenye mataifa makubwa. Nenda na madawa ya kulevya china, sinzia bungeni korea, fanya ufisadi malysia, chelewa kuripoti kazini marekani na mengine mengi lakini tanzania ripoti saa tatu na nusu koti linatundikwa hakuna shida tumekuwa watani kupita kiasi
 
Siyo jambo la kujisifia; mnafikiri nchi za wenzenu zimejengwa na watu wenye kusoma mstari mmoja? Labda ndio maana mgombea fulani hazungumzi sana kwa sababu akizungumza sana anaweza akawapoteza watu bure...
Ni vigumu kusoma pumba za ccm muda mrefu.Safari hii miafrika haidanganyiki na miafrika inaoishi ulaya
 
we mwanakijiji mshumbusi tumeishakudharau, alishindwa mmeo dokta mihogo utakuwa wewe?
 
Mzee Mwanakijiji tumekuchoka!Why Lowassa?
Kila siku unakuja na hoja za kumponda tu.
Magufuli yeye ni malaika hana mabaya ya kusemwa?
Au sababu Lowassa kamnyang'anya tonge mdomoni swahiba wako Slaa?
Hizi chuki dhidi yake zimezidi!
Lakini kumuongelea kwako kila siku kunaonesha ni jinsi gani anakunyima usingizi......
Naam,huyo ndiye Lowassa.

Kumbuka tupo vitani.
 
mganga.jpg

KWANI LOWASSA KAWA MGANGA WA KIENYEJI?
Na. M. M. Mwanakijiji

Jamii nyingi za Kiafrika (na inawezekana sehemu nyingine duniani) zina hofu kubwa ya watu ambao wanaaminiwa kuwa wana uwezo fulani hivi ama wa kudhuru watu au kuponya watu. Watu hawa wamepewa majina mbalimbali kutegemeana na kabila au mila na desturi za mahali; wanajulikana kwa majina mengi lakini kwa ujumla wao tunawatambua kama “waganga wa kienyeji”.

Waganga hawa wanatofautishwa vile vile; wapo wale ambao kazi yao kubwa ni kutibu kwa kutumia miti shamba na hawa hujulikana kama waganga wa tiba za “asili” na hawa hutumia zaidi madawa yatokanayo na miti na mimea (na hata wanyama) kujaribu kutibu wagonjwa wao. Kundi jingine ni la wale ambao hutumia siyo tu madawa mbalimbali bali pia hutumia “kunuia”; yaani wanaaminiwa wana uwezo wa kutoa maneno (sala, dua, maapizo n.k) ambayo yanachangia katika kuleta tiba kwa mtu au kumuondolea mtu matatizo yake. Hawa hujulikana zaidi kama waaguzi (seers); na katika kundi hili wapo wasoma nyota, viganja, alama za sayari, wenye kutumia vitabu vya kidini n.k
Katika hilo hilo kundi la pili wapo ambao pia huaminiwa kuwa siyo tu wana uwezo wa kutibu au kumuondolea mtu matatizo yake bali pia wanaweza (wakiamua kunuia) kumdhuru mtu na kumfanya mtu limfikie jambo baya. Kundi hili ni kundi la waganga wanaoogopwa sana kwani hawa ndio hujulikana katika lugha za wenzetu kuwa wanafanya “black magic” yaani wana uwezo wa kudhuru watu na wanapofanya hivyo basi tunawaita ni “wachawi”. Wachawi hasa ni kundi la mbali zaidi ambalo wao hawajishughulishi na tiba bali katika kudhuru watu (wawe na sababu au bila sababu). Wapo waganga ambao wanaanzia upande mmoja na mwisho wanaweza kujikuta upande mwingine kabisa.

Hata hivyo, watu wengi katika bara letu, nchini mwetu na hata sehemu nyingine duniani huwaendea zaidi wale waganga wenye kuonekana wana uwezo wa kutibu hasa wenye kuchanganya miti ya asili (mitishamba) na namna fulani ya kunuia. Waganga hawa wengine wakitumia mbinu za kimazingaombwe (viinimacho) wanaweza kabisa kuwaaminisha watu kuwa vitu fulani vipi au havipo na wanaweza kufanya vitokee au visitokee na hivyo kujijengea imani hasa. Na watu wa namna hii huogopwa sana hasa kwa vile inaaminika wana “uwezo fulani”. Karibu jamii zote duniani zimewahi kuwa na watu wa namna hii.

