Swali la Ugomvi: CCM ni kama nini?

Swali la Ugomvi: CCM ni kama nini?

Sijui wewe mwenzangu unaifananisha na nini CCM katika mawazo yako. Kwa uzuri au kwa ubaya!​
Kwa vile Tanu ndie baba wa CCM, na Tanu ndicho kilichotupatia ukombozi, then like father like son, CCM ni chama cha ukombozi wa Watanzania.

Wengine wetu kama sisi tunakifananisha na mkombozi, muokozi!.

NB. Huku kuendelea kueneza chuki dhidi ya CCM kwa njia ya kuivoke ridicules, its not gonna add up the votes come 2015!, CCM itarudishwa kwa sympathetic votes kuwa ilitukanwa sana!.

Pamoja na CCM kuwa ndie chama mwokozi wetu, bado hajaweza kutufikisha kwenye ile nchi ya ahadi!. Kufuatia hali hii, watu sasa wanaijengea chuki CCM na kuifanya ionekane kama ni li zimwi!. Kwa kuwa hakuna mwingine as of now aliyeonyesha uwezo wa kutufikisha, then 2015, kuna hatari ya kuendelea kulichagua hili hili li zimwi CCM maana ndilo likujualo!

Pasco.
 
sisiem mm nafananisha na govi umefika muda wa kuliondoa kwa sasa lina madhara mengi!
 
Mi nakifananisha na kunguru,,,yani ccm haifugikiiiiii
 
Mimi nipo taofauti sana na watu wengi humu.ccm mi naifananisha na raia anayetaka kuonekana askari(aliyepiga picha na lema).
jina chama cha mapinduzi ni jina zuri lakini mapinduzi ni kazi,ni cheo na ni harakati.ni tofauti na kujiita chama cha wananchi.
ccm ni muunganiko wa tanu na asp,mapinduzi ya znz hayakufanywa na ccm kwa maana hiyo ni sawa na mtu kujiita kanali wa jeshi kisa mama yake alikuwa na cheo hicho.
kichekesho ni pale anapo kutana na wanajeshi wa ukweli wakati wenzake wanatembea kikakamavu yeye anadunda,wakati wenzake wakivaa kama wanajeshi yeye nguo za jeshi amevaa mlegezo.wakati wenzake wakifuata protokali za kijeshi kusalimiana yeye ni saluti kwa kila anayemwona ndani ya gwanda hata wakati mwingine saluti kwa mikono miwili.
kichekesho nipale anapojipandisha cheo na kujihamisha.
mifano ya haya ni mambo yaliyofanyika toka kuzaliwa kwa chama,miradi mingapi imekufa?mapinduzi yamefanyika sukita,viwanda,reli,bandari,atc,mashamba,nbc,mahoteli ya umma,usafiri wa umma,madini,shule na vyuo vya umma.
 
Kwa vile Tanu ndie baba wa CCM, na Tanu ndicho kilichotupatia ukombozi, then like father like son, CCM ni chama cha ukombozi wa Watanzania.

Wengine wetu kama sisi tunakifananisha na mkombozi, muokozi!.

NB. Huku kuendelea kueneza chuki dhidi ya CCM kwa njia ya kuivoke ridicules, its not gonna add up the votes come 2015!, CCM itarudishwa kwa sympathetic votes kuwa ilitukanwa sana!.

Pamoja na CCM kuwa ndie chama mwokozi wetu, bado hajaweza kutufikisha kwenye ile nchi ya ahadi!. Kufuatia hali hii, watu sasa wanaijengea chuki CCM na kuifanya ionekane kama ni li zimwi!. Kwa kuwa hakuna mwingine as of now aliyeonyesha uwezo wa kutufikisha, then 2015, kuna hatari ya kuendelea kulichagua hili hili li zimwi CCM maana ndilo likujualo!

