Swali fikirishi: Je, tunahitaji idadi kubwa ya watu ili kujikwamua kiuchumi au tunahitaji watu wenye tija kwenye uchumi wetu?

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
886
930
Angalizo: Mada hii haiwahusu wenye mtizamo wa kuijaza dunia katika mtizamo wa imani za dini.

Wakuu, bila kuwachosha naingia moja kwa moja kwenye mada. Kwanza, nikiri wazi kuwa mie si mtaalamu wa uchumi, bali ni mdau wa mambo fikirishi tu.

Nimekuwa nikisoma baadhi ya maoni ya watu wakisema eti nchi yetu ni kubwa sana hivyo inabidi tuendelee kufyatuana sana. Kwamba ina mapori makubwa sana yaliyo wazi kwahiyo inabidi tuzae sana ili kujaza hayo mapori. Wengine wameenda mbali wakitolea mfano wa nchi kama China na India kuwa uchumi wao unafanya vizuri kutokana na wingi wa watu walionao.

katika upande mwingine, nchi za Ulaya zina idadi ndogo ya watu lakini uchuimi wao unafanya vizuri sana. Katika muktadha huu, nisingependa kuhusianisha mada hii na concepts ngumu ngumu kama 'Population Density', ' Gross Domestic Product' (GDP)', 'Gross National Product' (GNP) wala 'Legacy ya Ukoloni' (Colonial Legacy).

Bali katika mjadala wangu uliojikita katika muktadha wa hoja ya kutokuwa na haja ya kuwa na idadi kubwa sana ya watu katika maendeleo ya uchumi, ningependa ku-focus ktk vitu rahisi sana kutazamika kwa macho ambavyo nimevishuhudia katika nchi zilizoendelea ukilinganisha na sisi tunaoelea kwenye dimbwi kubwa la umaskini kama ifuatavyo:

1) Nimeona watu waliopo Nchi zilizoendelea wakifanya kazi kama machine: Namanisha kuwa, kwa namna hawa jamaa wanavyofanya kazi, unaweza sema uchukuwe watu 10 katika nchi yetu ndio sawa na productivity ya mtu mmoja wa nchi zilizoendelea.

Hapa namanisha kuwa, ufanyaji kazi ktk nchi zilizoendelea hasa Ulaya na Amerika (Marekani na Canada) ni kwa mfumo wa working hours. Kwahiyo mtu analipwa kutokana na masaa aliyofanya kazi. Aisee, hawa jamaa wanamanisha inapokuja suala la kufanya kazi kwa masaa.

Wazee, yaani kama ni muda wa break ni break, na kama ni muda wa kazi ni kazi kweli (unakuta hata huwezi kutumia simu wakati wa kazi). Sio kama Bongo unakuta mtu anafanya kazi kwa kujivuuta, yaani siku nzima ka-deliver kitu ambacho kingefanywa na mtu wa Ulaya kwa li-saa limoja tu.

2) Hawa jamaa buana wanajua kutumia nguvu kazi vilivyo. Yaani unakuta kwa mfano, gari ya kusafirisha mizigo ina mtu mmoja ambaye ndiye driver, na ndiye mpakiaji na mtoa mizigo kwenye gari.

Yaani kiufupi kupakia hadi kupakua mzigo anafanya mtu mmoja (japo wanatumia simple machine kuwarahisishia kupakia na kushusha mizigo), ila naamini ingekuwa bongo hapo kungekuwa na driver, msaidizi wake na vibarua wengine wasiopungua wanne.

3) Kwa mazingira hayo wakuu, ndio maana unakuta hata malipo yao yanakuwa mazuri. Yaani kwa kazi tu ya -udereva mtu anakula maisha vizuri tofauti na bongo. Ile pesa kwa bongo unakuta imegawanywa kwa watu wengiiiii ambao hata wakipewa haiwasaidii kulipa hata kodi ya nyumba.

4) Yaani hata ukienda Supermarket unakuta mtu mmoja kanunua mahitaji yake ambayo ingekuwa ni bongo ni sawa na bidhaa hizo zinunuliwe na watu karibia ishirini ndio ufikie kiwango cha mtu mmoja wa Ulaya.

Sasa ndugu zangu, hii inaonesha wazi kabisa kuwa, yaani kazi ya mtu mmoja wa Ulaya kwa siku ni sawa na kwamba imefanywa na watu 10 wa Afrika/Bongo. Kwahiyo kwa hesabu rahisi ni kuwa idadi ya watu milioni 1 kwa Ulaya, productivity yao ni sawa na watu milioni 10 kwa Afrika.

Kwa muktadha huu ndugu zangu, sisi tunahitaji watu wengi ili kuendelea kiuchumi au tunahitaji watu wachache tu ambao watakuwa na impact kubwa kwenye uchumi wetu?

Yaani sisi unakuta tuna utitiri mkubwa wa watu ambao kazi yao kubwa ni betting, bodaboda, kuuza karanga, kuuza soksi na vitu vinavyofanana na hivyo. Yet, tunajisifia kuwa tunawatu wengi na bado tunauhitaji wa watu wengi zaidi.

Hapohapo ukumbuke jinsi idadi kubwa inavyokuwa mzigo mkubwa katika utoaji wa huduma za kijamii ktk nchi maskini. Kila siku idadi ya vyoo na madarasa hayatoshi. Madawati ndio usiseme kabisa. Bado watu wanazaliana eti unakuta familia moja, baba kazaa watoto 7 mpaka 8. Yaani hata chupi tu mazazi wake hawezi kununua na bado anataka tuendelee kufyatua.

Ningelikuwa kiongozi mwenye dhamana ningefanya yafuatayo:

1) Ningehamasisha mpango bora wa uzazi ili watu wazae watoto angalau wawili tu kila familia. Ili kufanikisha hili ningetoa incentives kwa watu wanaozaa watoto wachache. Matangazo ya uazazi wa mpango yangeenea kama yalivyo matangazo ya betting.

Yaani kila kona zingesikika sauti za uzazi wa mpango. Ningehamasisha kampeni hii angalau kuanzia sasa hadi miaka 20 ijayo kisha nione impact yake kwenye uchumi wetu.

2) Ningewaonesha wananchi kwa dhati kuwa ninachukia ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya pesa ya umma. Ningepunguza matumizi yote ya Serikali yasiyo ya lazima kama posho za wakubwa wote, mishara yao, kupunguza ununuzi wa magari ya kifahari, n.k.

3) Kwa kufanya namba 2 hapo juu hivyo wananchi wengi wangeanza kurejesha imani yao kwa Serikali na wangeanza kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi kwa hiyari yao. Hivyo makusanyo ya kodi yangeongezeka kutokana na watu kufanya kazi kwa bidii na kulipa kodi na uchumi wetu ungepaa juu.

4) Ningeboresha mfumo wa elimu na kutoa ufadhili kwa vijana wanaopenda kusoma mafunzo kwa vitendo kupitia VETA na vyuo vingine vya kati ili kuzalisha vijana wengi wenye ujuzi.

5) Ningeboresha mazingira bora ya uwekezaji kwa kuwavutia watu wenye mitaji mikubwa waje wawekeze kwenye shughuli ambazo zingetengeneza ajira kwa wingi na kuwafanya vijana wengi kufanya kazi na kuboresha uchumi wa nchi.

6) Ningewaagiza na kuwawezesha wataalamu wa uchumi na wengineo (walio ndani na nje ya nchi) walete mawazo yao ya kitaaluma ya namna gani ya kuboresha uchumi wa nchi yetu. Kiufupi maamuzi yangu asilimia kubwa yangefanyika kutokana na tafiti za kitaalamu.
 
Uchumi wa nchini hautokani na wingi wa watu bali watu wenye ujuzi wa kuzalisha ndio ukuza uchumi wa nchi. Kuwa na population kubwa lakini ipo iddle haizalishi, haitumii huwezi kuza uchumi. Nchi yetu still wengi wanaishi for free bila kuzalisha. Unakula kwa Shemeji, vijijini kuni, maji, mboga bure, kuoga bure, ununui umeme, vocha, nk. Bado yapo maisha sio lazima ukutane na hela ndipo uishi.
 
Simple answer! Scandinavian countries are in the First World Group, rich countries, very rich. what is the population of these countries?

Screenshot 2023-05-03 151656.png
 
Kuhusu swala idadi ya watu na maendeleo binafsi Nakuunga mkono ni Bora uwe na idadi ndogo ambayo ina tija kuliko ilivyo sasa watu shazi lkn matokeo hakuna
 
TANZANIA au afrika hatuna shida ya population kwa mgawanyo wa eneo KWA mraba. Tatizo lililopo ni uwiano Mdogo Kati ya matumizi ya raslimali zilizopo na idadi ya watu.

Raslimali zisizotumika ni nyingi kuliko nguvu kazi isiyotumika.
 
Wao mifumo yao inawabeba kutimiza ndoto zao sisi ni mifumo ni kikwazo kinachokuvuta nyuma usiendelee kwa malengo ya kisiasa zaidi
 
TANZANIA au afrika hatuna shida ya population kwa mgawanyo wa eneo KWA mraba. Tatizo lililopo ni uwiano Mdogo Kati ya matumizi ya raslimali zilizopo na idadi ya watu.
Raslimali zisizotumika ni nyingi kuliko nguvu kazi isiyotumika
CC: Mawaziri wote wanaohusika na hili. Maaana tunaambiwa JF inasomwa na hao waheshimiwa watunga sera pia. Ningetamani mjadala kama huu ungeingia ndani ya Bunge.
 
watu ni mtaji pia. Suala la ufanyaji kazi kwa tija ni suala la mwenye kazi yake atakavyotaka iwe na asimamie
Nenda sector binafsi, watu wanafanya kazi kama ulaya tu
serikalini ndo vitu haviendi-hakuna motisha. ufanye kazi usifanye mshahara wako upo palepale
 
Wingi wa watu bila akili haisaidii kitu.