Katika nchi yetu hata hivyo, imani hii kwa waganga wa kienyeji inatokana na imani za kishirikina zaidi (superstitious beliefs). Tunaogopa vitu fulani fulani, tunaamini vitu fulani fulani, na wakati mwingine hata kuwafuata watu kwa sababu ya imani hizi hizi. Mtu akitaka kumtishia mtu mwingine basi anamwekea “hirizi” kwenye mlango wa ofisi yake na mtu huyo akiikuta anaweza kutahamaki kuwa wanataka kumroga (na anaweza kuwa ni msomi na PhD juu yake) lakini mara moja ataahirisha kwenda kazini siku hiyo na yeye aende “Bagamoyo” kwenda kutafuta Kinga. Na kama “Bagamoyo” alikokwenda hakuji na majibu ya kutosha basi anaweza kuamua kwenda “Sumbawanga”. “Sumbawanga” hiyo ikikataa basi anaweza akaamini waganga wakali zaidi wako “Tanga” na hivyo atatafuta safari ya kwenda Tanga! Maisha ya mtu huyo utaona mara moja yanazidi kuzama katika imani hizi kiasi kwamba hata dini kama alikuwa nayo inapotelea mbali au anachanganyia “mumo kwa mumo”.

Katika matatizo yote ya wananchi wenye kunufaika ni hawa waganga wa kienyeji hasa wale wenye majina ya kutisha zaidi na ambao sifa zao zimetangaa nchi nzima. Wapo – kwa mujibu wa vyanzo vingi – waganga ambao wanafanya “house calls”; yaani, hawa ni waganga ambao huweza kualikwa na kwenda kufanya huduma kwenye nyumba za watu hasa kama mtu mwenyewe hawezi kwenda kwa mganga huyo akaonekana. Wapo watu mashuhuri ambao hutembelewa na wengine wanao waganga wao ambao wako kwenye malipo yao!

Ukiangalia sana siasa zetu za mwaka huu ni lazima mtu ujiulize kama watu wanaomshabikia Lowassa wanafanya hivyo kwa vile wanamuamini au wanaamini katika uwezo wake? Nimeshangaa sana kuwa hata baadhi ya watu ambao wanakubali kabisa kiakili kuwa Lowassa hafai kuwa Rais lakini na wao wamejipanga mstari kusema “tutampa tu” ilimradi asionekane kumpinga! Wengine ambao kwa hakika unaweza kuamini walikuwa ni watu wa misimamo lakini na wao wamegeuka na kuwa “watu” wa Lowassa. Unajiuliza imewezekana vipi?
Ukiangalia hata watu wengine wanavyomshabikia ni kana kwamba wameamua kuegesha akili zao mahali wenyewe wakaamua kutembea kwa miguu!

Imenifanya nijiulize kama watu wanamuangalia Lowassa kama mganga wa kienyeji hivi? Unajua kabisa kuwa unachoamini hakiingii akilini lakini bado mtu anaenda kuvaa hirizi kubwa imeandikwa “ulipo tupo!”! Unajiuliza vipi watu waamini mtu ambaye hajawahi kuwa na imani ya upinzani wala kuonekana kuwa anaelewa unachosimamia leo yeye ndiyo awe “mabadiliko” na kuwa “mabadiliko” ni yeye na unakosa jibu zaidi ya “Hamtuambii chochote Lowassa nitampa kura yangu”; kama watu walioamua kupeleka kuku, mbuzi na hela zao kwa masangoma wakiamini kabisa kuwa majibu yatakuwa wanavyofikiria! Unajiuliza inakuwaje watu wanaruka ruka na kushangilia kabisa kwa imani hupati majibu zaidi ya “nyie mko nje ya nchi, tuachienie mganga wetu!”

Mwisho wa siku unagundua kuwa imani za kishirikina ni imani zenye nguvu sana kwa wenye kuziamini. Mtu anaweza asile, anaweza kufanya mambo ambayo angekuwa na akili nyingine asingefanya! Mtu mzima kavaa suti kumbe begani kuna hirizi kama simu ya iphone6 inaning’inia! Binti mzuri kabisa na kapendeza kabisa na amesoma na anajiita msomi (anafanya Masters yake mwenyewe tena ya Fizikia) lakini kiunoni kwenye makutano ya shanga kuna pande la hirizi limezunguka na chale zilizofichika!