Pasco.
Kwanza, CCM haikutanguliwa na TANU pekee bali ilitanguliwa na TANU na ASP, vyama viwili vilivyokuwa na sera na malengo tofauti kabisa.

Zaidi ya yote, CCM ya wakati huo haiwezi kuwa sawasawa na CCM ya sasa kwa kuwa waanzilishi wa CCM wa wakati ule walikuwa na focus zao tofauti na zile za wanaoiongoza CCM hivi sasa? Hata CHADEMA ya Mtei si sawa na CHADEMA ya Mbowe, hilo hata wewe unalijua. Ni kwa vipi unarahisisha namna hiyo kusema kwamba CCM ni chama cha ukombozi ilihali unajua shughuli ya ukombozi na malengo ya Ukombozi ya TANU yalishakamilika kabla ya CCM kuzaliwa?

CCM ilikuja kumkomboa nani ilihali kazi ya ukombozi kutoka katika utawala wa kisultani na ule wa kikoloni ilikuwa imefanywa na TANU na ASP? CCM ni chama cha ukombozi dhidi ya nini? ilihali ndicho kilichoshika madaraka? Ungesema vyama vya upinzani ni vyama vya ukombozi ningekuelewa, kwa maana ya kwamba vyama vya upinzani vinatukomboa kutoka kwenye utawala dhalimu na wa kifisadi wa CCM.

Hivi sasa kila idara inanuka rushwa, kila sector (public sector) ina substandard services, bado unaiita CCM chama cha ukombozi. VIongozi wachache wanagawana rasilimali za nchi na kuwakandamiza mamilioni ya watanzania maskini, bado unakiita CCM chama cha ukombozi? You disappointed me Pasco! Ninavyokufahamu na ulivyoandika hapa ni tofauti kabisa.
 
Hao Ndg yangu utaifakwanza hawapo kwenye CCM umebaki na mafisadi kina Rostam, EL,& CO kama ulikuwa hujui kimbia unamezwa na majoka CCM..!!
 
Last edited by a moderator:
chama cha machuma ulete,yanakula %99 ya kile tulichoachiwa na mwalimu ili kitukomboe yanatuachia %1 itupake mafuta kwa mgongo wa chupa
 
You disappointed me Pasco! Ninavyokufahamu na ulivyoandika hapa ni tofauti kabisa.
Mkuu Lukolo, pole for disappointment, kama ulivyonifahamu, ni tofauti na sasa, then ulidhani unanifahamu, nikimaanisha hunifahamu!.

Nakiri moja ya madhaifu yangu ni kuwa mkweli too much!. Nimeifananisha CCM na zimwi, ambayo baada ya miaka 50 bado haijaweza kutufikisha nchi ya` ahadi zaidi ya kuendelea kututafuna!.

Ukweli mchungu ni kuwa, kuelekea 2015, as of now, bado hakuna mbadala wa CCM!, japo Chadema angalau inaonyesha dalili, lakini bado!. Kwa vile uchaguzi mwingine ni 2015, ukweli mchungu ninausemea hapa, ambao ndio umeku disappoint ni hii fact kuwa japo CCM ni li zimwi, 2015 ni zimwi hili hili!.

Calling CCM names, gonna change nothing kwa matokeo ya 2015!. Tusiichukie CCM!, akitokea mbadala tuiondoe CCM kwa upendo kwa shangwe na mapambio na sio kuijengea chuki, ili tuiondoe kwa hasira, itaumia kwa kinyongo, na matokeo yake sio mazuri!.

Kilichonidisappoint mimi si huo mtazamo wako wa CCM kuwa Zimwi lisilotaka kuachia ngazi, bali ni mtizamo wako wa kwamba CCM ni chama cha ukombozi ilihali kwa ushahidi wa wazi usio na shaka CCM inaonyesha dhahiri dhalili kwamba ni chama cha kinyonyaji. Kukiita chama cha ukombozi ni kama kukipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Na kwa mtizamo huo sikuoni kama msema ukweli bali nakuona kuwa ni mnafiki.

