Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Ohoooo, yan lait ndo ningekuwa mie nakuambia tu baba mulete tu bimdogo tuendelee kuishi,
 
Ninanukuu maelezo ya mume mtu yaliyotolewa mbele ya mke mwenyewe na mashahidi wengine wengine.


“tumeishi kwenye hii ndoa kwa miaka tisa (9) bila mtoto na sikuwahi kulalamika wala kuuliza chochote coz najua maswala ya watoto ni majaliwa ya Mungu na ishu za kulalamikia watoto ni za kizamani.

Huyu mwenyewe ndiyo alianzisha hayo mambo akaniburuza tukaenda hospitali na baada ya vipimo wote tukaonekana tupo vizuri na tuna uwezo wa kuzaa, tatizo likaja akawa ananilaumu eti sina shabaha ndo mana siwezi kumpa mimba"


Akaendelea, “ndiyo nikatafuta kabinti ka kawaida kabisa nikachepuka nako ili kupima shabaha yangu maana matusi yalianza kutoka nje ya nyumba kwenda kwa wanandugu na mitaani. Nimekadunga mimba na kamenizalia baby boy hivi karibuni, tatizo ndiyo lipo hapo mi kuzaa nje ya ndoa!”

Mwisho “nasema ni kweli nimezaa nje ya ndoa lakini aliyetaka, siwezi kumlazimisha kuendelea kuishi nami, anaweza kuondoka au kama anataka kuendelea kuishi na mimi its ok, mimii nampenda sana ila lawama za mimi kuzaa nje sizitaki kwa sababu kasababisha yeye mwenyewe na nilimuonya sana hakunielewa, lengo langu lilikuwa ni kumuonyesha tu kuwa nina shabaha ila ninayapenda maisha ya amani ndo mana sikujali hayo ya mtoto sasa mbona mwezie hata miezi mitatu haikupita kapata mimba?”

Swali, kama wewe ndiyo huyo mke utabaki kwenye hiyo ndoa au utaondoka?

Still utakuwa na furaha kama zamani endapo utabaki?


Je, huyu mwanaume kamtendea sawa huyu mwanamke?

Na wewe unauhakika gani uyoo mtoto hujabambikiziwa....
 
Mkuu una uhakika gani na huyo mtoto uliyepata kwa mwanamke wa nje ni wa kwako?
 
inawezekana hatu huyo mtoto aliyezaliwa sio wake asijigambe
 
wangoni utawajuwa tu kwa komenti zao


Mkuu umenifurahisha sana. Hata akijifika kwa feki id bado utawajua tuu, hawa watu ni shida, mpe pesa itafika kama ilivyo, mkeo, kama hatamgegeda basi atashika hata ma.kalio japo kwa bahati mbaya!
 
Hili jambo bana ni gumu sana.

Najiuliza wote kama kweli 'wazima' kwa nini mwanamke asishike Mimba? wy Jamaa alipojaribu nje first attempt mimba ikashika? isije ikawa wananyimana unyumba huko nyumbani??
 
Hili jambo bana ni gumu sana.

Najiuliza wote kama kweli 'wazima' kwa nini mwanamke asishike Mimba? wy Jamaa alipojaribu nje first attempt mimba ikashika? isije ikawa wananyimana unyumba huko nyumbani??

Kaka hata sie tulishangaa sana lakini jamaa alisema wameishi vizuri sana mpaka siku chache zilizopita wife alipogundua jamaa ana kid nje!

Wengi wanadai inawezekana sababu za life style ya siku za nyuma kama aliwahi kudisturb kizazi kwa madawa au kuchoropoa ujauzito!! Hizo ni tetesi yote anayajua Mungu kaka
 
Back
Top Bottom