Swali la kizushi

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,539
21,567
Wewe ni muuzaji wa duka, mteja anakuja na shilingi elfu Kumi (10,000/-) feki anataka Mkate wa shilingi 2,000/- ...wewe bila kujua unaipokea lakini unagundua hauna change ya kumpa mteja unaamua kuomba change kwa jirani yako na hiyo hiyo 10,000 feki kisha unamrudishia mteja shilingi elfu nane (8,000/-) na mkate, baadae jirani anakuja kukuambia ile pesa uliyompa ni feki unaamua kuichukua na kumpa shilingi 10,000/- halali. Je, utakuwa umepata hasara ya shilingi ngapi?
A. 12,000

B. 18,000

C. 10,000

D. 20,000

E. 8,000

F. 2,000
 
D. 20,000/=

ulimpa mteja mkate (2,000/=) + chenji (8,000/=)
wewe ukabakiwa na 10,000/= feki (ambayo ina thamani ya 0/=), yaani ni sawa na hajakulipa chochote
Jumla umeshapoteza 10,000/= bila kupata chochote

Bado ulitoa tena 10,000/= halali ukarudishiwa 10,000/=feki toka kule ulipoomba chenji.
Unapoteza 10,000/= nyingine tena

Jumla 20,000/=


 
E
kuomba chenji bado nikapewa elfu 10 halali
nimerudisha chenji halali elfu 8
yule karudisha feki nimempa elfu 10 halali
nimepoteza elfu 8 na mkate wa elfu 2.

apana chezea switi mangi...im very experienced.
 
Hasara ya 10,000 tu, hela isingekuwa feki usingepata hasara yoyote, imekuwa feki basi hasara uliyopata ni ya mkate na 8,000 aliyompa
 
D. 20,000 mkate uliompa sh 2000 na chenji uliompa sh 8000=10,000 na 10,uliompa jirani
 
E
kuomba chenji bado nikapewa elfu 10 halali
nimerudisha chenji halali elfu 8
yule karudisha feki nimempa elfu 10 halali
nimepoteza elfu 8 na mkate wa elfu 2.

apana chezea switi mangi...im very experienced.

Hasara hapo ni shilingi elfu 8 kwani tayari ulikuwa na elfu 2.
Iko hivi, 10,000 feki ulienda kuomba chenji=hivyo huna hasara
Ukaja na chenji ukamrudishia mnunuzi 8,000 na ukabakiwa na elfu 2.
hivyo hapo bado hukuwa na hasara.
Baada ya muda, ukarudishiwa feki ukatoa orijino. Hivyo hasara hapo ni 10,000
 
ELF 8 YA CHENJI + ELFU 2 YA MKATE+ ELFU KUMI YA JIRAN YAKO = 20,000

JIBU D
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom