Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Swali kwenu wanawake wa Jamiiforums

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,458
Ninanukuu maelezo ya mume mtu yaliyotolewa mbele ya mke mwenyewe na mashahidi wengine wengine.


"tumeishi kwenye hii ndoa kwa miaka tisa (9) bila mtoto na sikuwahi kulalamika wala kuuliza chochote coz najua maswala ya watoto ni majaliwa ya Mungu na ishu za kulalamikia watoto ni za kizamani.

Huyu mwenyewe ndiyo alianzisha hayo mambo akaniburuza tukaenda hospitali na baada ya vipimo wote tukaonekana tupo vizuri na tuna uwezo wa kuzaa, tatizo likaja akawa ananilaumu eti sina shabaha ndo mana siwezi kumpa mimba"


Akaendelea, "ndiyo nikatafuta kabinti ka kawaida kabisa nikachepuka nako ili kupima shabaha yangu maana matusi yalianza kutoka nje ya nyumba kwenda kwa wanandugu na mitaani. Nimekadunga mimba na kamenizalia baby boy hivi karibuni, tatizo ndiyo lipo hapo mi kuzaa nje ya ndoa!"

Mwisho "nasema ni kweli nimezaa nje ya ndoa lakini aliyetaka, siwezi kumlazimisha kuendelea kuishi nami, anaweza kuondoka au kama anataka kuendelea kuishi na mimi its ok, mimii nampenda sana ila lawama za mimi kuzaa nje sizitaki kwa sababu kasababisha yeye mwenyewe na nilimuonya sana hakunielewa, lengo langu lilikuwa ni kumuonyesha tu kuwa nina shabaha ila ninayapenda maisha ya amani ndo mana sikujali hayo ya mtoto sasa mbona mwezie hata miezi mitatu haikupita kapata mimba?"

Swali, kama wewe ndiyo huyo mke utabaki kwenye hiyo ndoa au utaondoka?

Still utakuwa na furaha kama zamani endapo utabaki?


Je, huyu mwanaume kamtendea sawa huyu mwanamke?
 
kama ndio mimi huyo mwanamke hapo naenda dukani nanunua kamba .......itaendelea baadae
 
Mwanamke hana akili ukipangiwa kuzaa una zaa tu hayakua majaliwa yake ndo bas tena aheme uamux.n wake aendelee au ahame
 
ntaendelea kukaaa tena kwa amani zote ntamwomba Mungu anipe amani

mwanamke huyu ana mdomo it seems sooo

kitanda hakizai haramu tena ashukuru ameambiwa wengne wanachepuka kimya kimya
amshauri mumwe alete huyo mke wale maisha

awe na upendo wa kashare ...japo inauma sanaaaaa
 
Naye ajaribu kutafuta ka Castle Lite Boy ajipime kama naye hana tatizo,,,,kiivyo tu!!
 
akubali kuwa mke mkubwa na mwenye mtoto awe mke mdogo, maisha yasonge mbele japo ataumia mwanzoni
 
bora aondoke tu maana, kitakachofata ni kumtesa mtotongwa tu....

Bora aondoke akalale na mwanaume mwengine anaweza pata mimbaa maana aya mambo yapo waeza ishi na mume miaka mingi bila mtu once mume au mke akitoka anapata mtoto
 
Back
Top Bottom