Ubaya wa imani hizi ni kuwa hazimruhusu mtu kutumia akili yake kufikiri kwa sababu akiamua kufikiri anaweza asiendelee kuamini. Kwa mfano, kama mganga wa kienyeji anauwezo wa kumfanya mtu awe tajiri kwanini yeye mwenyewe maskini? Mtu mwenye imani hizi haruhusu maswali katika kichwa chake na mtu yeyote atakayejaribu kumfanya ajiulize maswali au kumuonesha upotofu wa hiyo imani ataonekana mara moja ni adui yake nambari moja na hachelewi kumtukana, kumfukuza au kumsemelea kwa huyo mganga! Huu ndio ubaya wa imani za kishirikina na kinachosikitisha ni kuwa Tanzania tunatajwa kuwa ni nchi inayoongoza kwa imani hizi (kwa mujibu wa Pew Research). Ati asilimia 93 ya Watanzania wanaamini katika uchawi! (hizi 'nyomi hizi!)

Uzuri ni kuwa imani hizi huwa zinaisha! Wakati mwingine kwa njia ya kawaida lakini wakati mwingine kwa kulazimishwa. Zinakwisha kwa sababu hatimaye watu wanafunguka na kuachana na imani hizi na kuona makosa ya njia zao (errors of their ways) na kuamua kurudi kwenye njia sahihi. Mashabiki wengi wa Lowassa hasa wale WanaCHADEMA walioingizwa mkenge huu wa kihistoria nab ado wanajitambua wataanza kuamka na kufunguka. Siku hizi chache zilizobakia tutawaona watu wale wale ambao walimshangilia Lowassa wakianza kumtupa mikono na kumuachia chama kilichokuwa compromised. Lowassa na kundi lake itabidi watumie mbinu nyingine za kujaribu kujijengea ujiko mwingine ili kutishia watu waweze kuamini katika uwezo wao.

Ndivyo ilivyo kwa waganga wote; ili upate wateja ni lazima uje na mbinu za kutishia zaidi au kufanya mambo ambayo watu itabidi waamini kuwa ndiyvyo ilivyo. Wapo watakaoamini na wapo amba wataendelea kuhoji na kukataa hata kama kwa kufanya hivyo watakuwa wamejipotezea marafiki; hasa marafiki ambao wameamua kuamini katika geresha hii ya kihistoria.

Hata hivyo, kwa vile hawa ni ndugu zetu hatutawateta au kuwasema vibaya; tunajua kuwa Oktoba 25 wakati Lowassa na agenda yake ya kuutaka Urais (ndiyo ajenda pekee aliyonayo) itakapokataliwa na WAtanzania ndugu zetu watarudi na kutambua walivyopotea – wengine watasema “walipotoshwa” na kuona kile ambacho wengine tumekiona mapema na kwa miaka sasa – Lowassa siyo tu hafai lakini ni miongoni mwa viongozi wabovu kabisa kupata kutokea katika nchi yetu.

Ni kama mganga wa kienyeji fulani hivi ambaye watu wamemuamini sana lakini mwisho wa siku wakatambua tu. Uganga ni dili tu; haihusiani kabisa na kutaka kutibu maisha ya watu.

MMM

Mzee MMM unapoteza muda wako.kisichohitajika hapa ni CCM kwa namna yeyote.leo hii Magufuli akihamia UKAWA na Lowassa kwenda CCM hata kwa muda huu tu uliobaki kabla ya uchaguzi then Magufuli atashinda kupitia UKAWA na Lowassa atachemka.Sina wasiwasi na utendaji wa Magufuli hata kidogo kama ilivyo ila chama anachokitetea na mifumo yake ndio imechokwa sana sana sana na kila mtanzania mwenye uchungu na nchi hii
 
Mwanakijiji naona sasa unapoelekea sipo. Kuondoka kwa Slaa imekuchanganya sana. Wewe Tulia na mapenzi yako waache wenye mapenzi na Lowassa wamshangilie. Uwezi jua anaweza kuwa kiongozi bora kuliko hao unaowapenda na unaowaona sasa. Mwanakijiji wewe sio mungu ujui ya kesho
 
