Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

inawezekana na mwanamke akatoka nje akapata ujauzito.
kuna siku niliulizwa hili swali kwa JF dokta ila sikupata jibu,niliwai kusikia kuna DAMU KUKATAANA.
 
attachment.php
 
One sided story....inawezekana mwanamke pia anaupande wake wa kuelezea. Wengi wanamshtaki mwanamke kwa kua na mdomo mbaya ila ni huyo huyo mwanamke ameishi nae kwa miaka 9. At the end of the day mwanaume kachagua option ya ubabe and guess what, its the woman's fault. Alternative zipo nyingi kila siku watoto wanatupwa au amwache kabla ya kutoka nje ya ndoa. Kilichobaki huyo mwanamke aende tu zake for her own sake and the supposedly new happy family.
 
Duuuuh amsamehe tuuu sababu inaonyesha mumewe anampenda kiukweli sio wote wenye kuwa na uvumilivu namna hiyo nimeona ndoa nyingine zimevunjika kwa kisa hicho bila hata kufikisha miaka mitano sembuse hiyo tisa..kwa mwenzangu hapo amejilipia tuisheni mwenywe na sijui kama atarudia makosa.
 
Ishu si kukosa akili, tatizo ni ushauri!! Siri za ndani kusimulia nje huko masalunini kinachofuata ni ushauri ambao unaigharimu furaha yako!!

Ushaur gani na.yeye kishaharibu au hujui mwanamke mwerevu hujenga nyumba ake mwenyewe na alie mjinga huibomoa kwa mikono yake
 
Mithali 14:1; "Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe."
 
Kukata mzz wafitina mwamke atafute mwenye shabaha na yeye azae...angalizo tafuta litajir koz akijichanganya na mlala hoi alafu ishu ikaja bunguluka badae itakula kwake mwanae ataishia saint kayumba..ndukiiii
 
One sided story....inawezekana mwanamke pia anaupande wake wa kuelezea. Wengi wanamshtaki mwanamke kwa kua na mdomo mbaya ila ni huyo huyo mwanamke ameishi nae kwa miaka 9. At the end of the day mwanaume kachagua option ya ubabe and guess what, its the woman's fault. Alternative zipo nyingi kila siku watoto wanatupwa au amwache kabla ya kutoka nje ya ndoa. Kilichobaki huyo mwanamke aende tu zake for her own sake and the supposedly new happy family.

To be honest, yule mwanamke alikuwa mkali mwanzoni kuwa mumewe kamzalia mtoto nje ya ndoa kamuabisha, kamdhalilisha na mambo mengi mengi!! Mwanaume alipopewa fursa ya kujitetea ndiyo akaeleza hayo na mengineyo na mwisho wa siku mwanamke aliishia kulia saaana na hakuwa na maelezo yoyote ya ziada thus why nikachuma point hiyo tu!! Wonderful enough, diary zilirekodi kila kitu siku mpaka saa! Paligeuka kituko baada ya kutoa midiary mitatu ya miaka tofauti tofauti ambayo pamoja na kuandika mambo yake mengine ila tangu mwanzo wa sakata hili alikuwa anarekodi, so ilikuwa rahisi kwake kukumbuka mengi zaidi (watu wanatumia diary kwa ufanisi jamani)

Jamaa si muongeaji so mwanamke alipokuwa akianzisha zogo ye anakaa kimya au kutekeleza anayotaka mkewe so alikuwa anaugulia moyoni na wengi wanasema watu wa pole ni wabaya sana kwenye maamuzi!! Alichokuja kuamua ndiyo hichoo
 
Ninanukuu maelezo
ya mume mtu yaliyotolewa mbele ya mke mwenyewe na mashahidi wengine
wengine.


“tumeishi kwenye hii ndoa kwa miaka tisa (9) bila mtoto na sikuwahi
kulalamika wala kuuliza chochote coz najua maswala ya watoto ni majaliwa
ya Mungu na ishu za kulalamikia watoto ni za kizamani.

Huyu mwenyewe ndiyo alianzisha hayo mambo akaniburuza tukaenda hospitali
na baada ya vipimo wote tukaonekana tupo vizuri na tuna uwezo wa kuzaa,
tatizo likaja akawa ananilaumu eti sina shabaha ndo mana siwezi kumpa
mimba"


Akaendelea, “ndiyo nikatafuta kabinti ka kawaida kabisa nikachepuka
nako ili kupima shabaha yangu maana matusi yalianza kutoka nje ya nyumba
kwenda kwa wanandugu na mitaani. Nimekadunga mimba na kamenizalia baby
boy hivi karibuni, tatizo ndiyo lipo hapo mi kuzaa nje ya ndoa!”

Mwisho “nasema ni kweli nimezaa nje ya ndoa lakini aliyetaka, siwezi
kumlazimisha kuendelea kuishi nami, anaweza kuondoka au kama anataka
kuendelea kuishi na mimi its ok, mimii nampenda sana ila lawama za mimi
kuzaa nje sizitaki kwa sababu kasababisha yeye mwenyewe na nilimuonya
sana hakunielewa, lengo langu lilikuwa ni kumuonyesha tu kuwa nina
shabaha ila ninayapenda maisha ya amani ndo mana sikujali hayo ya mtoto
sasa mbona mwezie hata miezi mitatu haikupita kapata mimba?”

Swali, kama wewe ndiyo huyo mke utabaki kwenye hiyo ndoa au utaondoka?

Still utakuwa na furaha kama zamani endapo utabaki?


Je, huyu mwanaume kamtendea sawa huyu mwanamke?

namwanamke achepuke aone wenda mbegu zenu haziendan?
 
namwanamke achepuke aone wenda mbegu zenu haziendan?

Siyo zetu, zao!! Walienda hospital wakaambiwa wako poa wanaweza kuzaa!! Sijui kama kuna mengine ya kitaalam zaidi ya hapo ndugu yangu
 
Back
Top Bottom