Kuna nchi jirani zinatuzidi sana na hawana watu wengi kama sisi ila wana akili kutuzidi

Sisi sio wehu ila kuna asilimia mdogo ya watu ndio majizi makubwa ambayo yanajua kabisa wao ndio chanzo cha yote haya

Hayo mapori yako tupu ila ukiomba ekari 1000 uanzishe mashamba makubwa huwezi kupewa na badala yake watakuambia hiyo ni hifadhi ya taifa

Yaani kila ardhi kubwa hata kama kuna kenge tu wanakuambia ni hifadhi

Akija mwarabu wa UAE au muzungu anapewa bila masharti kwa kujua kuwa wameishakula rushwa na wako tayari kuuwa watu ili wapishe

Mkuu hata ukiwa muadilifu kiasi gani kama uko peke yako na ukaanza kupunguza matumizi ya majizi haya yaliopo serikalini yatakuuwa kwa kuingilia milo yao
 
Yani hawa watu tulionao hatujui kuwatumia, wanalalamika hawana kazi, halafu tuongeze wengine kwa makusudi ili iweje?

Yani hapo umekuwa sawa na ntu ambaye hana wazo la biashara, kaomba mtaji, kapewa, anaomba mtaji zaidi.

Wakati hata mtaji aliopewa awali hajautumia vizuri na hana idea akiongezewa mtaji atafanya nini.
 
Angalizo: Mada hii haiwahusu wenye mtizamo wa kuijaza dunia katika mtizamo wa imani za dini.

Wakuu, bila kuwachosha naingia moja kwa moja kwenye mada. Kwanza, nikiri wazi kuwa mie si mtaalamu wa uchumi, bali ni mdau wa mambo fikirishi tu...
Hili mbona halina mjadala? Watu wengi bila mipango ni kukaribisha umaskini. Haya ni mafundisho basics sana tena ya msingi na sekondari. Siku hizi hawafundishi?
 
Population control imefeli afrika sababu ya nature ya waafrika.

Ukiwa iddle ni lazima utawaza ngono tu kama starehe nyepesi. Hakuna mifumo inayotubana tufanye Kazi Ili tuishi wajomba ni wengi tofauti na ulaya Mjomba ni akili yako.

Kama tusingedai UHURU tungekuwa na mifumo ya maendeleo kama wao ambayo ingepunguza gap la umasikini, KWA maana tungekuwa na middle income wengi zaidi kuliko masikini
 
Hata uwachukue malaika kwa mifumo yetu hawawezi toboa watakutana na vikwazo toka KWA wanasiasa. Utashhi wa Siasa Ina nguvu kuliko taaluma.

Wataalamu wengi tu watanzania toka nje wamefeli na iddle zao walipokuja bongo
 
Angalizo: Mada hii haiwahusu wenye mtizamo wa kuijaza dunia katika mtizamo wa imani za dini.

Wakuu, bila kuwachosha naingia moja kwa moja kwenye mada. Kwanza, nikiri wazi kuwa mie si mtaalamu wa uchumi, bali ni mdau wa mambo fikirishi tu...
Idadi kubwa ya Watu ni muhimu sana tena sana
 
Population control imefeli afrika sababu ya nature ya waafrika.
Ukiwa iddle ni lazima utawaza ngono tu kama starehe nyepesi. Hakuna mifumo inayotubana tufanye Kazi Ili tuishi wajomba ni wengi tofauti na ulaya Mjomba ni akili yako...
Wewe ndugu ulipaswa ndio uwe mvaa suti na ukae kwenye kota za watunga sera. Inamana viongozi wenye dhamana wana upofu wa kutotambua mawazo haya?
 
Yani hawa watu tulionao hatujui kuwatumia, wanalalamika hawana kazi, halafu tuongeze wengine kwa makusudi ili iweje?

Sent from my SM-S908U1 using JamiiForums mobile app
Bwana Kiranga haya yalishapatiwa majibu wakati wa kipindi cha awamu ya kwanza cha Nyerere. Kulikuwa na kampeni kabambe ya kuzaa kwa mpango na kulikuwa na chama kinaitwa UMATI (uzazi wa mpango Tanzania).

Haya mambo karibu kila mwananchi alikuwa anayajua ila nashangaa wasomi wa siku hizi wanaturudisha tena nyuma miaka ya 60 na 70.

Ni yule mjinga Magufuli aliwamwagia sumu na kwa sababu nchi yetu imejaa nyumbu watu wameanzisha tena mijadala.
 
CC: Mawaziri wote wanaohusika na hili. Maaana tunaambiwa JF inasomwa na hao waheshimiwa watunga sera pia. Ningetamani mjadala kama huu ungeingia ndani ya Bunge.
Viongozi hawapo kwa ajili yako, afrika uongozi ni ajira binafsi na sio wito wa kuipigania jamii, thus mifumo yetu ya sheria inawaogopa au ni butu kwa Wala rushwa na mafisadi
 
Back
Top Bottom