Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Tatizo mabinti wa siku hizi (si mabinti tu hata wanaume) mna maamuzi ya haraka sana bila kuangalia apnde zingine za maisha!! (Nimekopi kutoka post ya juu but nitaongezea) Maisha ya ndoa hayahitaji visasi maisha ya ndoa hayahitaji ushenzi!! Kuna uvumilivu mkubwa unahitajika katika maisha ya wawili, mimi kama mimi ushauri nilioutoa ni kwamba!! Cha kwanza tumewapatanisha kwa kuwaonyesha wote wana makosa ili iwe ngoma droo!! Cha pili ni wamchukue mtoto, mawasiliano ya mwanaume na upande wa pili yakatiike then baada ya hapo wafanye taratibu za kitaalam ili kuhakikisha na wao wanapata mtoto/watoto wao wa pamoja!!

Kuna kitu kimoja nikwambie, huyu katika miaka kumi na kadhaa waliyokaa ameona (tunaangalia ushahidi) amesalitiwa mara hiyo moja tena kwa nidhamu mpaka yeye kagundua mtoto!! Upo?? Utaachana na huyu mwanaume wa hivi utaenda kuolewa na mwanaume ambaye atakusaliti kila siku huku unaona na dharau juu na watoto lukuki kutoka nje!! Heri nini?? Huyu aliyekukosea mara moja katika umri huo wa ndoa na akakuomba msamaha kwamba haitajitokeza tena ilikuwa ni maamuzi ya hasira kutokana na ulichokianzisha wewe mwenyewe mwanamke au ukaolewe na ambaye hujamkosea lakini vitimbi haviishi!!!?? Kikubwa ni kuangalia kosa limetokea wapi na kusawazisha tu, kutoka nje na wewe ili kulipa kisasi hakutasaidia chochote zaidi kutakuvuruga tu amani

Angalia pande zote mbili kwa kina then rudia tena jibu lako na uamuzi wako!!

No comment you are right mkuu thanks
 
Back
Top Bottom