Mzee Mwanakijiji, Tanzania hii kila mtu anayo haki na uhuru wa kuamua mambo yake bila kuingiliwa, mradi havunji katiba, sheria wala kanuni za nchi. Katika masuala ya siasa na uchaguzi kila mtu anaweza kuelekea upande wowote. wapo ambao ni bendera kufuata upepo na wapo ambao wameamua kwa uthabiti kuwa upande fulani kwa ubaya au kwa uzuri. hata wewe unazo sababu za kuwa uoande wa Magufuli kwa sasa, hata kama haukuwa upande wa Kikwete zamani (or am I imagining this?). Hakuna mtu mwenye haki ya kumhoji mwenzake kwa nini ameamua kuwa upande fulani. kama akitaka kukujibu utakapomwuliza anaweza, lakini hakuna lazima kufanya hivyo. sababu ni za mtu binafsi na anazijua mwenyewe. Kama akitaka kuwashirikisha wenzake kwa nia ya kuchochea uungwaji mkono, atafanya hivyo, lakini hatakiwi kufanya hivyo kwa mtizamo wa kujitetea tu ili akina MMM wasimwone kapotea!

Wapo watu ambao wanaona CCM imeshachoka. wana sababu zao za kuamini hivyo. Na kwa imani yao hiyo, kuchoka kwa CCM ni sababu MOJA INAYOJITOSHELEZA. Tatizo ni kwamba ukiambiwa na huyo unayemwuliza kwamba atapiga kura dhidi ya CCM kwa kuwa anaamini imechoka na hataki kuiona ikirejea madarakani awamu ijayo, wewe hutaki kuikubali kama sababu ya msingi. Nina hakika wengine watafanya maamuzi kwa kuzingatia hilo tu.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania Now Hawana Haja Ya Kusikia Kinaongelewa Nini!! Maana Tumeshaambiwa Na Kusikia Maneno Mengi Mno Na AHADI Nzuri Saaana Kama Za MAISHA Bora Kwa Kila Mtanzania, Mabilioni Ya Kikwete, Tukaambiwa Tuunde Vikundi Vya Vijana Na Akina Mama Tukaombe Mikopo, MATOKEO Yake Mabilioni YALE Wajanja Wameyapiga Yote!! Tumeishia HAPO!! Na Sasa Magufuli ANAKUJA Na AHADI Lukuki Ambazo Hazitekelezeki Hata Kwa Miaka 50 Mingine!! Sasa Watanzania Hatutaki Tena Kusikia UONGO Wao!! Eti SERIKALI Yake Itajenga Viwanda Vikubwa, Vya Kati Na Vidogo Nchi Nzima, Ili Vijana WAPATE Ajira!! Kila Kijiji Kinatajengewa Zahanati, Kila Kata Kituo Cha Afya,Kila Wilaya Hospital Yenye Hadhi Ya Wilaya Na Kila Mkoa Hospital Ya Rufaa!! Tena Zikiwa Na Dawa, Vifaa Tiba, Waganga Na Wauuguzi!! Kila Kijiji Million 50 Na Kila Kata Million 150!! KAMA CCM Ilishindwa Kuliendesha Shirika Lake La SUKITA Na Kuliua!! Itawezaje Kujenga, Kuanzisha Mashirika Ya Umma Au Kuyafufua!!?? Kwa SERA Na ITIKADI Zipi, Za UJAMAA Au UBEPARI!!! Kama SERIKALI Iko Ktk. SERA Za Soko Huria, Zenye KUACHA Njia Kuu Za Uchumi Mikononi Mwa Sekta BINAFSI!! Na SERIKALI Kazi Yake Ni Kuweka Mazingira Bora Ya Uwekezaji Kwa Kuweka Miundombinu Mizuri!! Na Kusimamia Sheria Na KUKUSANYA Kodi!!! Sasa HIVYO Viwanda Vya Magufuli Nchi Nchi Ni Vipi!!!?? Au KUTAKA Kuwapora Wale Waliouziwa Na Kuuza Upya!!!?? Je, Hao Wawekezaji Tunaowaomba WAJE Kuwekeza Watakuja!!! Ndorooobai!!!! @ Paul Alex Hii NDIO Sababu Hatutaki Kusikia Porojo TENA!! Tunaenda Kutazama Show Tu Za DIAMOND, COMEDY YA MPOKI, YAMOTO BAND, CHEGE & TEMBA NA PUSH UP!! Maamuzi Tunayajua Wenyewe 25 Oct.
 
Back
Top Bottom