Lakini pia hoja ya ama kushinda au kushindwa kwa CCM mwaka 2015, haiifanyi CCM ionekane nzuri. KUshinda au kushindwa kwake kutatokana na level ya uelewa wa watanzania hasa wale wa vijijini ambao tayari CCM ilishawatia upofu kwa kuwanyima haki halali ya elimu na kuhabarishwa. Maskini wale watu wale wa vijijini ambao bado wanaamini kwamba CCM ni chama cha Nyerere, haitakuwa rahisi kuikataa CCM kwa kuwa kwao Nyerere ni mkombozi. Lakini kama wangeujua ukweli kwamba CCM hivi sasa ipo mikononi mwa fisadi Kikwete, katu wasingekubali kuipa CCM kura yao. Kwa hiyo hapa hoja isiwe CCM ina likelihood kubwa kiasi gani ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 bali iwe ni ina sifa gani?

Mwanakijiji keshasema kwamba CCM ni kama mbwa mwitu aliyejifanya bibi. Na ndivyo ambavyo CCM imekuwa ikifanya ikifika huko vijijini ambako huwa inajifanya bibi mwenye nia ya kuwaokoa, lakini ikishakubalika inawatafuna.
 
Mkuu Lukolo, kusema maji yamejaa nusu glasi, au yamepungua nusu, wote wako sawa!. Japo tunatofautiana kuhusu CCM, ila kwa matokeo ya 2015 hatutofautiani sana.
Pasco.
 
Mi naifananisha na mtetea hata ummwagi mchele sakafuni bado atauchakura tu, hawezi kula tu ashibe.
 
CCM huiwezi ifananisha na chochote labda kuzimu waliowahi fika huko wanaweza elezea!!
 
Utter rubbish, that's how I've seen and judged CCM!

Kuna mabingwa wa kukariri hapa naona wamekuja na hadithi zilizo katika makaratasi yenye wino mweusi na kuyahuisha kwa mihemko kuwa ni kitu halisi. Kwa taarifa tu (nimewahi kufanya homework yangu ktk hili), hayo maandishi hayajawahi kutekelezwa hata kwa 40% toka CCM izaliwe; ila kwa sababu ya kiwango cha elimu cha umma wa Watanzania walio wengi hakikuwa zaidi ya wastani (average) na pamoja na mashine ya propaganda ya CCM ikafanywa ionekane ilivyoonekana lakini zaidi ya hapo kuna matobo mengi na nyufa kibao throughout their miserable span.

Ukiondoa miaka michache baada ya kuundwa kwake hasa kati 1977-1982, CCM hakikuwa tena kuwa relevant kwa Tanzania wala wananchi wake. Na ndio maana hawakuwahi kujiamini. Baadhi yetu tunakumbuka vema namna wakati ule mfumo wa vyama uliporudishwa tena MWAKA 1992, jinsi CCM ilivyohaha kuvihujumu vyama "vipya tena vichanga vya siasa" kwa njia nyingi ikiwemo TISS, Mahakama, TRA, ufisadi (hongo na rushwa hasa nyakati za chaguzi), hodhi ya mali ya umma kama majengo, viwanja nk.

Swali mtambuka ni kwa nini kama CCM walikuwa wazuri, kama walikuwa wanapendwa kama ilivyokuwa inakuzwa je nini chanzo cha hofu yao ile? Na leo wana hofu kubwa zaidi kuliko wakati wowote wa historia yao hafifu. Kwa nini?

Nijuavyo mimi, CCM walikwishapoteza relevance zamani sana, toka awamu ya mwisho wa Mwl Nyerere. Ikapoteza political legitimacy wakati wa Mzee Mwinyi na kisha ikawa genge la wahuni, mafisadi na wauawaji wakati awamu ya tatu na nne.

So, very politely I hereby wish to challenge Pasco and anyone to provide evidences to the contrary.
 
Back
Top Bottom